Nampongeza sana Aslay Mihogo, vijana kuweni wabunifu

Nampongeza sana Aslay Mihogo, vijana kuweni wabunifu

Mara nyingi hua naenda kula mihogo na Samaki hapo Coco huku nikiburudishwa na nyimbo za wale vijana, siku hiyo nikasema nikapaangalie hapo kwa Aslay Mihogo, dogo amejua kujibrand ila hakuna tofauti yoyote na wafanyabiashara wenzake wa hapo Coco
Sema kabichi lao la kibabe sana aiseee wanalileta bichi hivyo hivyo tutafune kama sungura 😄
 
Last week nilipita pale nikapata zangu Samaki na Mihogo swaaaafi kabisa. Hio ni baada ya kuona matangazo mbali mbali instagram kuhusu Aslay Mihogo

Vijana kuweni wabunifu, huyu anakuchanganyia Samaki na Mihogo hadi unajiramba ramba.

Basi aje mrembo mmoja PM kesho niende nae tena
Hivi mnajua maana ya neno ''ubunifu''? Samaki kama hawa na mihogo tumekuwa tunakula miaka zaidi ya 20 iliyopita. Kinondoni kuna chochoro nyingi tu watu walikuwa wanakaanga jioni na kachumbari nzuri sana. Social media ndiyo inakufanya udhani ni kitu kipya?
 
Nakula vingi tu ila siwezi kwenda mahali pa kula bata nianze kula mihogo, ugali, maharage au dagaa. Ila combo ya mihogo na Samaki popote pale ni uzushi mtupu kwangu.
Hiyo sio sehemu ya bata Yoda, ni ya kula tu. Hapo mi sijawahi enda.

Hata nyumbani huli muhogo na samaki?
 
Back
Top Bottom