Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Kwanza nianze kwa kukiri ya kuwa pamoja ya kuwa Mimi ni mtu mzima, na mtoto wa Askari polisi aliyetukanwa sijapokea na kumsamehe Joji Simbachawene.

Siwezi msamehe Mh Waziri Simbachawene kamwe na Sitofanya hivyo maana Baba yangu mzazi amefedheheshwa sana sana sana sana mbele ya macho ya umma.

Siwezi kubali hakika ya kuwa Baba yangu atukanwe kwani yeye ndiye aliyenizaa Mimi Nina hakika ila sio sana maana mwenye hiyo hakika ni mama yangu.

Ila nimeamua kwenda mbele zaidi baada baba kurudi nyumbani kimefanyika kikao kizito cha kujadili ilihali wa baba yetu aliyetukanwa, Ili kudhibitisha yakuwa sio kweli tusi alilotukanwa na sisi tu wanae.

Katika kikao hicho tumekubaliana yafatayo.

Kwanza watoto wote tufanyiwe vipimo vya DNA testing.

Pili Ikibanika tu Wana wa baba mmoja basi baba atukubalie sisi tufungue kesi dhidi ya Simbachawene kwa malezi yake mabaya kwa vijana nguzo ya Taifa hili.

Niliwahi jiuliza Kwanini mwendazake aliwahi mwambia Simbachawene yakuwa hakuwa Ikulu kuuza sura? Sasa naanza pata majibu.
 
Shida kubwa sana ipo kwa jamaa zetu.
Tukio limetokea namba za gari mmezipata, mmiliki mnamfahamu, kuna haja gani kumkimbiza?

Shida imetokea hakuna kifo, wahusika wapo tayari kuyamaliza Nyie mnang’ang’ania twende kituoni, wakafanye nini?.

Ila pia kuna kipimo cha pombe ili kuthibitisha kiasi alicholewa dereva, je hicho kilifanyika?

Ya wezekana alikuwa element anakunywa Maji.

Hivi leo hii wakipanda mahakamani nani anashinda kwa mazingira kama hayo.?

Kila mtu akitimiza wajibu wake hatuwezi fika huku.
 
Hapana hao askali ni waongo. Yule dogo siyo kichaa afanye hayo aliyoyafanya. Nina uhakika kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Kuna mtu mmoja siku moja Dar alikuwa hizi hoteli za uswahilini, tena ni dereva wa serikali, sasa askali wakapita walikuwa na ukaguzi wa kawaida.

Basi wakamgongea mshikaji akafungua, bahati mbaya jamaa alikuwa kaweka waleti yenye hela zimetuna na zingine zimetokezea (zilikuwa per diem na mafuta ya safari), basi yule askali alivyoona jamaa alipigwa bonge la kofi na mateke bila hata kumuuliza na akasema nyie ndiyo majambazi tunawatafuta.

Baada ya hapo jamaa kapigwa pingu na kupelekwa mahabusu, alijitahidi kujielezea wapi, akaenda kuwekwa mahabusu na waleti yake na hela zimechukuliwa.

Wakaanza kumuandikisha maelezo yeye kama jambazi. Bahati nzuri alifahamiana na watu, yule askali alifukuzwa kazi baada ya kujulikana ukweli.

Naamini watoto wa viongozi wanapaswa kupewa heshima na siyo kuwadhalilisha.
Eee stori yako inasikitisha sana hawa askari wenu ni warafiii balaa.. ila kuhusu watoto wa viongozi kuheshimiwa hapo hapana kila mtu amuheshimu mwenzake tu.
 
Mapya yaibuka
Kumbe jamaa askari waliomba rushwa ya laki moja , baadae wakashuka hadi elfu hamsini tena walimuomba kwa vitisho lakini akagoma, baadae aliposema Baba yake ni fulani ni waziri ndio wakastuka wameingia choo cha kike wakamgeuzia kibao.

Askari wetu nao njaa zimezidi ndio maana wanatukanwa tu matusi ya wazi wazi.

Kwa nini waombe rushwa kwanza?
 
Kama kweli usemalo basi baadhi ya traffic police nao ni shida....mtu kashafanya uharibifu na amelewa, wanataka atoe rushwa ili wamuachie akasababishe ajali nyingine mbele!?

Pamoja na hilo kama kweli lilikuwepo, bado halifanyi mtuhumiwa atukane na kudhalilisha jeshi la polisi. Kijana ana dharau sana yule
 
Mi sijui hata mnataka kutetea Nini hapa. Hebu Kuna kipindi acheni ushirikina nyie watu. Yaani baada ya kuona hizo clip zote Bado mnataka kumtetea? Ama kweli watanzania nyoko asee.
wapate chochote kituu mkuu,. si unajua uchawa/kuuza utu ndo biashara inayolipa mjini
 
Kumbe alikimbia ?,yeye nimesikia anasema walitaka kumpiga, ila Kuna vitu hao jamaa wamemkosea hawasemi tu

Mfano wanadai kakejeri passo, huenda walimkera
Kwann watoe clip au warekodi? Tcra wamekaa kimya wanasubiri sisi paukwa tupogwe fine
 
Hao Askari ni wapuuzi wooote hapo kituoni...tena wanastahili kuhamishiwa kijijini kusiko na umeme na maji

1.Dogo alikuwa mlevi na twajua pombe sio chai angeweza hata kuvua nguo je wangerusha picha zake?
Mtu yuko tungi tungi bado unamtegeshea kamera ili iweje?kama hawakuwa na nia ovu ya kumdhalilisha waziri?

2.Always protect your Superior...hao Askari baada ya kujua ni mtoto wa bosi wao na yuko mtungi wangemsukuma ndani faster kumficha toka kwenye macho ya umma.

3. Quickly wamemtaarifu mzee wake kuwa mwanao tumemficha hapa kituoni kuna msala kafanya na yuko tungi

4. Naamin Simbachawene angeagiza fanyeni Assessment waathirika wanataka nini au shilingi ngapi nimalizane hao ndani ya dakika kumi watawanyike

5. Baba yake angemaliza Jambo juu kwa juu sasa hapo ndio angejuana na mwanae njee ya macho ya umma
 
Binafsi nilishangaa sana watu walivyomshambulia mwana wakati video zenyewe ni vipande vipande.

Na kuna sehemu alikuwa anasema wamlipe walimsukuma hii inaonyesha kabisa kulikuwa na sintofahamu kubwa ambayo hiyo video haionyeshi. Ila wabongo na hasira za Tozo wakaamua kumshushia makasiriko yao.
 
Back
Top Bottom