Hapana hao askali ni waongo. Yule dogo siyo kichaa afanye hayo aliyoyafanya. Nina uhakika kulikuwa na mazingira ya rushwa.
Kuna mtu mmoja siku moja Dar alikuwa hizi hoteli za uswahilini, tena ni dereva wa serikali, sasa askali wakapita walikuwa na ukaguzi wa kawaida.
Basi wakamgongea mshikaji akafungua, bahati mbaya jamaa alikuwa kaweka waleti yenye hela zimetuna na zingine zimetokezea (zilikuwa per diem na mafuta ya safari), basi yule askali alivyoona jamaa alipigwa bonge la kofi na mateke bila hata kumuuliza na akasema nyie ndiyo majambazi tunawatafuta.
Baada ya hapo jamaa kapigwa pingu na kupelekwa mahabusu, alijitahidi kujielezea wapi, akaenda kuwekwa mahabusu na waleti yake na hela zimechukuliwa.
Wakaanza kumuandikisha maelezo yeye kama jambazi. Bahati nzuri alifahamiana na watu, yule askali alifukuzwa kazi baada ya kujulikana ukweli.
Naamini watoto wa viongozi wanapaswa kupewa heshima na siyo kuwadhalilisha.