➡YESU KRISTO alijaribiwa kwa udanganyifu na shetani kwa mtindo na maneno kama haya yako kwenda kwa Tundu Lissu, kwamba aachane na mpango wake kuwakomboa watu na ulimwengu ili mradi tu amjudie shetani na angempa utajiri wa fedha zote, madini yote, ardhi yote na fahari zote za dunia hii...
Soma Biblia yako hapa👇🏻
Mathayo 4:8-9 SUV
"...Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia....."
Ulinganifu wa hoja hii ya shetani kwa YESU KRISTO dhidi ya hii yako kwa Tundu Lissu : WEWE unataka/unamshauri Tundu Lissu amsujudie shetani aliye ndani ya Samia na CCM ili apate milki na fahari (pesa, maisha ya anasa nk) lakini ndugu zake (wananchi wenzake, Watanzania) wabaki kwenye vifungo (bondage) na mateso ya utawala wa kishetani wa CCM wa miaka 64.
➡Jibu la YESU KRISTO kwa shetani:
Mathayo 4:10 SUV
".....Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake...."
➡Najaribu kujiuliza swali hili: Kwamba hivi YESU KRISTO angeikubali hongo/rushwa hii kwa tamaa zake za kimwili, mimi na wewe tungekuwa wapi leo? Tungekuwa na hali gani leo...???????
Anyways, hebu tuendelee kuona majibizano haya yaliishaje..
➡Baada ya ushawishi na udanganyifu huu wa kiovu wa shetani huyu kushindwa mwisho wake ukawa nini....?
Soma hapa👇🏻👇🏻
Mathayo 4:11 SUV
".....Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia...."
Swali kubwa kwako
Best Money ni hili:
Kwa muktadha huu, wewe ni nani?
➡Bila shaka wewe
Best Money ni shetani yuleyule aliyemwendea YESU KRISTO na kutaka kumwingiza mkenge ili aharibu kusudi la Mungu la kuukomboa ulimwengu toka kwa huyohuyo shetani kwa tamaa ya mali, fedha na maisha ya kupenda anasa za kupita za dunia hii...
➡Kama haikuwezekana kwa YESU KRISTO, haitawezekana kwa mkombozi wetu Tundu Lissu...!
Biblia inasema hivi:
➡Baada ya shetani kushindwa kumdanganya YESU KRISTO, Ibilisi/shetani alimwacha, tazama malaika (yaani mbingu) wakaja na kumhudumia na kumpatia kila alichohitaji kwa njia ya halali inayokubalika mbele za Mungu...
➡Tundu Lissu ameshashinda kila jaribu. Hakuna binadamu wa kumuua au kumdanganya au kumhonga kwa lolote ili aisailiti nchi na watu wake...
➡Hakika, Ibilisi/Shetani CCM/ Samia atachoka mwenyewe tu na mbingu na malaika wamekuja na kumhudumia Tundu Lissu na NCHI NA TAIFA HILI LIMEKOMBOLEWA TAYARI. Bado kitambo kidogo tu idhihirike kwa macho ya mwili na nyama ya kila mtu mwenye mwili wa nyama na macho haya..!!
Mungu ktkt Yesu Kristo akurehemu na aondoe ujinga wa fikra na akili ulio kichwa mwako ili upate maarifa na ufahamu...
➡Lakini, Kumbuka na weka kichwani mwako hili, kuwa, Mungu Yehova yuko kazini kuikomboa nchi na taifa hili toka kwa hayawani waitwao CC kupitia watumishi wake wengi mmoja wao akiwa ni Tundu Lissu...!