Unaweza kujiuliza maswali 200,na usipate jibu hata moja juu ya taifa la Tanzania hasa watu wake.
Hivi hawa ni Binadamu kutoka sayari hii ya Dunia au ni viumbe kutoka Planet X?
Binadamu aliyekamilika ni lazima awe na kumbukumbu za kutosha juu ya kila Tukio analopitia.
Tanzania hii hakuna tena anayekumbuka juu ya vitambulisho vya kupigia kura na Driving Licence kuwa vyote vina mfumo wa Biometric (unaohifadhi alama za vidole).
95% ya Watanzania wana vitambulisho vya kupigia kura vyenye mfumo wa Biometric sawa tu na Vitambulisho vya Taifa, lakini leo hii eti hivyo Vitambulisho havitakiwi kusajilia line za simu hadi viwe Vitambulisho vya Taifa.
Eti lengo ni kudhibiti uhalifu, sasa binadamu mmoja ana fingerprints ngapi kama ID za kura ambazo pia zilipatikana kama Vitambulisho vya Taifa kwa njia hiyo hiyo ya alama za vidole leo tena havifai?
Wenye akili wameshasoma mchezo, kuna kitu kinatafutwa hapo, kwa sababu fingerprints tayari watu walishachukuliwa kwenye Vitambulisho vya kura na Driving Licence, sasa kuna haja gani ya kutesa watu kiasi hiki?
Details za kila raia na fingerprints zake zipo Tayari kupitia Vitambulisho vya kura. Taifa lenye mamilioni ya wajinga wamesahau kuwa information zao zilishachukuliwa na fingerprints pia.
Neno la Mungu katika Kitabu cha Mithali linasema "Mwanangu mtafute sana Elimu na wala Usimwache aende zake”.
Poleni Watanzania.
Sent using
Jamii Forums mobile app