Namtafuta mwanaume atakayekuwa tayari kumuoa dada yangu

Namtafuta mwanaume atakayekuwa tayari kumuoa dada yangu

Sisi shughuli kama hii hatuiiti ukuwadi.Ni mafunzo ya dini yetu kutafuta kheri kwa tuwapendao wakiwemo dada zetu na watoto wetu.
Wallah umemjibu vizuri ,,binafsi sijawahi kujishughulisha kutafuta mke ,,yaan Mara zote nilizooa marafiki zangu huwa wananiambia TU kule Kuna nusra ,,Ni kheiry nyingi Sana wazipatazo wenye kuunga undugu
 
Weka namba
Si kwamba mume wa dada yangu kapotea ndio namtafuta, hapana. Ni kwamba dada yangu hana mume na natafuta atakayekuwa tayari na atakayefaa kumuoa.

Dada yangu amewahi kuolewa na ana mtoto mdogo. Ni mzuri wa umbo na mcheshi sana. Tangu alipoachika amejishughulisha kutafuta riziki zake za halali mpaka amefanikiwa kujenga kijumba chake.

Anachotaka sasa ni mume wa kuishi naye kwenye nyumba yake na kumpatia huduma akitamani kuzaa mtoto mwengine haraka. Mwenyewe huwa nampatia huduma zote muhimu isipokuwa moja ndio naomba msaada.
Umri wake ni miaka 32 na ukewenza si tatizo kwake ilimradi mume awe muwajibikaji.

Sharti moja muhimu la huyo mume mtarajiwa awe ni muislamu na mwenye kufanya ibada vizuri. Ambaye yuko tayari awasiliane nami binafsi ndani ya boksi tuone wapi pa kuanzia.

Dada mwenyewe ni mmoja katika hao hapo chini.

360_F_210510641_C3KC65UupFXlgrkX0rv9hv1ZAuSCb1Ld.jpg
Weka namba ili tukutafute, PM hatuji🤪
 
Nachokaga kabisa kusikia hilo neno...kwamba sasa hivi hajajistiri?😆
Labda pengine hujaelewa........

Mwanamke ni kiumbe Cha thamani sana chini ya jua kama tu ataijua thamani yake.......ndio maana mwanamke akikithiri kwenye matendo machafu jamii inamshangaa kuliko mwanaume akifanya........

Katika dini mwanamume ni kiongozi na muangalizi wa mwanamke......mwanamke akipata mume ambaye anamhudumia huduma zote maana yake amamuondolea aibu zake........na hiyo ndio stara.....sote tunafahamu macho na mitazamo ya wana jamii juu ya mwanamke mzinzi ukilinganisha na mwanaume mzinzi.........
 
Ukisikia kuuziwa mbuzi kwenye gunia ndio huku. Hata kwato hatuzioni wakti mbuzi Yuko sokoni?
 
Back
Top Bottom