Uchaguzi 2020 Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa 'fair play' ya leo kwenye mkutano wa Tundu Lissu mjini Morogoro

Uchaguzi 2020 Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa 'fair play' ya leo kwenye mkutano wa Tundu Lissu mjini Morogoro

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
284
Reaction score
912
Nimefurahishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kutimiza wajibu wake bila upendeleo.

Leo kwenye hadhara ya kutafuta wadhamini, mgombea urais kwa tiketi ya chadema, Bw. Tundu Antipas Lissu akiwa mkoani Morogoro, askari wa Jeshi la Polisi walionekana wakiimarisha ulinzi na kuhakikisha Bw. Tundu Antipas Lissu anakuwa salama muda wote.

Mpaka hadhara inaisha, amani ilikuwa imetamalaki na hakuna vurugu zozote zilizotokea.

To be honest; from the bottom of my heart nalipongeza jeshi la polisi kwa fairness ya leo. Natamani na maeneo mengine ambayo bado Bw. Tundu Antipas Lissu hajapita, polisi waonyeshe fairness kama walioonyesha polisi wa Morogoro.

Kama hali ikiendelea hivi; uchaguzi utakuwa huru na wa haki na amani itazidi kudumu katika taifa letu.

Mungu awabariki polisi wote
 
Mdaiwa-Sugu,

Lissu Kama Lissu! Huyo ndo shujaa wa Tanzania ndugu. Utampenda tu kwa kweli. Kwa madini aliyotema Leo ya kuwajali watu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Najua tu maneno yaliwaingia vizuri sana leo hawa jamaa hadi wakaamua kumlinda leo. Huyo ndo Lissu ndugu, Rais mtarajiwa wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
 
Hilo jeshi la polisi sijui limegawanyika nchi hii, wapo waelewa na wapo wale wenzangu na mimi, au labda leo ndio siku yao ya kupewa mishahara ndio maana wamekuwa na furaha, maana yake nikimkumbuka yule aliemkamata Sugu kule Mbeya juzi, hata siwaelewi hawa polisi wetu.
 
Hilo jeshi la polisi sijui limegawanyika nchi hii, wapo waelewa na wapo wale wenzangu na mimi, au labda leo ndio siku yao ya kupewa mishahara ndio maana wamekuwa na furaha, maana yake nikimkumbuka yule aliemkamata Sugu kule Mbeya juzi, hata siwaelewi hawa polisi wetu.
Kila fani haikosi majuha. Yule wa Mbeya ni kati ya majuha ndani ya Jeshi la Polisi.
 
17 Agosti 2020
Mikumi, Morogoro
Tanzania

MHE TUNDU LISSU AINGIA JIMBO LA MIKUMI NA KUPOKELEWA NA UMATI MKUBWA WA WANANCHI



Tundu Lissu akumbusha juu ya nasaha za kauli mbiu ya Mwalimu Nyerere iliyosisitiza utu ni UHURU katika kila kitu yaani Uhuru na Kazi pia Uhuru na Maendeleo na Uhuru na Umoja

Tundu Lissu anauliza kwanini Nyerere hakutanguliza Ma-barabara na Maendeleo au Miundo-mbinu na Maendeleo alijua kwanza utu wa mtu kupitia Uhuru kwanza ndiyo kitu muhimu ili kupata Maendeleo ya Kweli.

Tundu Lissu anasema binadamu siyo mifugo ukaamua kuondoa utu wao wa kuwa HURU kwa kisingizio kuwa kwa kuwanyima uhuru wa utu wao, kuwanyanyasa , kuwabeza ndiyo unataka kuwaletea Maendeleo.
source: CHADEMA MEDIA TV
 
Back
Top Bottom