Namna ambavyo bila kujua unatumia kipato chako kuwalipa wengine bila ya kujilipa wewe kwanza

Namna ambavyo bila kujua unatumia kipato chako kuwalipa wengine bila ya kujilipa wewe kwanza

Uzi wako una hoja ya msingi lakini uneshindwa kucapture maisha ya wenye kipato cha chini ambacho kinachapatikana hakitoshi hata mahitaji ya msingi, yani inabidi wacompromise hata mahitaji muhimu kabisa Ila waweze kuishi. Mtu Kama uyo unamwambiaje awake 10% za kujilipa?
Kwa fikra inaonekana ni rahisi lakini uhalisia ni tofauti mshahara unaisha kabla ya kuupokea.
 
Kwa fikra inaonekana ni rahisi lakini uhalisia ni tofauti mshahara unaisha kabla ya kuupokea.
Hakuna mafanikio rahisi mkuu.

Ukisema ni ngumu,ni ngumu,ni ngumu na siku zinaenda pia
 
Ndo matatizo ya kusoma Sana Ayo mavitabu yenu.

Matuletea vitu tofauti na uhalisia wa maisha yetu mtaani.
 
alafu ukimpa scenario kama iyo ya laki mbili ambao ni uhalisia bado anangangania theories zake
Kama unashindwa kusave hata 2000 tsh kwenye laki mbili basi unahitaji maombi.

Akiba ni chochote unachosave sio lazima iwe 10%.

Unaweza kuamua kusave hata 2.5% ya laki mbili na bado hyo inakuwa yako.
 
"Kiasi hiki hautakiwi kukigusa kwa lolote litakalotokea,badala yake zile 90% zilizobaki ndio utumie kwa mambo unayoyaona hayaepukiki".

Kwa hiyo kumlipa Landlord, mangi dukani na konda wa daladala ni mambo yanayoepukika? Watu wasevu hela bila kujiumiza.
 
Hii ndo Bablylonian principle of financial success na ipo applicable.

Kwa kuongezea tu, kama mtu unataka financial freedom na upo na madeni ukishatenga hizo asilimia zako kumi za kujilipa, asilimia ishirini zingine zigawanye kwa wadeni wako wote, ikiwezekana waandikie barua kwamba umekaa chini ukaona unataka kuwa na financial freedom na umeamua kuanza kuwalipa asilimia ishirini ya mapato yako hadi utakapomaliza deni lao hivyo kuwaahidi kila baada ya mda flani utawalipa kiasi kadhaa, hapa utabakiwa na asilimia sabini.

Wapo wadeni wako watakupongeza kwa namna ulivyoamua kuwalipa, ila wapo wengine ambao wanataka uwalipe kila unachopata ili uje ukope tena waendelee kukutawala kifikra. Hawa usiwaogope hata kama watakupeleka mahakamani, hakuna mahakama duniani ambayo itapingana na maamuzi mazuri uliyoyachukua.

Mfano pato lako ni laki mbili kwa mwezi, wanaokudai ni watano kila mmoja laki mbili, jumla ya deni ni milioni moja, hapa ukisema utamlipa kila mmoja kila unachopata utakopa tena na tena mpaka ushangae. Kwahiyo asilimia ishirini hapo ni elfu arobaini, ukigawa kwa tano elfu nane, kwahiyo kila mwezi utawalipa elfu nane hadi deni lao litakapoisha ndipo uanze kutumia asilimia tisini.

It sound "kimotiveshono spika" ila hakuna namna.
Mkuu hapo kwenye madeni umeeleza vyema sana. Hii comment yako iwekwe kwenye rasimu ya Warioba.
 
Back
Top Bottom