Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
This is mature argument.Hii nchi kuna mambo mengi hufanyika bila kufikiria mbele. Leo tunakimbizwakimbizwa kwa ajili ya kitambulisho cha NIDA. Lakini kwa mujibu wa sheria ya utambulisho wa uraia, kadi/namba ya NIDA ndio kithibitisho pekee halali cha uraia wa mtanzania; yaani aliyesajiliwa NIDA ndo anatambulika kisheria kuwa ni raia wa Tanzania.
Wakati NIDA hutumia alama za vidole (fingerprint) katika kusajili raia, juzi tu hapa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imetanganza kufanya maandalizi ya kuanzisha kanzidata ya taifa ya vinasaba (National Centre for Human DNA Database). Kanzidada hii itatumika katika utambuzi wa watu/raia na kwamaana hiyo kanzidata hii itaunganishwa na za mamlaka zingine hasa zile za NIDA kuboresha utambuzi wa raia.
Biometria ya alama za vidole (fingerprint) inayotumiwa na NIDA ina mapungufu ukilinganisha na ile ya vinasaba (DNA fingerprint). Mathalani, fingerprint haiwezi kuonesha uhusiano (unasaba) wa ndugu wa karibu (closely related individuals). Zaidi, fingerprint haiwezi kutumia sampuli ya mwili ulioharibika kubaini utambulisho wa mwenye huo mwili au ndugu yake wa karibu.
Ingawa fingerprint ni biometria ya haraka, isiyo na gharama kubwa na haihitaji mtaalamu katika ukusanyaji wake, haikupaswa kutumiwa na NIDA kutokana na udhaifu wake kama ulivyooneshwa hapo juu na badala yake mamalaka hiyo ingetumia DNA profiles za watu zitazoandaliwa na GCLA. Hii ni kwasababu moja ya masharti ya NIDA ni muombaji usajili kutoa uthibitisho wa "makaratasi" kuonesha uraia au asil ya wazazi wake kwasbabu makaratasj hayo yanaweza kuwa na taarifa za uwongo hata kama zinatolewa na mamlaka halali kama vile RITA au Mahakama/Wakili.
Wasiwasi uliopo ni kwamba hapo baadae kutakuwa na usumbufu kwa raia kwasabu kanzidata ya DNA profile zitakazozoandaliwa na GCLA zitakinzana na taarifa za uhusiano (nasaba) za mzazi na mwanawe zinazokusanywa leo na NIDA kwa kutumia ushahidi wa "makaratasi". Je, ikitokea DNA profile ya raia X hairandani na ya mzazi wake (raia Y) aliyemtaja kwenye taarifa za NIDAQ
Utaandika sana kutetea lakini nakuhakikishia kuwa hakuna taarifa mpya katika usajili wa NIDA ambayo haikuhusika kwenye passport au leseni ya udereva. Naona unajaribu kusisitiza "nguvu" ya cheti cha kuzaliwa katika kuthibitisha uraia, lakini kumbuka kwenye cheti hicho kuna maandishi madogo yanasmomeka "cheti cha kuzaliwa sio uthibitisho wa uraia".
Kwa taarifa yako affidavity hutumika pia na NIDA kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa kwa mtu asiye nacho. Lakini unaposema postal code si lolote bali ni anwani ya makazi ambayo kwenye kwenye fomu za maombi ya passport pia huhitajika.
Shukrani mkuu, nakuunga mkono 95% hoja yako.