Namna ambavyo bila kujua unatumia kipato chako kuwalipa wengine bila ya kujilipa wewe kwanza

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Unapata kipato chako mfano laki tano kwa mwezi, mtu anakuambia pesa yako hii bila kujua unawalipa watu wengine wewe hujilipi, swali la kujiuliza kwani hii laki tano si ya kwangu najilipaje sasa wakati laki tano hii ni yangu?

Ni kweli yako lakini sasa katika laki tano mfano utagawa mahesabu kama ifuatavyo:

150000 chakula = hapo umemlipa muuza chakula ili akulishe wewe,hivyo katika 500K 150000 sio yako.

50000 nauli = hapa umemlipa mwenye usafiri nauli hivyo katika laki tano 200000 sio zako.

50000 kodi = hapo umeshamlipa mwenye nyumba hivyo katika 500K basi jua 250000 sio zako.

Let say 50000 mavazi = manake 50K umemlipa muuza nguo manake kwenye laki tano 300000 sio yako.

50000 bata bar = hapo ushamlipa muuza bar 50000 hivyo kwenye 500K jua 350000 sio zako.

Let say umetuma 50000 home= hapo jua 50K umewalipa au umewapa wazazi hivyo kwenye 500K basi 400k sio zako.

Let say 50000 umehonga,manake hapo umemlipa demu 50k means kwenye 500k basi 450k sio yako.

Let say 20000 umetumia vocha,means hyo 20K umemlipa muuza vocha tayari,hivyo katika 500k basi 470k sio zako.

Basi na hizi 30k ukatumia katika kununua vitu vya hamu kwa mwezi means laki tano yote umetuma.

Swali ; je wewe umebakiwa na nini ?

Jawabu umebaki na korodani tu.

Je ni kweli ile laki tano iyopokea kwa mwezi ni yako au ya watu hao hapo ?
Jawabu sio yako kwa sababu ingekuwa yako ungelikuwa mpaka sasa lakini umetumia kwa sababu ya huduma ambazo ni lazima kila mtu azipate.

Je wewe ni mtu wa kuishi ukitafuta kula,kulipa kodi,kunya na kuvaa tu ?
Una tofauti gani na mfanya ama mtumwa ambaye anafanya kazi na kupewa huduma muhimu tu kama wewe ?

Hakuna kingine unachohitaji katika maisha yako ?

Kama jibu ni ndio hapo ndio inakuja dhana ya kujilipa mwenyewe kwanza.

KUJILIPA MWENYEWE ni kitendo cha wewe kutenga kiasi kadhaa katika kila pesa unayoipata na kuweka kiasi kadhaa hiko akiba yaani huigusi kabisa kwa matumizi ya pale juu tuliyoyaona

Kiasi kadhaa hiki wengi wanapendekeza kwa kuanza uweke 10% ya kila kipato unachopata.

Kiasi hiki hautakiwi kukigusa kwa lolote litakalotokea,badala yake zile 90% zilizobaki ndio utumie kwa mambo unayoyaona hayaepukiki.

Hii 10% unayosave ndio yako kwa sababu haiendi kwa mtu mwingine hivyo ni pesa ambayo jnatakiwa kuithamini kuliko hizo 90% zilizobaki kwa sababu hizo 90% unaenda kuwapa watu wengine kwa kununua huduma zao.

Hakikisha hii 10% yako unaiweka na kujiwekea malengo kwamba uiwache mfano ukisema uiwache hii 10% ya laki tano (50000) kwa mwaka mmoja itakuwa ni laki sita.

Hii laki sita ukishafanikiwa kuipata sasa unaanza kuwekeza katika jambo ambalo litaingiza faida na kuzalisha pesa zaidi.

Lakini zingatia yafuatayo unapowekeza..

1.hakikisha hauna pupa ya faida ya haraka.

2.wekeza katika jambo ambalo una ujuzi nalo,au hakikisha umeomba ushaurina umehakikishiwa usalama wa pesa zako na WATAALAMU HASWA wa biashara hiyo.

Kama huna mtaalamu yeyote wa biashara unayotaka kufanya usiifanye biashara hiyo vuta subira utakuja kulia.

Usishawishike na mtu akisema kitu fulani ni rahisi na kina faida kweeli,weeeee
Weeeeeeeee
Weeeeew

Denzel washington iwahi kusema kwamba "ease is the great threat to progress than a hardship".

Naomba kuwasilisha.
 
Uzi wako una hoja ya msingi lakini uneshindwa kucapture maisha ya wenye kipato cha chini ambacho kinachapatikana hakitoshi hata mahitaji ya msingi, yani inabidi wacompromise hata mahitaji muhimu kabisa Ila waweze kuishi. Mtu Kama uyo unamwambiaje awake 10% za kujilipa?
 
Kwa iyo uzi huu umeandikia wanaume tuu. Mbona ume wa exclude wanawake kwenye uwasilishaji wako wa taarifa
 
Hii ndo Bablylonian principle of financial success na ipo applicable.

Kwa kuongezea tu, kama mtu unataka financial freedom na upo na madeni ukishatenga hizo asilimia zako kumi za kujilipa, asilimia ishirini zingine zigawanye kwa wadeni wako wote, ikiwezekana waandikie barua kwamba umekaa chini ukaona unataka kuwa na financial freedom na umeamua kuanza kuwalipa asilimia ishirini ya mapato yako hadi utakapomaliza deni lao hivyo kuwaahidi kila baada ya mda flani utawalipa kiasi kadhaa, hapa utabakiwa na asilimia sabini.

Wapo wadeni wako watakupongeza kwa namna ulivyoamua kuwalipa, ila wapo wengine ambao wanataka uwalipe kila unachopata ili uje ukope tena waendelee kukutawala kifikra. Hawa usiwaogope hata kama watakupeleka mahakamani, hakuna mahakama duniani ambayo itapingana na maamuzi mazuri uliyoyachukua.

Mfano pato lako ni laki mbili kwa mwezi, wanaokudai ni watano kila mmoja laki mbili, jumla ya deni ni milioni moja, hapa ukisema utamlipa kila mmoja kila unachopata utakopa tena na tena mpaka ushangae. Kwahiyo asilimia ishirini hapo ni elfu arobaini, ukigawa kwa tano elfu nane, kwahiyo kila mwezi utawalipa elfu nane hadi deni lao litakapoisha ndipo uanze kutumia asilimia tisini.

It sound "kimotiveshono spika" ila hakuna namna.
 
Unapata kipato chako mfano laki tano kwa mwezi, mtu anakuambia pesa yako hii bila kujua unawalipa watu wengine wewe hujilipi, swali la kujiuliza kwani hii laki tano si ya kwangu najilipaje sasa wakati laki tano hii ni yangu?

Ni kweli yako lakini sasa katika laki tano mfano utagawa mahesabu kama ifuatavyo:

150000 chakula = hapo umemlipa muuza chakula ili akulishe wewe,hivyo katika 500K 150000 sio yako.

50000 nauli = hapa umemlipa mwenye usafiri nauli hivyo katika laki tano 200000 sio zako.

50000 kodi = hapo umeshamlipa mwenye nyumba hivyo katika 500K basi jua 250000 sio zako.

Let say 50000 mavazi = manake 50K umemlipa muuza nguo manake kwenye laki tano 300000 sio yako.

50000 bata bar = hapo ushamlipa muuza bar 50000 hivyo kwenye 500K jua 350000 sio zako.

Let say umetuma 50000 home= hapo jua 50K umewalipa au umewapa wazazi hivyo kwenye 500K basi 400k sio zako.

Let say 50000 umehonga,manake hapo umemlipa demu 50k means kwenye 500k basi 450k sio yako.

Let say 20000 umetumia vocha,means hyo 20K umemlipa muuza vocha tayari,hivyo katika 500k basi 470k sio zako.

Basi na hizi 30k ukatumia katika kununua vitu vya hamu kwa mwezi means laki tano yote umetuma.

Swali ; je wewe umebakiwa na nini ?

Jawabu umebaki na korodani tu.

Je ni kweli ile laki tano iyopokea kwa mwezi ni yako au ya watu hao hapo ?
Jawabu sio yako kwa sababu ingekuwa yako ungelikuwa mpaka sasa lakini umetumia kwa sababu ya huduma ambazo ni lazima kila mtu azipate.

Je wewe ni mtu wa kuishi ukitafuta kula,kulipa kodi,kunya na kuvaa tu ?
Una tofauti gani na mfanya ama mtumwa ambaye anafanya kazi na kupewa huduma muhimu tu kama wewe ?

hakuna kingine unachohitaji katika maisha yako ?

Kama jibu ni ndio hapo ndio inakuja dhana ya kujilipa mwenyewe kwanza.

KUJILIPA MWENYEWE ni kitendo cha wewe kutenga kiasi kadhaa katika kila pesa unayoipata na kuweka kiasi kadhaa hiko akiba yaani huigusi kabisa kwa matumizi ya pale juu tuliyoyaona

Kiasi kadhaa hiki wengi wanapendekeza kwa kuanza uweke 10% ya kila kipato unachopata.

Kiasi hiki hautakiwi kukigusa kwa lolote litakalotokea,badala yake zile 90% zilizobaki ndio utumie kwa mambo unayoyaona hayaepukiki.

Hii 10% unayosave ndio yako kwa sababu haiendi kwa mtu mwingine hivyo ni pesa ambayo jnatakiwa kuithamini kuliko hizo 90% zilizobaki kwa sababu hizo 90% unaenda kuwapa watu wengine kwa kununua huduma zao.

Hakikisha hii 10% yako unaiweka na kujiwekea malengo kwamba uiwache mfano ukisema uiwache hii 10% ya laki tano (50000) kwa mwaka mmoja itakuwa ni laki sita.

Hii laki sita ukishafanikiwa kuipata sasa unaanza kuwekeza katika jambo ambalo litaingiza faida na kuzalisha pesa zaidi.

Lakini zingatia yafuatayo unapowekeza..

1.hakikisha hauna pupa ya faida ya haraka.

2.wekeza katika jambo ambalo una ujuzi nalo,au hakikisha umeomba ushaurina umehakikishiwa usalama wa pesa zako na WATAALAMU HASWA wa biashara hiyo.

Kama huna mtaalamu yeyote wa biashara unayotaka kufanya usiifanye biashara hiyo vuta subira utakuja kulia.

Usishawishike na mtu akisema kitu fulani ni rahisi na kina faida kweeli,weeeee
Weeeeeeeee
Weeeeew

Denzel washington iwahi kusema kwamba "ease is the great threat to progress than a hardship".

Naomba kuwasilisha.
Naomba uwe rafiki yangu mkuu,watu kama wewe tupo wachache....wengi hawatakuelewa.
 
Uzi wako una hoja ya msingi lakini uneshindwa kucapture maisha ya wenye kipato cha chini ambacho kinachapatikana hakitoshi hata mahitaji ya msingi, yani inabidi wacompromise hata mahitaji muhimu kabisa Ila waweze kuishi. Mtu Kama uyo unamwambiaje awake 10% za kujilipa?
Aaaagh mchumi mashuhuri Duniani John Maynard Keynes keynessian umeuliza swali muhimu Sana. Lakini ukitafakari, hakuna namna, haijalishi unalala njaa, unalala stand ya basi, una kipato Cha 50,000 kwa mwezi BILA KUFANYA UWEKEZAJI HUFIKI POPOTE.

Namaanisha hivi, kila mtu Lazima afanye investment, iwe ni kwenye biashara au elimu (hasa kwa waliopo kazini wakitegemea kupandishwa cheo na mshahara). Ni lazima uwekeze, no way out no alternative, Lazima uongeze kipato. Hakuna mzungu au ndugu yako atakuja kuwekeza kwa niaba yako na kukupa maisha Bora, kiufupi wewe ndiye pilot wa maisha yako.

Ngoja nikupe mfano halisi. Mimi kipindi nipo form two, Mama alinipa kuku nikaenda 1 katetea. Kale kakuku nilikalea kakaja kutaga, kakaatamia na kutotoa vifaranga 12. Kama unavyojua maisha ya vijijini, sikuwahi kumpa chakula labda mabaki tu, Wala dawa sijawahi kumpa. Baada ya miezi kadhaa nikahama mpaka mkoa mwingine. Yule kuku na watoto wake walimla. Mpaka Sasa kwa kweli huwa namkumbuka Sana yule kuku, laiti kama ningejuwa angekuja kunipa mtaji.

Kwa hivyo hata kama unaanza na kuku 1, unaweza kushangaa anakupa kuku 100 hata 500.
Yaani bila kupepesa macho, maisha yako yapo mikononi mwako. Nafanya kazi na miradi hii donor funded projects naweza kukwambia tu kuwa hii miradi inalembwa lembwa tu kuwa inasaidia watu wa Hali ya chini, but deeply ni miradi ya upigaji wa wachache wanaojilipa millions wakipeleka maneno matupu kwa wakulima.

Ni lazima mtu awe na malengo hata ya miaka 5, hata kujiwekea vikuku 10 au mbuzi 2 kila mwaka. Hali ngumu.
 
Mkuu upo sawa kabisa. Nafurahi kwa kuwa umesema umeishi kijijini so unafaham maisha halisi ya mtanzania.

Kwa kuwa una uzoefu na maisha nionyeshe mtu mwenye familia ya watu watatu anavyoweza kuishi, kusave na kuinvest kwa kipato cha 200,000(sina uhakika sana lakini naamini kuna wengine hawafikishi hiko pia) jijini dar es salaam.

Kwa haraka haraka assume
1.Kodi ya nyumba 50,000(hapa lazima uwe nje ya mji kidogo which means kuna element ya nauli)
2.Chakula 3000@30 =90,000(hii ni very basic na ina maana hata nyama hawezi kula)
3.Nauli 1000 @30 =30,000
4.Maji na Umeme 30,000

Mpaka hapo 200k imeisha
kuna vitu basic bado sijaviweka kama nishati ya kupikia, mawasiliano n dharura.
Kumbuka huyu hata bima ya afya hana na bado ana mke na mtoto mmoja mdogo.

Ndo mana nimemwambia mleta mada, andiko lake ni zuri mno nawewe pia umeongeza vizuri lakini kiukweli hizo mbinu haziwezi kumkwamua mtu anayeishi aina ya maisha kama uo mfano hapo juu.
 
Uzi wako una hoja ya msingi lakini uneshindwa kucapture maisha ya wenye kipato cha chini ambacho kinachapatikana hakitoshi hata mahitaji ya msingi, yani inabidi wacompromise hata mahitaji muhimu kabisa Ila waweze kuishi. Mtu Kama uyo unamwambiaje awake 10% za kujilipa?
Linapokuja suala la akiba hakuna udhuru.

Kama mtu anapata alfu 2 kwa siku aweke 200 tu akiba kwa siku.

Ni jambo linawezekana kwa mwenye nia
 
Mkuu upo sawa kabisa. Nafurahi kwa kuwa umesema umeishi kijijini so unafaham maisha halisi ya mtanzania.
Kwa kuwa una uzoefu na maisha nionyeshe mtu mwenye familia ya watu watatu anavyoweza kuishi, kusave na kuinvest kwa kipato cha 200,000(sina uhakika sana lakini naamini kuna wengine hawafikishi hiko pia) jijini dar es salaam.

Kwa haraka haraka assume
1.Kodi ya nyumba 50,000(hapa lazima uwe nje ya mji kidogo which means kuna element ya nauli)
2.Chakula 3000@30 =90,000(hii ni very basic na ina maana hata nyama hawezi kula)
3.Nauli 1000 @30 =30,000
4.Maji na Umeme 30,000

Mpaka hapo 200k imeisha
kuna vitu basic bado sijaviweka kama nishati ya kupikia, mawasiliano n dharura.
Kumbuka huyu hata bima ya afya hana na bado ana mke na mtoto mmoja mdogo.

Ndo mana nimemwambia mleta mada, andiko lake ni zuri mno nawewe pia umeongeza vizuri lakini kiukweli hizo mbinu haziwezi kumkwamua mtu anayeishi aina ya maisha kama uo mfano hapo juu.
Kama mindset zenyewe ndio hizi sitegemei kama mtu kama wewe utakwamuka na kuweka akiba mkuu.

Mtu anayepata laki mbili kwa mwezi akiba ya 10% ni 20000 tu,inatakiwa kuna matumizi apunguze afanye yale ya muhimu tu.

Kama hujawa tayari haiwezekani,ukiwa tayari inawezekana.

Ukiweka akilini kwamba matumizi yote unayofanya unawalipa watu basi kuna uchungu utakuja wa kujilipa wewe kwanza.
 
Back
Top Bottom