Swali zuri sana hii ndio shida ya binadamu tunapenda kujiona mainnocent tunapoelezea maisha ya mahusiano mbele ya jamii na kuona wenzetu wanamakosa hasa hii ipo kwa jinsia ya kikeHaiwezekani iwe wanaume Tu ndo Wana shida ...na wewe je?
Umerekebisha kasoro zako?
Au bado unaamini " uko perfect" ?
Hukuwa na shida kabisa?...
Kasoro zako unazijua na umezifanyia kazi ...au ni mume na familia yake ndo Wana 'matatizo "wewe huna kabisa?
Nakushauri ulee tu wanao, mwanamke huolewa mara moja tu na ataishi na mumewe hadi kifo kiwatenganishe (isipokuwa kwa sababu ya uzinzi) hakuna kuachana.Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.
Ni kweli mkuu Mungu anisaidieKama ni hivyo jitahidi u adjust kuendana na hiyo ndoa mpya.shida ni moja kubwa naiona kwako.
Hauna utayari hivyo utakata tamaa napema na kuachia ngazi pale inapotokea changamoto ndoani, maana sasa hivi kila ukiwaza moyoni unaguna mmmh!
wengi tunapitia hali hii
Barikiwa sana cute🙏🏽Dada mzuri binti kiziwi kampa ushauri mzuri.
Kwakuongezea tu...
Watu hawafanani! Kama wanapendana, na mahusiano yao na familia zao sio mabaya asijinyime raha kisa tu alipata bahati mbaya huko nyuma.
Olewa zako mwaya To yeye ufurahie maisha!
👍🤝👏📝Ninakuelewa na ninaona ni kwa nini hii hali inaweza kukutia wasiwasi na kuwa ngumu kwako. Kufanya maamuzi kuhusu kuingia tena katika ndoa, hasa baada ya kupitia changamoto kubwa katika ndoa ya awali, si jambo rahisi. Unaweza kufanya yafuatayo kukusaidia kufikia maamuzi yenye afya na yenye kujenga kwa mustakabali wako na wa familia yako:
Pata Muda wa Kutosha wa Kuponya na Kuelewa Yaliyopita: Kabla ya kufikiria kuingia katika uhusiano mpya, ni muhimu kuhakikisha kwamba umepata muda wa kutosha wa kuponya majeraha yaliyotokana na ndoa yako ya awali. Pia, jaribu kuelewa kwa kina kilichosababisha ndoa hiyo isifanikiwe ili kuepuka kurudia makosa yaleyale.
Usikimbilie Maamuzi: Jipe muda wa kufikiri na kutafakari kwa kina kuhusu uamuzi wako wa kuingia tena katika ndoa. Usijihisi unalazimika kufanya maamuzi haraka kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa wengine au hata mchumba wako mpya.
Mawasiliano na Uwazi na Mchumba Wako: Ni muhimu sana kujenga mawasiliano ya wazi na ya dhati na mchumba wako kuhusu hofu na wasiwasi wako. Kujenga msingi imara wa mawasiliano kutawasaidia nyote wawili kuelewa matarajio na mipaka ya kila mmoja.
Fanya Uchunguzi wa Pamoja na Ndugu: Kwa kuwa una wasiwasi kuhusu uhusiano na ndugu wa mume, ni vyema kufanya jitihada za pamoja na mchumba wako kujenga uhusiano mwema na familia yake. Hii itasaidia kujenga mazingira ya uelewano na kuepuka migogoro ya baadaye.
Tafuta Ushauri wa Kitaalamu: Inaweza kuwa na manufaa makubwa kuzungumza na mshauri au mtaalamu wa mahusiano ambaye anaweza kukupa mwongozo na msaada wa kitaalamu. Hii itakusaidia kuelewa hofu zako na kujifunza mbinu za kujenga mahusiano yenye afya na yenye furaha.
Fikiria Kuhusu Watoto Wako: Katika kufanya maamuzi yako, ni muhimu kuzingatia ustawi na hisia za watoto wako. Fikiria ni mazingira gani yatakuwa bora zaidi kwa ustawi wao wa kimwili na kihisia.
Sikiliza Moyo Wako: Mwisho, lakini si kwa umuhimu, sikiliza sauti ya moyo wako. Kama una hisia nzuri kuhusu uhusiano huu mpya na unaona kuna nafasi ya kujenga maisha yenye furaha na yenye kujenga pamoja, basi huenda ikawa ni jambo la kufikiria.
Uoga ni akili, Pamoja na Hilo uoga usitufanye tukaacha kufanya maamuzi huku tukizingatia tahadhariHapana ila kiuoga tu mkuu
Mliishi pamoja kwa muda gani, na mmeachana lini?Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....
Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.
Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭
Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.
Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
Hii ni point hana utayariKama ni hivyo jitahidi u adjust kuendana na hiyo ndoa mpya.shida ni moja kubwa naiona kwako.
Hauna utayari hivyo utakata tamaa napema na kuachia ngazi pale inapotokea changamoto ndoani, maana sasa hivi kila ukiwaza moyoni unaguna mmmh!
wengi tunapitia hali hii
Noo haya Maneno sio sahihi.Ndoa ngumu mkuu,Mwenyezi Mungu awapambanie sana.Asante sana
Ubarikiwe sana loveTo yeye ,,,,najua tumekuwa na utani wa kimapenzi humu ndani kama kuitana wapenzi na makopakopa lkn kwa ajili ya kufurahi tu na mwisho siku inapita.
Kwa roho safi kabisa nashauri kubali kuolewa na huyo mwamba nahisi ana roho nzuri kama yangu, na kama anapenda watoto wako hiyo ni point kubwa mno
Wakati mwingine tunakosa mambo mazuri kwasababu ya hofu zisizo za msingi, ishinde hiyo hali kwa kuamini kila kitu kitaenda kuwa sawa
Kama unaamini he is the one basi usiuweke usiku olewa na huenda ukaja kufurahia maisha ya ndoa ambayo hukuyapata hapo kabla
Nimekupa baraka zangu zote
Mpenzi wako wa zamani wa jf
Etugrul bey