Namna ya kujilinda na kuwa salama unapokuwa Bar

Namna ya kujilinda na kuwa salama unapokuwa Bar

Baada ya taarifa kutoka Mwanza ya kuwa kijana ameuliwa na mabaunsa wa Bar, nimeona nitoe elimu kidogo ambayo haitolewi popote

Hii ni elimu ya mtaa

1. Bar sio sehemu ya watu wanyonge.
Ukijua wewe ni mlaini usikanyage bar au night clubs, watakupiga wakuuwe

2. Hakikisha una kampani.
Kampani itakuhakikishia usalama ndo maana matajiri hulipa machawa na wapambe ili kuwa na ulinzi kipaumbele

3 kuwa na silaha iwe ya jadi au ya moto
Bar hasa usiku Kuna ubabe kwaiyo kuwa na mguu wa kuku ni vyema zaidi.
Watu makini Huwa hawaendi bar chukuchuku

4 Kagua milango ya kutokea na kutoroka in case emergency ya fujo ikitokea.
Masela laZima wajue Chocho zote za ku escape labda ukiishiwa pesa na huku ushakunywa bia

5. Kuwa na usafiri au nauli. Sio unalewa pesa zote, wahuni watakufanya vibaya.

6. Achana na mademu wa bar.
Wajanja hatuchukuaji mademu wa bar, hawa ni j
Hatari kwanza wanakuletea maadui usiowajua au hata wao kukudhuru

7 Epuka migogoro isiyo ya laZima.
Usilete usela mavi, bar Kuna wahuni wamepinda na washalewa kukumwaga ubongo hawachelewi

8. Epuka rafiki mpya wa bar
Usijenge sana urafiki na mtu ambaye ndo umekutana nae kwenye pombe

9. Usitafute umaarufu bar, watakuwa wahuni
Kunywa bia, dance, kula ondoka acha misifa

10. Wape tip kiaina hao mabaunsa ili ukizingua wawe upande wako

Soma Pia: Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000
Bar ni mlango wazi wa kuelekea kuzimu, period! Jitahidi kadri uwezavyo, usipazoee.
 
Nimekubali na nitazidi kukubali kuwa bar zina fujo. Lakini siyo kwa kiwango ulichoweka wewe na zile tahadhari. Haya; umeingia bar na kisu au bastola halafu mlevi chakari akakutuka na kukutapikia, silaha itasaidia nini? Hata akikuzaba kibao, silaha itasadia nini? Mimi nazungumzia kutokana na uzoefu. Kama hutaki kisikia ushauri wangu basi endelea kuingia na silaha kwenye ulevi.
Bar sio sehemu ya kinyonge
Matukio hayatokei mara Kwa mara ila Kuna siku likitokea ukiwa upo kizembe utaukumbuka huu uzi
 
Maduka tisa ndo paki ngese sana pale sku moja chupchup mude wangu apgwe chupa imeerushws chupa na wakurya wa nyanshana walikua wanagombana yan staki kukumbuka kule wezi wote ndo wanapga starehe wanaishi mtaa wa msumbij
Eti wakurya wa nyanshana🤣
Duh pole maduka 9 wahuni na malaya ndio wengi zaidi ndiomaana bucket ilifungwa!
 
Back
Top Bottom