Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Space muhimu. Mi tumekuwa Maza anatupigia story kuwa kuna kipindi alikuwa anahisi M'dingi anamchukulia poa, basi anamtishia kuwa anataka kurudi kwao kupumzika, na mtu mzima anamuambia nenda. Baada ya wiki kadhaa anamfuata. 26+ years, and them old folks are going stronger. Space heals most of the time.
 
Shemeji ajifunze ku- appreciate juhudi zako aisee... kama uliyoyaandije ndiyo hali halisi unajituma sana. Hebu zungumzeni mvunje ukimya

Angekua anaongea malalamiko yake hata nisingekuwa nawaza ningeshajua wapi nakosea may be ndo vile tu binadamu haturidhiki, may be ataona umuhimu wangu nikiwa sipo
 
Hahaha gelofriend nimecheka huku hadi nimeshtua watu na sauti langu baya.

Hakuna kitu kizuri kama kujitambua unataka nini, hutokaa uyumbishwe na misimamo ya watu wa humu. Kuna watu kila kitu hawafanyi while in reality wanafanya hadi na nyongeza. Na kuna wengine hawafanyi kweli na mambo yako poa. Ila wewe usipofanya habari itakuwa nyingine kabisaaa, zubeda litakufata nyuma. Be you, do you coz hata tukijifanya kukushangaa kwani tunakupunguzia nini. Ahsante kwa kitchen party ya leo looh
 
Last edited by a moderator:
wanaume mara nyingi hawaridhikagi hata ufanye wema wa kiasi gani hata iweje hawana roho ya KURIDHIKA wao ni kulalama kama wamewekewa morta kwenye midomo yao yaani ni watu wa ajabu sana mm siwaelewi na sijui kwanini wao walikuwa wa
kwanza bora siye tungekuwa wa kwanza kuumbwa hakuna lolote ni lawama tu hao
 

Hapa sasa labda maombi katika akili yangu ya kibinadamu na kujitathmini kwangu naona Sina tatizo kwakweli mapungufu yapo ila sio kiasi cha kulalamikiwa
 
Mpendwa asikuambie mtu kwenye relation ukisikia tu habari za kupeana space tafuta pa kujiweka or join chama la mabachala hakunaga space kwenye mapenzi hayo ni matayarisho ya kuachana
Basi jaribu kubadilisha mbinu. Usipike, usifue, usimeze *clears throat*, kuwa gogo ukilala. Halafu uone. Asipoongea, then fanya maamuzi magumu au vumilia tu sasa.
 
usiwe kama yule jamaa wa kwenye biblia alimfuata yesu na kumwambia afanyeje aweze kuurithi ufalme wa mbingu yesu akamuuliza unatoa zaka, unashika sheria za torati na unafanya yoote mungu anayokutaka ufanye?...jamaa akaijibu ndio rabii kila kitu nafanya....yesu akamaliza mchezo kwa kumwambia "nenda kauze kila ulichonacho kisha unifuate"...jamaa akashindwa mchezo na kiaina akaupoteza ufalme wa mbingu...

back to your topic......umefanya vyooooote kwa mmeo. sasa nami nakupa moja tuu la kufanya ili uuteke moyo wa mumeo mpendwa.
KUTOKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA UTANDAWAZI.....MPE MMEO MTANDAO PENDWA WA WAZEE NA VIJANA NA AMINI UTAKUWA USHAUTEKA MOYO WAKE WOTE.
 
If it worked for your parents, doesn't guarantee kwamba na kwa ES itafanya kazi effectively. Aisee watafute tu alternative nyingine, mambo ya space sio kwa kizazi hiki kabisa.
 
Kama nini vile hebu nisaidie

vifanyie kazi hivyo anavyokulalamikia. Tena umepata mtu mzuri anayelalamika kwa hiyo ana communicate asichopenda na anachotaka afanyie. Sijui tatizo liko wapi Evelyn Salt kama mtu anaongea na wewe fanyia kazi anayoyalalamikia. Pia hizo kanuni zako ulizotoa za food, sex and space hebu achana nazo mapenzi hayana formula yoyote kwenye sehemu ya upendo onesha upendo kwenye sehemu ya kumliwaza mliwaze kwenye hitaji la ushauri mshauri, kwenye haja ya kumwombea mwombee akiwa na furaha furahi nae na akiwa na huzuni kuwa mfariji wake na akiwa na machozi kuwa mfutaji wa machozi yake na anaposhindwa kusimama mwenyewe simama nae

Ndoa ni kujitoa kila mmoja kwa mwenzake hamna kanuni
 
Last edited by a moderator:
ES,huwa nakusoma kwa tabasamu kila nionapo comment yako jukwaani,kwa hili uliloandika hapa nimeongeza tabasamu mara dufu,wewe ni mwanamke wa shoka,I've appreciated your efforts towards the strength of your marriage,unayoyapitia ni kawaida sana kwenye ndoa,hakuna mkamilifu 100%,kwa kuwa wewe ndiye mlalamikia jikague upya ujifanyie tathmini,yawezekana huduma unazotoa kama mke zimepungua ubora,au unazitoa kwa moyo uliokunjamana,kagua mawasiliano yako na mumeo,how do you use your words,facial&body while communicating to your hubby? ni kipi kipaumbele chako kati ya 'kidume cha mbegu' na 'dume la mbegu' katika huduma?,junior analala saa ngapi? isijekuwa badala ya kumuengaenga mume unamuenga enga 'kidume cha mbegu'? je unampokea anaporudi kazini? je unajipamba na kujitia manukato 'spesheli' kwa ajili ya mume wako? nina mengi ya kukuuliza ila jitathmini kama unaona uko sawa hebu create something different,nimeona ukiandaa maji bafuni tu sijawaona mkioga pamoja...
 
Hahahaha
My dear fanya kilicho bora kwako... kama shemeji anapenda mfanyie. Hapa jukwaani acha tu tupige blah blah ukifika ndani unakua mpole na kuboresha ndoa



 
Last edited by a moderator:
Kwakweli kwa maisha haya basi kuwa mwanaume ni raha, mie sijui haya maraha ntapewa na nani au tumeumbwa kutoa tu maraha?
Pole sana Kamanda kwakweli mwaka huu si mzuri kabisa...!
 
Kwakweli kwa maisha haya basi kuwa mwanaume ni raha, mie sijui haya maraha ntapewa na nani au tumeumbwa kutoa tu maraha?

Inatakiwa mpeana raha...sio kutoa wewe tu...

Ila kibongobongo mwanamke ndio wajitoooooaaa kwa hiyo usishangae
 
Ok jaribu kufanya apendavyo mkiwa wote jaribu kutokuwa busy na simu au uweke simu pembeni ...! Pengine ina furahisha sana ukiwa na mtu kama mnapiga story na yeye ana changia kidogo hata kwa kuuliza maswali! Pengine tatizo sio kuchat labda ni kuto kuonesha uko pamoja nae kwenye yale maongezi!
 
Nina washangaa hao wanao kushangaa wewe maana unatimiza wajibu wako vizuri.

Nikushukuru kwa hayo unayoyafanya na usikate tamaa. Naamin ipo siku atajifunza ku appreciate

Kuhusu kulalamika ni hali ya ubinadamu ivumilie tu. Maana na asiye lalamika pia ana mapungufu yake
 
Pia na yeye ana wajibu wa kukusaidia malezi.
Wanaume wakumbuke hata wao sio wakamilifu ila wake zao wanayakubali yake mapungufu. Na haswa kama una mtoto mdogo jamani shemeji aelewe na kuvumilia.

Hapo kwenye malezi mmh labda kucheza nae tu sio kind ya wababa waleaji kama ambao nshawaona na am okay with it ndivo alivo
Kuna baba nilikua naishi nae arusha jirani ana watoto 3 wamefatana kama ngazi basi yule baba kila siku asbh anawaweka kwenye pots, anawasafisha, anawapa uji, anafua nguo zao then anaenda kazini mke wake yupo ila naona hiyo ilikua ratiba ya baba kumsaidia mke nilimpenda bure
 

Vitu vidogo ndo vipi mfano? Hapo kwenye kufanya mapenzi tumebakiza tu kufanyia ndani ya friji.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…