Kuna jamaa yangu wa mkoani aliagiza kiatu duka fulani sinza akaniomba nikifuatilie nilipie nimtumie, bei ilikuwa 170K. Akantumia picha nikapita k/koo nikakitafuta nikakipata kwa 75K.
Ikapita wiki baada ya kukipata jamaa yake nae akakipenda na kuagiza alikuwa na shughuli na ilikuwa jpili, k/koo jpili kumepoa sana nikakitafuta nikakikosa ikabidi niende sinza kuchukua kile cha pichani ili mwamba afanikishe jambo lake, hicho cha sinza kilikuwa kimekaa sana dukani hadi kimepoteza mvuto ila bei juu. Faida ni kubwa na hapo ni kwa bei y Rejareja.