Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
10,771
Reaction score
14,129
GTs,

Kama tulivyoona kijana wa Waziri Simba Simbachawene alivyoingia kituoni halafu kuna askari akamchokoza kwa tusi. Je, hiyo ni sahihi? Je, ni kweli alitukana na alipokuwa nje, na je ndiyo njia sahihi ya askari kufanya kazi?

Je, haki za kijana wa Simbachawene zilifuatwa, au alitishiwa na hao askari ili atoe rushwa ila baada ya hao askari kujua ni mtoto wa kiongozi, ikabidi wamrekodi na kumchokoza ili akasirike warekodi na kumdhalilisha?

Video uliyorekodiwa iko ki mkakati zaidi kwa sababu hakuna hata sehemu tumemsikia dogo akijitapa yeye ni mtoto wa Mh. Simbachawene.

Naamini Jeshi la Polisi litafanya uchunguzi ili kubaini hasa kitu gani kilitokea. Maana hao askari inaonekana walijipanga kuhakikisha dogo wana mdhalilisha.

Na kibaya walilenga kumdhalilisha Simbachawene, na huyo kijana inaonekana ni mtu mwenye heshima na anajitambua ila hao askari walimtengenezea mazingira baada ya kuona wamekosea ili kujikosha kwa jamii.

Ila mtindo wa askari ndiyo huo kudhalilisha na kusumbua ili wapate rushwa.

Naamini Simbachawene atamlinda mwanae, akiwaachia hao askari Polisi wamshughulikie mwanae wanaweza kufanya yale ya Mtwara.

Chondechonde Simbachawene, hukupaswa kabisa kutoa ruhusa mwanao ashughulikiwe wanaweza kumuua ili wapoteze ushahidi maana mifano ipo mingi ya askari kuua watuhumiwa ili kuficha ushahidi.

1661269272654.png



 
Alitoka ELEMENT kulewa SAA 11 asubuhi akabutua/akagonga gari mbili ikiwemo Passo ya mnyonge mmoja wakamfukuzia wakamdaka ndio ukaona hayo uliyoona!..
Hapana hao askari ni waongo. Yule dogo siyo kichaa afanye hayo aliyoyafanya. Nina uhakika kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Kuna mtu mmoja siku moja Dar alikuwa hizi hoteli za uswahilini, tena ni dereva wa serikali, sasa askari wakapita walikuwa na ukaguzi wa kawaida.

Basi wakamgongea mshikaji akafungua, bahati mbaya jamaa alikuwa kaweka waleti yenye hela zimetuna na zingine zimetokezea (zilikuwa per diem na mafuta ya safari), basi yule askari alivyoona jamaa alipigwa bonge la kofi na mateke bila hata kumuuliza na akasema nyie ndiyo majambazi tunawatafuta.

Baada ya hapo jamaa kapigwa pingu na kupelekwa mahabusu, alijitahidi kujielezea wapi, akaenda kuwekwa mahabusu na waleti yake na hela zimechukuliwa.

Wakaanza kumuandikisha maelezo yeye kama jambazi. Bahati nzuri alifahamiana na watu, yule askari alifukuzwa kazi baada ya kujulikana ukweli.

Naamini watoto wa viongozi wanapaswa kupewa heshima na siyo kuwadhalilisha.
 
GTs,

Kama tulivyoona kijana wa Mh. Simbachawene alivyoingia kituoni halafu kuna askari akamchoza kwa tusi. Je, hiyo ni sahihi? Je, ni kweli alitukana na je, ndiyo njia sahihi ya askari kufanya kazi?

Je, haki za kijana wa Mh. Simbachawene zilifuatwa, au alitishiwa na hao askali ili atoe rushwa ila baada ya hao askali kujua ni mtoto wa kiongozi, ikabidi wamrekodi na kumchokoza ili akasirike warekodi na kumdhalilisha?!

Naamini jeshi la polisi litafanya uchunguzi ili kubaini hasa kitu gani kilitokea. Maana hao askari inaonekana walijipanga kuhakikisha dogo wana mdhalilisha.

Na kibaya walilenga kumdhalilisha Mh. Simbachawene, na huyo kijana inaonekana ni mtu mwenye heshima na anajitambua ila hao askari walimtengenezea mazingira baada ya kuona wamekosea ili kujikosha kwa jamii. Ila mtindo wa askari ndiyo huo kudhalilisha na kusumbua ili wapate rushwa.
Ni askari sio askali mkuu.
 
Kumbe alikimbia ?,yeye nimesikia anasema walitaka kumpiga, ila Kuna vitu hao jamaa wamemkosea hawasemi tu

Mfano wanadai kakejeri passo, huenda walimkera
Ndiyo maana tusimhukumu dogo, uchunguzi ufanyike. Simbachawene hana shida kabisa na huyo dogo hatujawahi kabisa msikia ukorofi wake. Ukiangalia vizuri hao askali nina uhakika walitaka kumpiga/rushwa na walimdhalilisha ila walipogundua mtoto wa kigogo wakaona wataenda kuchomewa, ikabidi haraka wamseti.
 
Element bia za local Ni 5500 za njje Ni kunzia elf 8000. Dogo katoka asbh kaenda kubutua tozoo zetu na ikimbukwe hakuwa Pekee ake pale element atakuwa kaacha milioni kwaone night ambazo hakika Ni uhakika Nia tozo zetu katoka kuziponda

All in all maskar na yule mwenye passo ndoo alikuwa anaongea maneno yasio na stah na lema nae wachadema amekimbia Twitter kujifanya kuwayey anajuwa kulea na simbachawene alimlea mtot vibaya siyo kweli hata yet asubiri wanae wakue ndio atajuwa kuwa alikozea au kapatia


Pila lema asijisahau alivyo kuwa muhuni akiwa kolila high school na akiwa mjini Arusha kufanya utapeli wa magari asisahau Hilo je Ni kwamb wazazi wake walimlea vibaya

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe alikimbia ?,yeye nimesikia anasema walitaka kumpiga, ila Kuna vitu hao jamaa wamemkosea hawasemi tu

Mfano wanadai kakejeri passo, huenda walimkera
Wamemrekodi clip nyingi nyingi tu kuanzia nje hadi ndani ya kituo, na wao wana makosa. Aligoma kuingia kituoni ikabidi wamfosi wakawa wanamsukuma ndio maana akawa anatukana pale ndani ya kituo na yeye anataka kulipwa kwa kudhalilishwa
 
Mi sijui hata mnataka kutetea Nini hapa. Hebu Kuna kipindi acheni ushirikina nyie watu. Yaani baada ya kuona hizo clip zote Bado mnataka kumtetea? Ama kweli watanzania nyoko asee.
Askari wetu tunawajua ndiyo maana unahitajika uchunguzi, maana hii ni stori ya upande mmoja. Kila dereva hii Tanzania alishawahi kudhalilishwa na askari na kama huna cheo au kufahamiana na wakubwa basi unaweza fungwa au kubambikiwa kesi. Kitu cha kujiuliza tu je kulikuwa na haja gani ya kumwambia dogo kuhusu hilo tusi? Na je kwa nini hilo tusi hawakulirekodi?? Walijua wameshampanikisha na wakawa wanamtega kumdhalilisha yeye na Mh Simbachawene.
 
Kwahiyo ukigoma kuingia kituoni unatakiwa ubembelezwe hadi saa ngapi?
Kwani uaambiwa aligoma? Kuna siku askari mmoja kamkata mshikaji na kwa sababu ya kutaka rushwa akampeleka kituoni na akazuia gari, unaambiwa alilia kuomba msamaha. Polisi wakikupeleka kituoni maana yake utoe rushwa kubwa
 
Askari wetu tunawajua ndiyo maana unahitajika uchunguzi, maana hii ni stori ya upande mmoja. Kila dereva hii Tanzania alishawahi kudhalilishwa na askari na kama huna cheo au kufahamiana na wakubwa basi unaweza fungwa au kubambikiwa kesi. Kitu cha kujiuliza tu je kulikuwa na haja gani ya kumwambia dogo kuhusu hilo tusi? Na je kwa nini hilo tusi hawakulirekodi?? Walijua wameshampanikisha na wakawa wanamtega kumdhalilisha yeye na Mh Simbachawene.
...So Kama Halikurekodiws Unajuaje kwamba lilisemwa???
 
Back
Top Bottom