Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

This is mature argument.
Shukrani mkuu, nakuunga mkono 95% hoja yako.
 
Mkuu lazima kuwe na mahali pa kuanzia hiyo nia njema.
Wewe umekuja na hoja nyingine nzuri sana ya DNA, na vizuri umesema mwenyewe DNA ni gharama kubwa kuliko fingerprints.
Na hali yetu ya kiuchumi unaijua ukizingatia gharama za kupima au kuchukua cha sample za DNA kwa kila raia.

Lazima tuwe na via umbel na tujikune tunapofikia.
 
Kaka huwa unasafiri kwenda vijini? Unaufahamu ukubwa wa hii nchi na umbali wa baadhi ya vijiji kutoka wilayani?
 
Kaka huwa unasafiri kwenda vijini? Unaufahamu ukubwa wa hii nchi na umbali wa baadhi ya vijiji kutoka wilayani?
Kaka miaka zaidi ya miaka 40 unashindwa kwenda wilayani mara mbili tu kufuatilia cheti cha kuzaliwa?
Kama unaweza kumiliki simu unakosa nauli ya bodaboda ya kwenda na kurudi mara mbili tu ktk miaka angalau 5 tu?

Wale masikini wasiokuwa na uwezo wa kununua hata simu siwalaumu inawezekana kukwama nauli.
 
Hata yeye hajui kinachotafutwa; labda kwa vile hakuweka tu alama ya kuuliza mwisho wa maneno aliyoandika.
Lakini hoja yake inajieleza vizuri nawe ungeelewa kuwa hata yeye hajui kinachotafutwa. Kisingekuwepo kinachotafutwa haya yanayofanyika yasingekuwepo.

Sasa kama wewe unajua, eleza, na sio kumuuliza anayetafuta jibu.

Kama huna jibu juu ya hilo, labda tueleze gharama zinazoambatana na usajiri huu. Kila sehemu iliyohitaji alama za vidole, watu wamesajiriwa kwa gharama kadhaa, na sasa gharama juu ya hizo inaendelea kurundikwa. Je huu sio ufujaji wa mali?

Au kuna hela ya uchaguzi inatafutwa hapa? Hili ni swali, kama una jibu unaweza pia ukaeleza.

Kwanza gharama zote hazijulikani tokea huko mwanzo. Hizi zitatangazwa tujue ni kiasi gani kimetumika katika zoezi la marudio yale yale yaliyokwishafanyika?
 
Naunga mkono hoja
P
 
hapo taget ni wapiga kura tu
 
CCM imetiliya mkazo ili ipate kuiba kura tu.
 
ukiwa huna ID hupigi kura hapo ndio CCM wanapopataka.
 
Mzee bongo mambo yote ni ya siasa hakuna jambo ambalo halihusu siasa CCM ni siasa kwenda mbele wao wanalolijuwa ni kubaki madarakani kwa vyovyote tu
 
Hili suala la simcard limethibitisha tusivyo na akili za kusolve matatizo yetu...
Hivyo nakuunga mkono kama umelifikisha mahakamani
 
technically ni wakati wa kupeana mrishonyuma. Mahakamani umeenda kufungua kesi?
 
technically ni wakati wa kupeana mrishonyuma. Mahakamani umeenda kufungua kesi?
Kinachoendelea kwa Sasa Ni uhakiki wa taarifa kuendana law amendment iliyopitishwa na bunge tarehe 6 September 2019 ya sheria namba 306 ibara 93 ibara ndogo ya 2 inayomtaka kila mtoa huduma ya mtandao kuhakiki taarifa za mtu waliyemmilikisha SIM card,
 
Na sheria haisemi wazi Kama Ni taarifa za nida, vivyo mie bado naamini taarifa Ni zile kulingana na jedwali namba 4 la sheria mama, hivyo kufungua sim card simply hakuna taarifa za nida naona sio sahihi
 
Technically alisema ana mawakili "elfu" na leo Jumatatu atafungua kesi dhidi ya serikali kwa kuwafungia laini za simu ambao hawajasajiliwa kwa namba za NIDA. Ndio namuulizia. Wewe una taarifa zozote za technically kufungua hiyo kesi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…