Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Mara nyingi wanao fanya huo uamuzi,ni vijana ambao hawana kipato cha kueleweka.

Hivyo wanatafuta mwanamke mwenye kazi ili awe na uhakika wa hela..wapo wengi mnoo,walimu wanaingizwa mkenge sana,wanajikuta wamechukua mkopo kumchukulia huyo jamaa,badae anakula kona.

Walimu ni wahanga wakubwa.Nina shuhuda zisizo pungua tano,wadada wanataabika na mikopo baada ya wanaume kula kona.

Take care To yeye
 
Kama hajawahi kuoa
Kama hafanyi kazi /biashara yenye kueleweka
Kama hana watoto
Kama ndugu zake hawajui kama uliwahi kuolewa na una watoto
Kama huna kipato cha kumudu kulea wanao bila assistance ya baba yao

Wazo lako la kusita sita ni sahihi ukiliendeleza!
Uko sahihi sana!
 
Kabisa maana hawa viumbe kwa kutafta huruma hawajambo.....afu anajiona kidume eti wanangu wawili.....hakuna mwanaume mkorofi mbele ya mwanamke mnyenyekevu,,,,
 

Uko sahihi sana!
 
Pole sana kwa changamoto...Mambo ya uhusiano hayana formula wala ushauri ,maamuzi unayo wewe kulingana na mziki unaouona ,sisi wengine tutashauri vitu ambvyo hata hatujui vilivyo.
 
Hao watoto sio wake pekeake ni wa jamii,yake na ya mume wake....na hakuna wa kuwtenganisha watu ambao Mungu aliwaunganisha zaidi ya kifo.....tena mbaya zaidi huyu mwanamke kwa uchungu alionao juu ya huyo mume,ni dhahiri alimpenda mno,atakaye jichanganya hapo lazima ale za utosi
 
Pole sana,kwanilivyosoma nakuelewa unachangamoto zaidi ya ulichoandika basi uwe makini na shauri zetu maana tutashauri kulingana na tulivyovisoma hapa mathalani kuelewa, kwanza watoto hao watoto sio wako pekeeee
 
Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma...

Kuna pointi moja ya muhimu sana umeiandika ila mbele ukaifukia fukia, mimi naihighlight..

''The sacrifices are not worth the thing''

Sacrifice unayozungumzia ni submissiveness..

Naomba kuuliza, ku submitt huwa ni sacrifice kubwa sana kwenu?
 
Tuliiva ila ndugu hawakuiva hawakutaka Kabisa tuoane mkuu...tukaforce na ndoa ikafungwa
Ndugu wananafasi kubwa sana katika ndoa nivile tu tunaforuce kwakweli ,napitia the same story japo mm niwakiume ila kuforce force huku ,wakati ukijua kabisa danger signs zote za ndoa kua na misukosuko sijui nikipi hua kinatukuta....yaani unajua kabisa huyu sio sahihi ila bado unaamua kuoa
 
Hii ni mbaya sana,hamtoboi mkuu....inaumiza sana
 
Wanangu sipo nao mkuu
Kitu ambacho nilikuwa sipendi kitokee ni kuishi mbali na familia/watoto ingali niko hai. Nashukuru Mungu anaendelea kutia wepesi kwenye hili. Labda ikija kutokea niwe nisiwepo kabisa kwa mapenzi yake Muumba.

Ushauri:

Wanaume hatufanani kama ambayo wanawake hamfanani, ila ukipata mwanaume ambaye anataka familia kutoka moyoni na yuko tayari kusonga mbele, basi hapo hauna budi kuingia chamani.

Usiingie chamani kwa kuwa wewe ndio unataka ilihali mwezako yuko mguu mmoja ndani mwingine nje.

Sasa kazi ipo kumpata huyo atakayekuwa tayari kuwa na familia.
 
Pole sana,kwanilivyosoma nakuelewa unachangamoto zaidi ya ulichoandika basi uwe makini na shauri zetu maana tutashauri kulingana na tulivyovisoma hapa mathalani kuelewa, kwanza watoto hao watoto sio wako pekeeee
Ni kweli mkuu,asante sana
 
Kama huyo Mwanaume ni mtu mzima (ana umri zaidi ya miaka 48) ningeshauri muendelee.

Ila kama yupo kwenye Rika la Ujana, ujue huyo atakufanya single Maza wa watoto 3 hapo baadaye.

Ukweli usemwe, hakuna Mwanaume atakayeweza kuoa Mwanamke single wa watoto wawili na yupo kwenye Rika la Ujana, Unless huyo Mwanaume ni mtu mzima ambaye pengine Mgane (Mkewe amefariki) na tayari naye ana watoto.

Sisi kazi yetu ni kushauri tu, ila mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe mwenyewe.

Wishing you all the best πŸ™πŸ™
 
Amina,asante sana Mwifwa
 
Amina...Barikiwa sana mkuu...nimekuelewa
 
Asante sana mkuu,Barikiwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…