Sijui kama unajua utaratibu wa kupata passport mpya?!
Huwezi kupata bila kitambulisho cha taifa.
Passport ya zamani ilikuwa inatolewa bila kukidhi vigezo vya cheti cha kuzaliwa maaana walikuwa wanapokea hadi affidavit ambayo nimeeleza udhaifu wake.
Jambo jingine hizo passport za zamani kulikuwa na mapungufu ya ukusanyaji taarifa za anuani za makazi.
Hakukuwa na kigezo cha kuweka nambari au kitalu cha nyumba unayo ishi.
Hiki kitambulisho cha NIDA kimekuja kuunganisha na utambuzi wa anuani za makazi ktk mfumo wa Postal code, ndio zile namba nne za mwisho za kwenye kitambulisho cha NIDA.
Nadhani kwa haya machache utakuwa umeelewa na kujifunza kitu.
CC:
Pascal Mayalla ,
My Son drink water TUJITEGEMEE