Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Yeah,nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili,nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
kamwonyeshe huyo mume mtarajiwa kaburi la mzazi mwenza wa watoto wako,la sivyo

Kamwonyeshe mume mtarajiwa kaburi la baba,wa watoto wako kwanza..ndio tuendelee na mipango mingine.
 
Sasa umeshasema kaka wa watu ni mwema hana makuu, kwanini unaogopa kuingia kwenye ndoa?

Jichanganye eti ni mwema halafu utaona moto wake utakuwa balaa hadi utaona aliyepita ana nafuu.
 
Tuliiva ila ndugu hawakuiva hawakutaka Kabisa tuoane mkuu...tukaforce na ndoa ikafungwa
Yaani ndugu anavunjaje ndoa ya watu wengine? Hii kitu huwa nashindwa kuelewa kabisa.

Huenda huyo mumewe wa zamani hana misimamo thabiti badala yake ni mtu wa kusikiliza ndugu na kufanyia kazi maelekezo yao.

Yaani mpendane kabisa halafu eti ndugu wasababishe mpeane talaka?

Big NO. Hata nyie hamkuwa na upendo wa dhati ndiyo maana ndugu wakawasambaratisha kiwepesi.
 
Si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane...

Sasa,mpaka inafikia kwenda kujitambulisha, na si wa kwanza, huoni we mdangaji! Kwamba wanakuwa waomba tu waoe,mbunye hawachakazi!!Ndoa ya nini sasa!!!
Unawadanganya kina nani! Mara ndugu,mara nini. Ndugu wanawapa kipato? Walikuwa wanawalisha?! Kama uliweza kuvumilia ukazalishwa,si ulishindwa kulea?
Sema anahitajika wa kukulelea watoto,maana wote hao unajisifu unaleta sababu mnaachana, si kweli. Kwa idadi hiyo ya watoto, single mother, huna ubavu huo,wanakuja tu kutua uzito,wakishakinai wanakuacha.
Ili upate msaada,nyoosha maelezo usipindishe kauli
 
Yaani ndugu anavunjaje ndoa ya watu wengine? Hii kitu huwa nashindwa kuelewa kabisa.

Huenda huyo mumewe wa zamani hana misimamo thabiti badala yake ni mtu wa kusikiliza ndugu na kufanyia kazi maelekezo yao.

Yaani mpendane kabisa halafu eti ndugu wasababishe mpeane talaka?

Big NO. Hata nyie hamkuwa na upendo wa dhati ndiyo maana ndugu wakawasambaratisha kiwepesi.
Bahati mbaya mhusika hayupo, ila utakuta huyu alikuwa na semina zisizoisha,ndugu walikuwa wakilazwa na yeye anaenda kuwauguza, mmewe akienda kuwajulia hali,alieambiwa amelazwa anamkuta shamba hana shida.
 
Ndoa ni taasisi nyeti Sana unapoamua kuingia ni lazima uwe umejiridhisha na uwe tiyari kuvumilia yatokanayo, shida ya wengi ni kwamba mke unaolewa lakini haujachanq na familia yako, na mme unaoa wakati huo haujachana na ndugu zako, mke akiwa ni wafamila nzima au mme akiwa ni wafamiliq nzima lazima itokee migogoro, na wengi wa chanzo cha ndoa kuvunjika ni ndugu, mwanaume mwenye akili zako unakubalieje kusikiliza mashitaka ya mke wako, mwanaume anapaswa kumlinda mke wake na mwanamke hivyo hivyo, lakini mkifungua milango kwenye ndoa yenu alafu kila mmoja ni msemaji wa ndoa yenu na nyinyi mnawasikiliza, hiyo ndoa haiwezi kudumu!!

Ushauri, kwa wakristo sisi ukishaolewa na ukaachika unapaswa ukae hivyo hivyo mpaka yule mme wako wa ndoa akifa utakuwa huru tena, vinginevyo ukiforce kuolewa tena, utakuwa unazini matokeo yake ni moto wa milele, hivyo basi kaa hivyo hivyo lea watoto wako
 
Ndoa ni taasisi nyeti Sana unapoamua kuingia ni lazima uwe umejiridhisha na uwe tiyari kuvumilia yatokanayo, shida ya wengi ni kwamba mke unaolewa lakini haujachanq na familia yako, na mme unaoa wakati huo haujachana na ndugu zako, mke akiwa ni wafamila nzima au mme akiwa ni wafamiliq nzima lazima itokee migogoro, na wengi wa chanzo cha ndoa kuvunjika ni ndugu, mwanaume mwenye akili zako unakubalieje kusikiliza mashitaka ya mke wako, mwanaume anapaswa kumlinda mke wake na mwanamke hivyo hivyo, lakini mkifungua milango kwenye ndoa yenu alafu kila mmoja ni msemaji wa ndoa yenu na nyinyi mnawasikiliza, hiyo ndoa haiwezi kudumu!!

Ushauri, kwa wakristo sisi ukishaolewa na ukaachika unapaswa ukae hivyo hivyo mpaka yule mme wako wa ndoa akifa utakuwa huru tena, vinginevyo ukiforce kuolewa tena, utakuwa unazini matokeo yake ni moto wa milele, hivyo basi kaa hivyo hivyo lea wa
 
"Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine."

Rekebisha hapo👆👆👆 halafu songa mbele.

Ukiwasikiliza ndugu sana hautafanya yako mema.

Kumbuka mchawi hatoki mbali bali ni huko huko kwenu.
 
Back
Top Bottom