Namna wachezaji mpira wa nje wanavyomiliki Ardhi Tanzania

Namna wachezaji mpira wa nje wanavyomiliki Ardhi Tanzania

Sehemu kubwa ya Dunia,inawezekana kasoro tu.Ardhi ya za Zanzibar & Rwanda.


Ubaguzi na chuki kwa wenzio sio nzuri.
Hata mda huu nenda Congo utapata ardhi TU mbona.
 
Mimi sina wivu na wageni hata Dola ilipoamua kwamba utajiri wa nchi hii uruhusiwe Kwa watz wenye asili ya asia naona poa tu!

Ninachataka katiba na Sheria zibadilishwe ili Kila MTU awe na haki na hata akishika asiharibu kabisa!!

RIP Reginald Mengi, RIP rama wa kariakoo aliejipiga risasi mwenyewe kwa kuhisi kunyanyasika kibiashara na hujuma alizopitia!!

Sheria zinadilishwe utajiri hapa bongo uwe fair kwa wote na sio TU Raia wenye asili fulani pekee!!

Haiwezekani top 10 ya matajiri bongo karibu wote eti ni raia wenye asili ya asia kana kwamba wazawa wote ni wavivu!!

RIP Ali Mufruki mpiganaji na wazawa matajiri waliopoteza maisha yao (MIMI SIKURIDHIKA NA VIFO VYAO) Ni kama kule kenya wasomali ndio ma don.wazawa wanaandamana kana kwamba wao hawana akilia ya utafutaji!!


Naishia hapa!

Mawazo huru na nadharia zinazokuja kichwani na kuondoka!!
Wewe si unaogopa kuuwa tembo kuchukuwa meno ukauze, waache matajili waendelee kuwa matajili.

Hakuna utajili wa halali labda waliorithi kama kina Manji na Mo Dewji na bado lazima umanipulate mfumo ili kuutunza utajiri na kuupanuwa utajili.
 
Mashamba yanaunzwa bei ya kutupa lakini vijana wengi hawana plan za kuyanunua.

Mnachoweza ni kujadili plan za Simba na Yanga.

Ila wageni wakinunua ardhi mnaanza kuhoji!
 
Tanzania ni nchi ya amani na kila mtu anaitamani.

Sasa hawa jamaa wanapokuja kucheza mpira hapa,

Maisha ya hapa yanawavutia mno.

Wamebuni mbinu ya kuzaa hapa.

Mali zao wanasajili kwa majina ya watoto wao.

Mfano mzuri yule jamaa aliyekuwepo kwa vyura na sasa yupo kwa waarabu.
Nenda Arusha uone, ndio maana Botswana walishituka hii mambo
 
Kama umiliki ni wa mtoto unamuonea wivu au ni nini? Yani hamtaki hata uwekezaji kidogo? Ardhi ni nini? Unataka huyo mtoto aende wapi kama kazaliwa hapa?
Wanataka wapigwe mkuyenge kama aliopigwa Mirembe na RC mtuhumiwa.Wazee wa Sanda banahhh
 
Wanataka wapigwe mkuyenge kama aliopigwa Mirembe na RC mtuhumiwa.Wazee wa Sanda banahhh
Ukute hata kula mchana hujala na bado unashabikia ujinga.

Taifa lililojaa wanjinga. Hii mali haina mwenyewe hii.

Wacha muibiwe.
 
Tanzania ni nchi ya amani na kila mtu anaitamani.

Sasa hawa jamaa wanapokuja kucheza mpira hapa,

Maisha ya hapa yanawavutia mno.

Wamebuni mbinu ya kuzaa hapa.

Mali zao wanasajili kwa majina ya watoto wao.

Mfano mzuri yule jamaa aliyekuwepo kwa vyura na sasa yupo kwa waarabu.
Bora hao wachezaji kuliko wachina na waturuki wanaozaa na kuwatelekeza watoto wao bila kitu.
 
Ukishakuwa ccm huna tofauti na mchawi.

Yani roho haikuumi bandari kupewa Waarabu ila unateseka Mtanzania akimuuzia mgeni ardhi yake anayoimiliki kihalali?

Wahindi wanamiliki viwanda vikubwa achilia mbali hizo plot za square meter 600.

Nina jamaa mbongo Marekani amenunuwa shamba, wewe uko dunia gani?

Nenda South Africa Wabongo kibao wanamiliki nyumba zao kisheria.

Ndio maana ccm mnapeana sumu mmejaa roho mbaya vifuani mwenu.

Ndikumana amezaa na Irene Uwoya na amekufa, yule mtoto atalelewa na ccm?

Sasa mimi namkatia shamba langu Aziz Ki ili uvimbe upasuke kabisa.
We jamaa kumbe una ufahamu mdogo kiasi hiki??
 
Sio tu wanazaa hapa hata huko Ulaya wanafanya hivyo hivyo. Binadamu kashindwa kuonyesha namna ndoto ya RIP Martin Luther isivyo na maana.

Wale machotara wa timu za Ulaya ni matunda ya wachezaji wa kiafrika kuzaa kule miaka ile ya 2000 mwanzoni.

Musiala, Bellingham, Ndoye, Sane na wengine wengi tu wakati mimba zao zikiendelea kukua matumboni mwa mama zao wenyeji wa mataifa yao walikuwa na mawazo kama haya ya mleta mada, ya kutanguliza ubaguzi dhidi ya wageni lakini leo hii vijana wanatamba katika timu zao za taifa wazungu kinafiki wanashangilia magoli yao ni kiwango chao cha mpira.
Kila nchi Ina utaratibu wake, je utaratibu wetu ndio huo? Sheria zetu zinaruhusu?
 
Kama umiliki ni wa mtoto unamuonea wivu au ni nini? Yani hamtaki hata uwekezaji kidogo? Ardhi ni nini? Unataka huyo mtoto aende wapi kama kazaliwa hapa?
Unamuonea tu aliyeweka hii mada, sio yeye bali sheria zetu
Mtoto kuzaliwa hapa sio sababu, anaweza luzaliwa hapa Ila akaamua kuwa raia walipotoka wazazi wake. Lazima tujue kwanza mtoto ni raia wa wapi
 
Uchoyo Ni nn? Sheria zetu zinasemaje? Ni mleta mada ndio aloyetunga hizo sheria?
Uchoyo ni kuwa na imani inayopitiliza kwamba kila mgeni anataka kutuibia, matokeo yake tunazeeka na kuaga dunia bila ya kuendeleza kile tunachojaaliwa na Mungu.

Huo 'usisi' na 'umimi' unapokuwa umetujaa ndani yetu kwa kisingizio cha kulinda rasilimali unatunyima pia fursa nyingi zinazotupita kanda.
 
Sehemu kubwa ya Dunia,inawezekana kasoro tu.Ardhi ya za Zanzibar & Rwanda.


Ubaguzi na chuki kwa wenzio sio nzuri.
Hata mda huu nenda Congo utapata ardhi TU mbona.
Kichekesho ni kwamba ukiwa njiani unatoka Dar kwenda huko mikoani ukiangalia kushoto na kulia kuna ardhi nyingi tu haijaguswa mpaka leo tangu tupate uhuru 1961.

Sisi wenyewe hatuna ubunifu kwani elimu zetu hazitupi udadisi wa kimaisha na hilo ni kosa la kisera limekuwa likirudiwa miaka na miaka.

Mawazo ya hiki ni chetu au cha kwangu yanatupotezea fursa nyingi na sio makosa ya wageni wanaokuja kutaka kuwa wabia wetu katika kufanya miradi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom