Nampongeza mzazi aliyemfuata mtoto wake shule na HELIKOPTA. Ni matumizi sahihi ya Utajiri

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Nimeona video moja, mzazi ametuma HELIKOPTA kwenda kuchukua mtoto mwanafunzi shuleni huko bukoba baada ya shule kufungwa.

Jamaa simfahamu ila nampa pongezi sana maana ndio matumizi halali ya Pesa .

Huwezi KUWA na pesa mingi alafu uzao wako unaishi kifukara KWA hofu kwamba watabweteka kimaisha. Huu mtazamo anao Billionea Wallen Buffet. Watoto wake hawaenjoy utajiri wake.


Kama unapesa nyingi, KWA nini utumie masaa 10 unasafiri wakati watu wamshabuni vyombo vya moto ya angani KWA DAKIKA tu?

Jamaa nimemkubali sana.
Abarikiwe zaidi na watokee wengi nchini ili kuwapa challenge MATAJIRI wenye fikra za kijima na kimasikini.

UPDATE
Kwa mujibu wa wadau ile habari haina ukweli ila maudhui ya habari yanapaswa kuzingatiwa. Ukiwa na Pesa zitumike kunufaisha familia kwanza. Usijibane kupanda bus wakati ungenunua Ndege na pesa unazo.

Ni hilo tu
 
Haikuwa kweli.
Nilimsikia mkuu wa shule, aliongea na Clouds, na hakuna mamlaka zozote zilizotoa kibali helcopter kutua shuleni.
Kama haikuwa kweli lakini ni jambo jema sana kama likifanyika.
Kama chombo kinatua hata juu ya mtu mamlaka zipromote watu wenye pesa halali wanunue hizo mashine, wapewe vibali. Helikopata isikuzwe sana ichukuliwe kama chombo lingine cha usafiri kama Baiskeli, Bus, Boda n.k
 
Unashabikia hela za watu wengine wewe unajua kuzitafuta
Nampongeza KWA matumizi Bora ya Pesa.
Sio mtu anang'ombe 2000 lakini mtoto anakufa KWA Kwashakoo. inatakiwa Serikali izitaifishe hizo ng'ombe maana utajiri uko kwenye mikono hatarishi KWA usalama wa raia ( watoto wa Tajiri).

Kuongeza sio kushabikia
 
Nyie ndo wale mnaoamini kila kitu mnachoona kwenye mitandao ya kijamii
Hata kama ni uongo, ila wazo Lile liko sawa sana. Wasanii na MATAJIRI wakubwa wakiwa na private jet KWA masafa marefu na HELIKOPTA KWA ajili ya safari za ndani. Watakuwa wametatua changamoto za foleni na ubovu wa miundombinu nchini.

Huwezi kucheleweshwa au kuchelewesha familia kisa unasubiri Serikali itatue changamoto za miundombinu. Unanunua chombo cha moto cha anga na unasomba mbele KWA kuzingatia vigezo na masharti ya TCAA.
 
Na bati zetu hizi zenye kutu ukitua hovyo utalipa fidia mtaa mzima.
 
Nampongeza KWA matumizi Bora ya Pesa.
Sio mtu anang'ombe 2000 lakini mtoto anakufa KWA Kwashakoo. Unatakiwa Serikali izitaifishe hizo ng'ombe maana utajiri uko kwenye mikono hatarishi KWA usalama wa raia ( watoto wa Tajiri).

Kuongeza sio kushabikia
Sasa huyo mwenye ng'ombe 2000 na mtoto anakufa kwa kwashiakor na serikali hiyo unayoitaka izitaifishe hizo ng'ombe wote wako sawa.

Serikali yetu chini ya CCM imeshindwa kutumia vyema baraka za Mungu za rasilimali kibao tulizobarikiwa kwa kuinua maisha ya Mtanzania kiasi mama mjamzito anapoteza maisha kwa kukosa 70,000 ya kujifungulia!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…