Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Haiwezekani iwe wanaume Tu ndo Wana shida ...na wewe je?
Umerekebisha kasoro zako?
Au bado unaamini " uko perfect" ?
Hukuwa na shida kabisa?...
Kasoro zako unazijua na umezifanyia kazi ...au ni mume na familia yake ndo Wana 'matatizo "wewe huna kabisa?
Swali zuri sana hii ndio shida ya binadamu tunapenda kujiona mainnocent tunapoelezea maisha ya mahusiano mbele ya jamii na kuona wenzetu wanamakosa hasa hii ipo kwa jinsia ya kike
 
Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.
Nakushauri ulee tu wanao, mwanamke huolewa mara moja tu na ataishi na mumewe hadi kifo kiwatenganishe (isipokuwa kwa sababu ya uzinzi) hakuna kuachana.

Huyo mkaka unayemuona ni mpole hana makuu, mwema.... 😂😂😂 ni mwanaume kama yule aliyekuwa anakutwanga mangumi hadi ukamkimbia. Kwa kifupi hana tofauti na yule uliyamkimbia.

Kama una shauku ya kuwa na bwana, rudi tu kwa mumeo boxer, na ikiwa umechoka kutwangwa mangumi basi baki kuwa single lady ulee tu wanao.
 
Kama ni hivyo jitahidi u adjust kuendana na hiyo ndoa mpya.shida ni moja kubwa naiona kwako.
Hauna utayari hivyo utakata tamaa napema na kuachia ngazi pale inapotokea changamoto ndoani, maana sasa hivi kila ukiwaza moyoni unaguna mmmh!
wengi tunapitia hali hii
Ni kweli mkuu Mungu anisaidie
 
Ninakuelewa na ninaona ni kwa nini hii hali inaweza kukutia wasiwasi na kuwa ngumu kwako. Kufanya maamuzi kuhusu kuingia tena katika ndoa, hasa baada ya kupitia changamoto kubwa katika ndoa ya awali, si jambo rahisi. Unaweza kufanya yafuatayo kukusaidia kufikia maamuzi yenye afya na yenye kujenga kwa mustakabali wako na wa familia yako:

Pata Muda wa Kutosha wa Kuponya na Kuelewa Yaliyopita: Kabla ya kufikiria kuingia katika uhusiano mpya, ni muhimu kuhakikisha kwamba umepata muda wa kutosha wa kuponya majeraha yaliyotokana na ndoa yako ya awali. Pia, jaribu kuelewa kwa kina kilichosababisha ndoa hiyo isifanikiwe ili kuepuka kurudia makosa yaleyale.

Usikimbilie Maamuzi: Jipe muda wa kufikiri na kutafakari kwa kina kuhusu uamuzi wako wa kuingia tena katika ndoa. Usijihisi unalazimika kufanya maamuzi haraka kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa wengine au hata mchumba wako mpya.

Mawasiliano na Uwazi na Mchumba Wako: Ni muhimu sana kujenga mawasiliano ya wazi na ya dhati na mchumba wako kuhusu hofu na wasiwasi wako. Kujenga msingi imara wa mawasiliano kutawasaidia nyote wawili kuelewa matarajio na mipaka ya kila mmoja.

Fanya Uchunguzi wa Pamoja na Ndugu: Kwa kuwa una wasiwasi kuhusu uhusiano na ndugu wa mume, ni vyema kufanya jitihada za pamoja na mchumba wako kujenga uhusiano mwema na familia yake. Hii itasaidia kujenga mazingira ya uelewano na kuepuka migogoro ya baadaye.

Tafuta Ushauri wa Kitaalamu: Inaweza kuwa na manufaa makubwa kuzungumza na mshauri au mtaalamu wa mahusiano ambaye anaweza kukupa mwongozo na msaada wa kitaalamu. Hii itakusaidia kuelewa hofu zako na kujifunza mbinu za kujenga mahusiano yenye afya na yenye furaha.

Fikiria Kuhusu Watoto Wako: Katika kufanya maamuzi yako, ni muhimu kuzingatia ustawi na hisia za watoto wako. Fikiria ni mazingira gani yatakuwa bora zaidi kwa ustawi wao wa kimwili na kihisia.

Sikiliza Moyo Wako: Mwisho, lakini si kwa umuhimu, sikiliza sauti ya moyo wako. Kama una hisia nzuri kuhusu uhusiano huu mpya na unaona kuna nafasi ya kujenga maisha yenye furaha na yenye kujenga pamoja, basi huenda ikawa ni jambo la kufikiria.
👍🤝👏📝
 
Umesema vizuri, ndoa ya kwanza mliforce, na hii umeona penzi.
Usisite, olewa. Ukifika mtii mumeo, penda ndugu zake.
Wanaume hatufanani, tuvumilie, utii, weka mazingira safi, akiongea onyesha kuheshimu maoni/maelekezo yake hata kama unaona ni pumba, kisha kwa kutumia hekima mueleweshe kama unashauri usionyeshe kiburi!!
Hata ukiwa Kamanda wa Polisi au Kikosi cha Jeshi lolote lile, ukiwa na mumeo mpe heshima na hadhi yake.
Na Mungu akabariki ndoa yako mpya. BUT: Usiwasahau hao watoto wako, wape muda wao.
 
To yeye ,,,,najua tumekuwa na utani wa kimapenzi humu ndani kama kuitana wapenzi na makopakopa lkn kwa ajili ya kufurahi tu na mwisho siku inapita.

Kwa roho safi kabisa nashauri kubali kuolewa na huyo mwamba nahisi ana roho nzuri kama yangu, na kama anapenda watoto wako hiyo ni point kubwa mno

Wakati mwingine tunakosa mambo mazuri kwasababu ya hofu zisizo za msingi, ishinde hiyo hali kwa kuamini kila kitu kitaenda kuwa sawa

Kama unaamini he is the one basi usiuweke usiku olewa na huenda ukaja kufurahia maisha ya ndoa ambayo hukuyapata hapo kabla

Nimekupa baraka zangu zote

Mpenzi wako wa jf
Etugrul bey
 
Mwanzo atakupenda ila akishakutana na wadau watamuuliza kakubali vipi mechi ianze 2-0 na hajaonyeshwa kaburi la Ex baada ya hapo na yeye atatafuta panga kuja kukuchinja
 
Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
Mliishi pamoja kwa muda gani, na mmeachana lini?
 
Kaa nae mda sana mpaka uone upo tayari
Mpaka umekuja kuuliza huku ni wazi bado una maswali
Ulikosea mwanzo ukikosea tena ni uzembe

Ila mwanaume anaeshindwa kutenganisha ndugu na ndoa yake ndoa inakuaga na misukosuko sana…. Speaking from experience
Mi sijapambana sana na ndugu ila kuna namna niliamua kudeal tu na mume wangu,sasa hivi tupo ok kama asilimia 70 tu
Ila wakati tunaona aisee kila ndugu alikua anatoa opinion yake ina leta stress sana kwenye ndoa
Almost 7 yrs na naona kabisa mbali na sex naona ni rafk yangu wa karibu sana siezi tena kuachana nae

Utakapo fikia hatua ya kuingia kwenye ndoa usimtegee afanye kosa au kuangalia sababu kila mara,ambacho hupendi sema mapema na weka kila kitu kwa table before any major step…
Cha mwisho mi nikiachika/tukiachana siwezi tena kuolewa na wala sitotaka coz nikiangalia nyuma kiwango cha sh**t nilichotolarate sitaweza tena ukizingatia nishakua shangazi magonjwa ya utu uzima yasijenimaliza sababu ya mtoto wa mama mkwe
 
Kama ni hivyo jitahidi u adjust kuendana na hiyo ndoa mpya.shida ni moja kubwa naiona kwako.
Hauna utayari hivyo utakata tamaa napema na kuachia ngazi pale inapotokea changamoto ndoani, maana sasa hivi kila ukiwaza moyoni unaguna mmmh!
wengi tunapitia hali hii
Hii ni point hana utayari
Akishaupata wala hataitaji uzi kuleta
 
To yeye ,,,,najua tumekuwa na utani wa kimapenzi humu ndani kama kuitana wapenzi na makopakopa lkn kwa ajili ya kufurahi tu na mwisho siku inapita.

Kwa roho safi kabisa nashauri kubali kuolewa na huyo mwamba nahisi ana roho nzuri kama yangu, na kama anapenda watoto wako hiyo ni point kubwa mno

Wakati mwingine tunakosa mambo mazuri kwasababu ya hofu zisizo za msingi, ishinde hiyo hali kwa kuamini kila kitu kitaenda kuwa sawa

Kama unaamini he is the one basi usiuweke usiku olewa na huenda ukaja kufurahia maisha ya ndoa ambayo hukuyapata hapo kabla

Nimekupa baraka zangu zote

Mpenzi wako wa zamani wa jf
Etugrul bey
Ubarikiwe sana love
 
Back
Top Bottom