Namna ambavyo bila kujua unatumia kipato chako kuwalipa wengine bila ya kujilipa wewe kwanza

Mkuu naona umesoma na kuelewa vyema falsafa ya mwandishi George Samuel Clason kwenye kitabu chake cha The Richest Man in Babylon
Kile kitabu nilikisoma muuda kidg ila kizuri kishenzi
 
Umeandika uzi mzuri sana ambao wengi wataupuuza. Washaaza hapo juu kusema ni motivation speaker, ungesema Yanga/Simba wangekuja mbio
Msimtie moyo kaandika utopolo, yaani hata ameshindwa kuwaza kuwa analipa pesa na anapata huduma ambayo mnasaidia yeye mwenyewe..
 
Vizuri mkuu na inawezekana ila kwa mfano wako apo juu it means huyo jamaa atasave laki sita kwa mwaka. Mh baada ya hapo
 
Msimtie moyo kaandika utopolo, yaani hata ameshindwa kuwaza kuwa analipa pesa na anapata huduma ambayo mnasaidia yeye mwenyewe..
Mkuu lazima tuangalie kusudi la mleta mada,amejaribu kutuonyesha namna gani kila mmoja anatakiwa kujilipa kwanza kabla ya kufanya jambo laolote ili uwe na financial freedom.Hilo peke yake tumpongeze kwa kutufunza kwani watu wengi tumeajiriwa but mpaka sasa tunaendelea kuteseka na umaskini.
 
Vizuri mkuu na inawezekana ila kwa mfano wako apo juu it means huyo jamaa atasave laki sita kwa mwaka. Mh baada ya hapo
Tatizo hamsomi ili muelewe mnasoma ili mujibu.

Mbona niliandika mkuu kwamba ukishasave kiasi fulani sasa unawekeza ambako pesa itazaa na huko kwenye kuwekeza kuna masharti nimeyaweka,ila hukusoma kuelewa ulisoma kujibu...
 
Nimesoma pote uwekezaji upi sasa wa laki sita ambao hauta athiri hiyo shughuli yangu inayonipa 500k per month? Twende taratibu tu acha jazba mimi sikukejeri bali nasaka maarifa kwako.

Amani iwe nawe.
 
Mkuu nimekupm
 
Mbona simple tu, mchanganuo umewekwa hapo, onyesha namna uyo mtu atakavyosave.

Kila aina ya matatizo yana suluhu zake, ila nasisitiza ulichoandika hakifanyi kazi kwa makundi yote.
 
Aweke hata mia mbili kwa siku Kuna siku atapata shida kubwa akiwa amefanikiwa kujiwekea hata 20 elfu atajikopesha, wengine mambo magumu kwa kushindwa kufanya displine ya maisha yake anataka akipata hata shida ndogo wengine ndo wahusike na shida zake ndogo ndogo.
 
Summation of this is stupidity! Hata ukiweka akiba hizi hela huenda Kwa watu vile vile
 
Na siyo kuteseka kwa umasikini tu bali hata kwa kukosa pa kujikopesha kwenye shida ndogo ndogo kama shida za ghafla za 5000 au 10, 000 kwa kukosa nidhamu ya kujilipa Kwanza.
 
Nimesoma pote uwekezaji upi sasa wa laki sita ambao hauta athiri hiyo shughuli yangu inayonipa 500k per month? Twende taratibu tu acha jazba mimi sikukejeri bali nasaka maarifa kwako.

Amani iwe nawe.
Mkuu angalia na sehemu uliyokuepo
Summation of this is stupidity! Hata ukiweka akiba hizi hela huenda Kwa watu vile vile
Sawa mkuu tunatakiwa tuyapokee na maoni kama haya yenu pia.
 
onyesha namna uyo mtu atakavyosave
Mkuu mimi nimesema kwenye laki mbili asave 20000 kwa mwezi kuna matumizi ayapunguze ili asave hiyo 20000.

Unataka mchanganuo gani tena ?
 
Nimesoma pote uwekezaji upi sasa wa laki sita ambao hauta athiri hiyo shughuli yangu inayonipa 500k per month?
Mkuu kuna mambo mengi ya kufanya kwa mujibu wa sehemu uliyokuwepo wewe ndio utumie akili ya kujua nimfuate nani mzoefu anielekeze juu ya biashara ambayo ninataka kuifanya.

Mimi sipo kukuambia ufanye mradi upi,naweza kukuambia uza nguruwe kumbe kwa mazingira yako ukiwafata wataalamu watakuambia hapa nguruwe hatoki kwa sababu kadha wa kadha.

Naweza kukuambia uza mabaibui kumbe ukiwafata wataalamu kwa maeneo yako watakuambia utafeli.

So kimsingi siwezi kukuambia uwekeze wapi,wewe akili yako na maeneo uliyokuepo ndiyo mtaamua mfanye kitu gani.

Kumbuka kwamba mimi nimetoa muongozo wa vipi ufanye na sijatuo muongozo wa nini ufanye,kuhusu nini ufanye wewe ndio utaangalia na mazingira yako.

Ila kama utaona hii mada ni nonsense kwako sio ishu mkuu.
ambao hauta athiri hiyo shughuli yangu inayonipa 500k per month?
Wewe ndio unajua shughuli unayofanya hivyo mimi siwezi jua biashara ipi ambayo haitokuathiri kwa sababu hiyo shughuli mimi siijui,ni wewe sasa ukae chini uamue utumie akili kipi ufanye ili usiathiriwe na biashara yako.
Twende taratibu tu acha jazba mimi sikukejeri bali nasaka maarifa kwako.
Nimeshatoa maelezo yangu hapo juu mzee
 
Ni kweli ndio maana mwajiriwa hapaswi kutegemea mshahara tu
Naam sasa tuko pamoja japokuwa sio lazima mtu kusave kwa sababu mtu anasave kwa faida yake,so akiona sio lazima anaweza kuacha kusave na maishs yakaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…