Hii ndo Bablylonian principle of financial success na ipo applicable.
Kwa kuongezea tu, kama mtu unataka financial freedom na upo na madeni ukishatenga hizo asilimia zako kumi za kujilipa, asilimia ishirini zingine zigawanye kwa wadeni wako wote, ikiwezekana waandikie barua kwamba umekaa chini ukaona unataka kuwa na financial freedom na umeamua kuanza kuwalipa asilimia ishirini ya mapato yako hadi utakapomaliza deni lao hivyo kuwaahidi kila baada ya mda flani utawalipa kiasi kadhaa, hapa utabakiwa na asilimia sabini.
Wapo wadeni wako watakupongeza kwa namna ulivyoamua kuwalipa, ila wapo wengine ambao wanataka uwalipe kila unachopata ili uje ukope tena waendelee kukutawala kifikra. Hawa usiwaogope hata kama watakupeleka mahakamani, hakuna mahakama duniani ambayo itapingana na maamuzi mazuri uliyoyachukua.
Mfano pato lako ni laki mbili kwa mwezi, wanaokudai ni watano kila mmoja laki mbili, jumla ya deni ni milioni moja, hapa ukisema utamlipa kila mmoja kila unachopata utakopa tena na tena mpaka ushangae. Kwahiyo asilimia ishirini hapo ni elfu arobaini, ukigawa kwa tano elfu nane, kwahiyo kila mwezi utawalipa elfu nane hadi deni lao litakapoisha ndipo uanze kutumia asilimia tisini.
It sound "kimotiveshono spika" ila hakuna namna.