Zanzibar 2020 Namba 5: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar

Zanzibar 2020 Namba 5: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar

Maamuzi ya mgombea Zanzibar hufanyika kisiwandui na jina kupelekwa Dodoma sio kinyume chake ndio maana fomu zinachukuliwa na kurudishwa kisiwandui sio Dodoma
Ni kweli fimu fomu zinachukuliwa Kisiwandui jirani kabisa na Michenzani na Mkunazini lakini wanaochagua nani awe mgombea kupitia CCM hukaa Dodoma, CCM Zanzibar haichagui mgombea badala yake inachuja tu wagombea wa kuwapeleka Dodoma. Hofu kubwa ya CCM ni kutopata mgombea mwenye msimamo mkali dhidi ya Muungano.

Sijui umeanza lini kufuatilia siasa za Visiwani, labda nikukumbushe tu.

Mwaka 2000 wakati Dr. Salmon Amour anamaliza miaka yake kumi. Waziri kiongozi 1995 - 2000 Dr. Gharib Bilal aliongoza huko Zanzibar dhidi ya wagombea wenzake akiwemo Aman Karume. Majina matatu yakapelekwa Dodoma- wakati huo Chimwaga. Watu wakafanya yao nafasi ikamwendea Aman Abeid Karume ambaye hakuwa mwanasiasa mkongwe zaidi ya kubebwa na jina la baba yake.
Mzee Bilal akapoozwa kwa umakamu wa rais miaka kumi baadaye mwaka 2010-2015 Serikali ya Jamhuri.

Mwaka 2010 - Wakati Aman Abeid Karume anamaliza muda wake. Waziri wake kiongozi akiwa na umri mdogo kabisa ndugu Shamsi Vuai Nahodha akiwa na miaka 47 aliongoza kwenye mchakato kwa upande wa CCM Zanzibar. Majina matatu yalipopelekwa Dodoma, nafasi ikamwendea Dr. Shein aliyekuwa Makamu wa Rais kutokea 2001- 2010 chini ya mzee wa Msoga. Dr Ali Mohamed Shein alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais chini ya Rais Mkapa mwaka 2001 mara baada ya kifo cha Dr Omar Ali Juma.

Kamwe chama cha kijani hakitakaa kiruhusu mgombea kupitia chama hicho achaguliwe Kisiwandui. Hawataki yarudie yale ya Bwana Jumbe.
 
Choice yangu mimi ni Prof Mbarawa.
Huyu baba ni jembe jmani. Wazanzibar wamshawishi huyu baba achukue form. Anaju kazi na pia hajikwezi.. Yuko simple and humble... Ataipeleka Zanzibar mbali..
Kumbe ni choice yako...
Huyo kasomeshwa na serikali ya mapinduzi lakini hajawahi kuitumikia serikali yake... ili tumpe kwanza atulipe hela zetu....
 
Hussein Mwinyi hawezi kuwa Rais wa Zanzibar kwa muhula huu. Ni wakati mgumu kuliko vipindi vyote kugombania Urais wa Zanzibar. He is too soft and diplomatic. Tume ikilazimisha kumtangaza wanaetaka basi itakuwa ni Zimbabwe kwa Tanganyika. Tukumbuke wakati ule tulikuwa na Kikwete aliyekuwa akicheza ngoma za mabeberu. Sasa hivi wanatafuta sababu tu watumwagie manyanga!
 
Prof. Mbarawa nendaaa kachukue fomu, mm naona Hussein Mwinyi sio mtendaji mzuri, kakaa ki VIP tu, ila utendaji sioni hapo.
 
Shiiiii ongea taratibu ? unamwongelea Mbowe na Joyce mukya mbunge viti maalumu kimafumbo? ASIKUSIKIE MBOWE shauri yako
Meko kawapa watoto wa dada zake vyeo,vipi dada hidaya unachukua fomu ya ubunge viti maalumu
 
Kama Mwinyi Angekua amewekwa wizara ngumu zinazohitaji mtu afanye kazi haswa akazimudu ningeamini anaweza Sana.
Wizara ya Mambo ya ndani
Wizara ya ujenzi
Wizara ya ardhi
Sasa Ukiwa waziri Wa wizara ya ulinzi na JKT haiwagusi wananchi moja kwa moja kwenye Maisha yao ya kila Siku.
Hata ukimuuliza mwananchi kule chini anaweza asimjue hata Huyo waziri na asijue hata anafanya kazi gani.
Ni nani alipewa Hiyo wizara ikamshinda?
Nafikiri aliwekwa makusudi kwenye wizara ambayo haiwezi kumletea madhara na wananchi haiwasumbui Sana.
Umesahau alikuwa waziri wa afya tena kwa wakati mgumu sana katika sekta hiyo.

Yeye ndio aliyeenda kutuliza joto la migomo na misuso ya madaktari pale wizadani enzi za Jk.

Baada ya maji kukorogeka pale wizarani na migomo mingi ya madaktari akatafutwa wa kwenda kumaliza migomo ile ikabidi atolewe ulinzi aende kusawazisha mambo pale wizarani.
 
Natumaini atashinda
Lakini shemeji yetu kwa ukimya wako utaweza kweli?!
WaZenji wapole utakuwa sawa
Go for it!
support you mingi mingi!
Hivi we mama si ulikuwaga chadema vile? au nakufananisha?
 
Hussein Mwinyi hawezi kuwa Rais wa Zanzibar kwa muhula huu. Ni wakati mgumu kuliko vipindi vyote kugombania Urais wa Zanzibar. He is too soft and diplomatic. Tume ikilazimisha kumtangaza wanaetaka basi itakuwa ni Zimbabwe kwa Tanganyika. Tukumbuke wakati ule tulikuwa na Kikwete aliyekuwa akicheza ngoma za mabeberu. Sasa hivi wanatafuta sababu tu watumwagie manyanga!
Hizi hadithi tumeanza kuzisikia toka mwaka 1995 na hakuna chochote kimetokea.

Kuna wakati upinzani zanzibar umekuwa na nguvu kuliko mwaka 1995 na 2015??
Sasa hivi umejionea kujifia kwa upinzani kumbuka Cuf imegawanyika,kuna Cuf na Act.
Upinzani umekwisha na upo ICU.
Na umeuliwa kwa makusudi na hila za CCM.
Kama upinzani ulishindwa kushika dola la zanzibar 2015 licha ya kushinda unadhani wataweza sasa hivi??

Kama Dr. Shein mpole, muungwana na mkimya ameweza kutawala kwa miaka 10,basi hata Dr. Mwinyi ataweza kabisa bila shida.
 
Back
Top Bottom