Iko hivi,hakuna ndoa inayovunjika halafu ukataka kuingia katika mahusiano mapya bila ya hasa kujua ni nani kati yenu alikuwa mkosaji,najua nikikuuliza hilo swali utasema yeye ndio alikuwa na makosa,ila inawezekana kabisa wewe ndio ulikuwa mkosaji,kuna vitu ulivianzisha vikamfanya yeye kubadilika.Sasa kama una uhakika kweli kuwa yeye ndio alikuwa na makosa,ingia kwenye hiyio ndoa ila kama umetafakari na kujua wewe ndio ulikuwa na makosa unatakiwa ubadilike,maana huko unakoenda kama utaingia na gia zilezile ulizo tumia kule uhusiano utavunjika tena,na huyo unaemwita mpole akakubadilikia kuliko hata yule wa kwanza...