Namna ya kujilinda na kuwa salama unapokuwa Bar

Namna ya kujilinda na kuwa salama unapokuwa Bar

Baada ya taarifa kutoka Mwanza ya kuwa kijana ameuliwa na mabaunsa wa Bar, nimeona nitoe elimu kidogo ambayo haitolewi popote

Hii ni elimu ya mtaa

1. Bar sio sehemu ya watu wanyonge.
Ukijua wewe ni mlaini usikanyage bar au night clubs, watakupiga wakuuwe

2. Hakikisha una kampani.
Kampani itakuhakikishia usalama ndo maana matajiri hulipa machawa na wapambe ili kuwa na ulinzi kipaumbele

3 kuwa na silaha iwe ya jadi au ya moto
Bar hasa usiku Kuna ubabe kwaiyo kuwa na mguu wa kuku ni vyema zaidi.
Watu makini Huwa hawaendi bar chukuchuku

4 Kagua milango ya kutokea na kutoroka in case emergency ya fujo ikitokea.
Masela laZima wajue Chocho zote za ku escape labda ukiishiwa pesa na huku ushakunywa bia

5. Kuwa na usafiri au nauli. Sio unalewa pesa zote, wahuni watakufanya vibaya.

6. Achana na mademu wa bar.
Wajanja hatuchukuaji mademu wa bar, hawa ni j
Hatari kwanza wanakuletea maadui usiowajua au hata wao kukudhuru

7 Epuka migogoro isiyo ya laZima.
Usilete usela mavi, bar Kuna wahuni wamepinda na washalewa kukumwaga ubongo hawachelewi

8. Epuka rafiki mpya wa bar
Usijenge sana urafiki na mtu ambaye ndo umekutana nae kwenye pombe

9. Usitafute umaarufu bar, watakuwa wahuni
Kunywa bia, dance, kula ondoka acha misifa

10. Wape tip kiaina hao mabaunsa ili ukizingua wawe upande wako

Soma Pia: Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000
Shida yote hii unaenda kutumia hela yako.
 
Sasa wewe ndio utafanywa kibudu siku ikikutokea huna pesa. Bora bar moja ili ikitokea hela imeisha wanajua hata kesho utaleta. Kimedani zaidi mgeni akiingia tu unaanza kumnusa na kumfuatilia na kujihami, isije ikawa walewale

Mwanaume huna pesa unaenda bar kufanya nini?
Hela imeisha, unaendelea kukaa bar kufanya nini?
 
Huko sio bar ni Darful aisee..!! 😹😹
Hizo bar za mateja na machizi watu timamu hazitufahi..!!

Sema ikitokea huko mtu kanizingua sihitaji silaha, hizo chupa ndo silaha zenyewe lazima nimpasue nazo mtu. Sijawahi kufail kwenye target…!!
Wale mabaunsa hawapo kwa ajili ya kupiga wanawake wanawake wakizinguana hua linaitwa pila kuja kuwachukua ila mwanaume ukizingua utapigwa mpaka pila lifike ushakufa kitambo nishashuhudia jamaa anachezea vitasa mfululizo kwa kujifanya yeye mbabe akampiga muhudumu mangumi yaan walipotokea wanaume kuja kumkabiri alichezea za uso mpaka midamu sasa imagine unakuta mwingine hakuachi anakugonga mpaka ufe kabisa
 
Back
Top Bottom