Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Haiwezekani iwe wanaume Tu ndo Wana shida ...na wewe je?
Umerekebisha kasoro zako?
Au bado unaamini " uko perfect" ?
Hukuwa na shida kabisa?...
Kasoro zako unazijua na umezifanyia kazi ...au ni mume na familia yake ndo Wana 'matatizo "wewe huna kabisa?
Tatizo huanza mdogo mdogo".........si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane......"

Akae atulie tuu alee familia yake kwa amani - hana uhakika ka baba wakambo atawapenda wanae 2 wakisha fika 18 yrs ndo atafte mzee mwenzie wayajenge. Halafu uje ukute waloachana nae anatuma matumizi ya watoto - kisiri siri.
 
Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma...

Kuna pointi moja ya muhimu sana umeiandika ila mbele ukaifukia fukia, mimi naihighlight..

''The sacrifices are not worth the thing''

Sacrifice unayozungumzia ni submissiveness..

Naomba kuuliza, ku submitt huwa ni sacrifice kubwa sana kwenu?
It is.
Kuwa submissive inatuchukua nguvu kubwa mno ndani yetu, namaanisha ile kuwa submissive toka ndani kabisa.
Hasa kwa mwanamke wa umri wangu, pengine maisha yameshakuwa defined kiasi zaidi ya ukike wa asili ambao yes unahitaji mwanaume, huna sababu nyingine ambazo wengi zinawafanya wanakuwa submissive.

Kwa hiyo kiukweLI kabisa kabisa!
Inatugharimu, na gharama yake ni kubwa zaidi ya kusema ''Ndio Mume Wangu''
Sasa ili hii ndio mume wangu niipractise kwa uhalisia kwa kumaanisha kuna vitu vingi mno mno vinapaswa kuwa ok.
ili yes, nisema well shoulders down, laying powers and all.
Take the lead, bila kujutia bila kujihisi unyonge bila kuona unanyanyasika.
It is sexy being submissive to my man, BUUUUT he shuld earn i!

Hapo kwenye kuearn it ndo kuna KIMBEMBE!
 
Dakika za jioniiii sana, Kataa Ndoa wanapata goal la kusawazisha hapa, haha
Kwanza pole sana, pili you need a psychological counselling na within time frame kama ya 3 month utakaa sawa nadhani. Mathalani ushafikia stage ya kuweza ku share free kama hivi what your fear is, you are nearly there to be okay. Ukikosa a therapist wa huko karibu na wewe unapokaa, PM me nikusaidie, it was my major during my undergraduate studies, i will help you for free. Pole na karibu.
 
Yes asitafute mtu ambaye hajawahi kuingia ndoani
Watu wengi wanaoingia ndoa za pili hupuuzia vitu vingi kwenye ndoa za pili.
Mostly pengine ya haraka kuonekana wamemove on na hawakuwa na tatizo kwenye ndoa za mwanzo na aliyekuwa mwenzi wake ndo mwenye tatizo!
So kuna kupuuzia kwingiiiii.
Ila mwanamke mwenye watoto wawili tayari, aliyewahi kuolewa , kuolewa na kijana ambaye hajawahi kuoa wala kuwa na watoto!
Aiseee ni changamoto zaidi ya sana!
t
 
wala hata usichelewa kupokea baraka hiyo Takatifu ya ndoa ikiwa umeiomba kwa muda mrefu.

Na bilashaka,
ndani ya maombi yako, ulimlilia Mungu sana, na ulifungua maskio ya Moyo wako ukaskia maelekezo na wito wa Mungu kwamba huyu hapa ubavu wako 🐒

usiogope,
Kwa Neema na Baraka za Mungu ingia kwenye ndoa ukiwa na amani na imani kwamba mengine Mungu atakuonyesha ukiwa ndani na atakufanyia wepesi na kuonyesha njia na nuru palipo na giza 🐒

Mpendane msichokozane, amani ya bwana iwe ndani yenu...
Hakuna NDOA ya pili huo ndio Ukweli, mke na mume ni mwili mmoja, (i.enyama moja na mifupa mimoja) hu undugu wa nyama katika nyama yangu na mfupa katika mifupa yangu yaani mke na mume haiwezi kutenganishwaa kamwe hapa duniani kinachowatengasha ni kifo t
 
Yeah,nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili,nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu[emoji24]

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu[emoji1431]
Jiangalie/jitathimini wewe na ujikubali, Inawezekana wewe ndio changamoto bila kujua, ikiwa hivyo usiingie
 
Mahusiano ya kimapenzi ni sehemu nyeti sana ya maisha ya mwanadamu na ndipo sehemu kubwa ya Maisha hufanyika au ni muda mwingi huwa tunatumia katika kufanya maisha yetu.

Kuna watu wanaopata nafasi ya kupata mahusiano ya kudumu muda mrefu ambayo huwapa nafasi ya kuambatana na mtu m'moja katika maisha ya ujana hadi uzeeni.

Ila hili swala halipo kwa kila mtu. Kwa wengine mahusiano ya kudumu ni ndoto ya kusadikika na hakuna matarajio ya kuyapata kwa sababu mbali mbali.

Leo nitaweka sababu kwann kuna watu hawana bahati au fursa ya kufurahia mahusiano ya muda mrefu na kudumu na wenza kwa uaminifu na kuwa na amani ya mahusiano hadi uzee.

Zifuatazo ni sababu kwann kuna watu hawafanikiwi kimahusiano:

1. Malezi ya mzazi m'moja: hapa niwe specific, malezi ya kulelewa na mama tu, hufanya kijana au binti kuona mapenzi ni pahala pa kupita tu ila maisha ni mtu kuwa mwenyewe. Kama ni mtoto wa kiume then kumuona mama bila baba ina mnyima nafasi ya kuelewa namna ya kumtreat mwanamke na hivyo kufeli kujua namna ya kuishi na mwanamke na kujua wajibu wa mume kwa mke.

Kama ni mtoto wa kike kuona Mama akipambana mwenyewe inampa sababu kuwa hakuna haja ya kuwa na mwanaume sababu mama hajawahi kuwa na mwanaume mimi nitaishije na mwanaume nataka kuwa kama mama.

2. Kutojifunza kutokana na makosa: kuna mtu makosa anayofanya kwa tabia zake kwa mwenza wake anahama nazo na kwenda nazo kwa mtu mpya. Kiburi hiki cha kuhisi yeye yupo sahihi huwa kinakuwa sugu na kumnyima nafasi ya kujifunza ili kujirekebisha. Matokeo yake kiburi kinakomaa na kuona mwenza anayekutana nae ndie mwenye shida kumbe yeye ndie tatizo.

3. Tamaa: kuna kuhitaji kitu na kutamani kitu. Mahitaji na tamaa ni vitu viwili tofauti. Mahitaji ni vitu ambavyo hatuwezi kuishi bila kuwa navyo ila tamaa ni vitu tunaweza ishi hata tusipopata. Kwa sasa watu wengi wamewekeza fikra kwenye tamaa na kutaka wenza wao wawapatie kile wanatamani hata kama kipo nje ya uwezo na hii huharibu maelewano. Kuendekeza tamaa si jambo zuri.

4. Poor Communication skills: kuna watu wamezaliwa na makuzi kama ya wanyama na hata pengine wasiwafikie wanyama katika kuwasiliana. Mtu anahitaji kitu badala ya kushawishi apatiwe anaweka vitisho, jeuri, mikwara, dharau, au mitego kuforce upande wa pili umpatie kitu ambao pengine hata hauna wazo kuwa kinahitajika. Ni ngumu sana kuishi na mtu asiyejua namna ya kuwasiliana na mwenzake.

5. Kuishi kwa mapokeo: hapa ni kuishi kwa kukopi mfumo wa maisha ya kizazi chako ulipotoka badala ya kutazama ni mazingira gani yapo sasa. Mfano, mtu anaclamisha kuwa wanaume ni providers kwa 100% na akikosa sio mwanaume halisi bila kutazama nyakati za sasa na miaka hiyo ni tofauti mambo mengi yamebadilika. Au mwanaume kudhani mwanamke anatakiwa kuwa mwoga kwa mume wake na kuishi kama paka na panya ndani bila kuwa best friends.

6. Kuishi double life: kuna watu wanaishi ila hawapo pale wanapoonekana kuwapo. Mfano mwanamke anakaa na kijana mwenye maisha ya kipato cha chini na huku anadate na mtu mwingine ambaye anamhitaji kwa sababu zingine, wizi wa mapenzi. Ni ngumu sana kuweza kusustain Maisha ya uhalisia kwa tabia hizi.

7. Matumizi mabaya ya muda: unatumiaje muda wako na mwenzi wako ina amua mnakuwa imara kwa kiwango gani. Kama unampenda utatengeza culture yenu itakayo wawezesha kufanya Maisha yenu kuwa simple kuishi pamoja na sio kuwa na mfumo wa Maisha ambao kuishi pamoja inakuwa ni vita au mzigo.

8. Kutofanya Psychological evaluation: ni vema kila baada ya muda kujitathimini kisaikolojia kama unakua au umeganda. Unakutana na mdada au mkaka wa miaka 25 au 26,27,28 au 30 ila mwenendo wake kitabia kwa wakati huo na alipokuwa miaka 22 ni sawa sawa. Hii inamaanisha huyu mtu hajifuatilii wala kujiboresha kiakili hivyo hakui. Mtu asiyekua kiakili ni ngumu kufanikiwa kimahusiano. Tabia zina athiri sana maamuzi ya mtu na mahusiano yake na wengine.

9. Uvivu: ni aspect inayoanzia kwenye fikra. Uvivu maana yake kwa kifupi ni kukosa msukumo wa kuwajibika kulingana na nafasi yako. Mtu mvivu huwa anaamini ana haki ya kufanyiwa yale anayoshindwa jifanyia hata kama ni wajibu wake. Mfano, wadada wengi leo wanalaumu wanaume kutowapa pesa za matumizi yao binafsi na kuamini sio watu sahihi ila ukweli ni kuwa wao wamerithi akili za umasikini tokea makwao na ndio maana wamezaliwa na sumu ya uvivu na kupenda kupewa vitu ambavyo sio stahiki yao. Ni ngumu kudumu na mtu kama wewe ni mvivu.

10. Kushindwa kuelewa purpose ya uwepo wako hapa duniani kwa kurejea maagizo ya MUNGU. Wengi mahusiano wanachukulia kama starehe kwa asilimia zote na kusahau majukumu na wajibu wa kuwapo katika mahusiano kwa misingi ya upendo, kujali, kujitoa, kupanga pamoja, kujenga pamoja, kutunzana, kuleta watoto, kuwalea kwa maadili, uaminifu, kuongoza na kutii. Nje ya hapa hakuna kudumu ni kupoteza muda.

Haya ni machache ila yapo mengi sana yanayochangia mahusiano ya sasa kuwa sehemu temporary ya kuishi huku mtu akingoja kwenda sehemu nyingine.
 
Hakuna NDOA ya pili huo ndio Ukweli, mke na mume ni mwili mmoja, (i.enyama moja na mifupa mimoja) hu undugu wa nyama katika nyama yangu na mfupa katika mifupa yangu yaani mke na mume haiwezi kutenganishwaa kamwe hapa duniani kinachowatengasha ni kifo t
kwan alikua kwenye ndoa au uchumba sugu 🐒

na ilikua ndoa ya dini gani, ya kimila au kiserikali 🐒
 
Ndoa ni ya watu wawili tu; muhimu mnaoamua kufunga ndoa muwe mnajielewa tu; ndugu hawatakiwi kuingilia mahusiano yenu, sisi kabla ya kufunga ndoa tulipata semina ya mwezi mzima, ingawa ndugu zangu hawampendi mke lakini sisi tunapeta tu, na tunapambana na uzao wetu.

Kwa sababu una watoto tayari, nachoweza kukushauri ni vizuri na huyo uliyenaye kwa sasa akiwa na watoto pia; au angalau awe amefikisha miaka 40+, nikimaanisha kwa mazingira hayo, atakuwa tayari ni mwanaume anayejielewa na aliyeamua kutulia kwenye ndoa.

Kwa kifupi tu; sisi wanaume huwa hatupendi watoto uliozaa na mwanaume mwingine, hii huwa inatutesa sana moyoni; muhimu katika mahusiano yenu mlijadili hili na mliweke sawa.​
 
Kama huyo Mwanaume ni mtu mzima (ana umri zaidi ya miaka 48) ningeshauri muendelee.

Ila kama yupo kwenye Rika la Ujana, ujue huyo atakufanya single Maza wa watoto 3 hapo baadaye.

Ukweli usemwe, hakuna Mwanaume atakayeweza kuoa Mwanamke single wa watoto wawili na yupo kwenye Rika la Ujana, Unless huyo Mwanaume ni mtu mzima ambaye pengine Mgane (Mkewe amefariki) na tayari naye ana watoto.

Sisi kazi yetu ni kushauri tu, ila mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe mwenyewe.

Wishing you all the best 🙏🙏
KABIIIIISA.
 
Yeah,nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili,nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
MITHALI: MLANGO 14

1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikonoy ake mwenyewe.

Kaa chini jikague NDANI yako (moyoni) b'se jukumu na mamlaka ya kujenga NDOA au familia au nyumba MUNGU aliyaweka kwa mwanamke Kwaiyo usihisi au kuona NDOA yako kuvunjika upo salama hapana This is wrongs thoughs unajidanganya mwenyewe 🙆🏻‍♂️

Ukikuta NDOA imevunjika ujue MWANAMKE amehusika kwa asilimia kubwa sana na nimatokeo ya MWANAMKE kutokujua NAFASI zake na mamlaka na uweza ambao amepewa na MUNGU kwaajili ya kusimamia na KULINDA kusudi la MUNGU (NDOA)😊

Mathayo 19.9
"Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu yau asherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini."

MUNGU muasisi wa taasisi hi ya NDOA hajatoa room yoyote wala sababu ya kuachana Kwaiyo kama unajihisi upo salama kwa NDOA yako kuvunjika kaa chini na ureview Mawazo yako NDOA kuvunjika ni mpango wa shetani na sio MUNGU

uasherati ni Kitendo cha kufanya tendo la NDOA nje ya utaratibu Yaani nje ya NDOA Kwaiyo aliposema isipokua kwa habari ya uasherati alimaanisha kwa watu ambao Bado hawajaunganishwa kwa NDOA takatifu mfano wa wachumba mmoja wao akitenda ngono hiyo ni halali kutengana Lakini sio kwa Wanandoa waliofunga NDOA takatifu

kwahiyo MUNGU hajatoa room au sababu ya Wanandoa kutengana haipo na afanyae hivyo na kwenda kuolewa au kuoa atakua anatenda uzinzi Hadi siku yake ya MWISHO na adhabu ipo kwa watu kwa wazinzi

ludi kwa mme wako ndugu yako wa nyama na mifupa huo undugu hauvunjiki kamwe
 
Yeah,nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili,nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
Dada To yeye, shida kubwa niionayo kwako, na kwa wanawake wengine pia, ni kumvisha mtu tabia ya mtu mwingine, hasa zile mbaya. Kwamba wa kwanza alitaka kukuuwa does not mean wanaume wote wanauwa..!!! NAdhani hata wewe huko Uyole na kwingine, umeshashuhudia ndoa zilizo safi. To me, olewa, maana umesema ile ya kwanza uliona dalili zote za kufosi kwenu. Kwa huyu wa sasa, umeona kuna kufosi?
 
Hapana Kaka ni moyo unamwitaji sema uoga tu wanisumbua
 
MITHALI: MLANGO 14

1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikonoy ake mwenyewe.

Mathayo 19.9
"Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu yau asherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini."

uasherati ni Kitendo cha kufanya tendo la NDOA nje ya utaratibu Yaani nje ya NDOA Kwaiyo aliposema isipokua kwa habari ya uasherati alimaanisha kwa watu ambao Bado hawajaunganishwa kwa NDOA takatifu mfano wa wachumba mmoja wao akitenda ngono hiyo ni halali kutengana Lakini sio kwa Wanandoa waliofunga NDOA takatifu

kwahiyo MUNGU hajatoa room au sababu ya Wanandoa kutengana haipo na afanyae hivyo na kwenda kuolewa au kuoa atakua anatenda uzinzi Hadi siku yake ya MWISHO na adhabu ipo kwa watu kwa wazinzi

ludi kwa mme wako ndugu yako wa nyama na mifupa huo undugu hauvunjiki kamwe
Amina
 
Back
Top Bottom