Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Exactly, hao Askari kweli wamekosea ,hapo lengo kumdhalilisha waziri
 
Kwa namna moja au nyingine niko upande wa dogo.

Mwanzo dogo alikua ni kama anaelekeza jinsi ilivyokua, lakini kuna wapuuzi walikua wanamchochea kichizi na ukizingatia alikua maji basi kupanick ni dakika 0.

Wamempanikisha mpaka akaanza kutema shit sasa, akitema shiti wao hawapanick bali wanazidi kumseti ateme shit zaidi.

Hata kwa huyo askali aliemuuliza eti unamuita mwanaume mwenzio msen** nae ni katika harakati za kumjaza upepo dogo. Na dogo nae akajaa mzima mzima akatema shit tena.

Pole kwa hao watu waliotukanwa na chalii.
Na kibaya/kizuri zaidi hawawez mfanya chochote huyo dogo, mzee wake anawajua wabongo kwa mihemko na wala sio wafatiliaji.
 
Exactly, hao Askari kweli wamekosea ,hapo lengo kumdhalilisha waziri
Tena wanarekodi inamaana askari kazi zao siku hizi imekuwa uandishi wa habari??? Yaani hawafai hata kutunza siri. Ina maana hata wakimkuta Rais Samia anapata ki wine chake wanaweza kutoa siri oh Rais anakunywa wine mchana. Yaani wameharibu sana kumdhalilisha Mh. Simbachawene.
 
Mh.Simbachawene unapaswa kuhakikisha kuwa unawalinda wanao kama baba. Tabia za askali wetu zinajulikana wengi wao wananapokuwa na hizo bunduki zao basi huona kuwa wanaweza kuwafanyia raia udhalilishaji wowote huku wakiwatishia kuwaweka ndani.
Tuhakikishe tunawalinda wanetu tukingali hai.
 

Simbachawene amewatega tu

Nani ana guts za kushughulika nae that much?
Unadhani Polisi mafala? Wanajua wanategwa pia
 
Askari wamemstahi sana dogo (wamemuogopa), dogo kaendesha amelewa, amesahabisha ajali kisha askari wamemkamata ja wanamuonyesha kiti akalie!

Customer care waliyoonyesha polisi kwa huyo dogo ni ya hali ya juu, angekuwa mwingine angepokelewa kwa mabanzi na kuamriwa akae chini sakafuni.

Vv
 
ikabidi haraka wamseti.
na ili ujue ni mchongo unatengenezwa,walikua wana record kila ujinga

hivi angekua kapuku wangekua wanarecord,hadi kituoni anarecordiwa

siku hizi vituoni askari wanaruhusiwa kurecord mtuhumiwa? kama si askari

alierecord,ina maana raia wa kawaida anaruhusa ya kuingia kituoni kurecord

video na simu yake? katika hili jambo POLISI ni wangese na namtetea sana huyu kijana

wamefanya jambo wakidhani wanamkomoa ila zaidi ni kujikomoa wenyewe na kudhihirisha upumbavu wao wa utendaji kazi wanapokua kazini mwao.

Nina amini huyu jamaa atatolewa,waziri kaandika vile public ili tu kuweka picha nzuri kwa wananchi,ila huko kituoni patachimbika, Kuanzia mrecord video mpaka mpost video,

hili jambo likikuzwa Kuna watu kazi wanakosa,vyeo vinanyofolewa,RIP JPM walahi angekuepo hili sakata likamfikia angepurua askari wote wa zamu na kijana kesi yake ingefika inapostahili ila lazima Kuna watu watajuta kupitia sakata hili.
 
tena nakukumbusha dogo amekutana na askari wastaarabu sana,angekutana navichwa vibovu yule angefurahi,nahivi baba yake hakuna alichowafanyia cha maana,then anamtaja taja kifala.
 
Hayo mambo ya mtoto wa Simbachawene yatakuja baadaye, sasahivi MLETE MZUNGU kwanza
 

upuuzi ni asili ya watanzania hawawezi kuwa nao askari peke yao.

1.video wakirekodiwa askari mnakata mauno kwamba ni ushahidi muhimu hasa wakiwa wanavua hizo nguo na kufanya mengine ya kujidhalilisha.wacha unafiki.

2.polisi boss wao ni serikali kwa ujumla wake,sio mtu mmoja mmoja,hata IGP hawamchukiliii kama boss waoi,simbachawene ni waziri mwenye historia ya kuwa waziri wa mambo ya ndani,hana mandate yeyote wizara hiyo kwa sasa.

3.simply,mzee kakutana na video mtandaoni,hakuna aliyejihangaisha kumtafuta baba yake wakati mtoto ni mtu mzima anayejitegemea na yuko tayari kujitwika msalaba wake kama alivyojitwika balimi.

4.hujui huyo mzee anaishi vipi na mwanaye,mpaka haraka kutoa tamko kali namna hiyo lisilo na kutafuna maneno.

5.hilo bado atalifanya hata sasa baada ya polisi kumalizana na mwanaye.
 
Simbachawene amewatega tu

Nani ana guts za kushughulika nae that much?
Unadhani Polisi mafala? Wanajua wanategwa pia
kwani unadhani watampiga risasi,ni kulipa gharama za gari alizozigonga na pesa kufuta kesi ya matusi aliyotukana.
 
weledi myfoot

msimponze huyo dogo watu wakaamua tu kumkomoa makusudi.
huyo baba yake wala hana ushawishi tena humo.
 
Usiseme hana ushawishi, serikali ni dude hata kama mtu katoka. Hao askari nina uhakika watafukuzwa ni waovu.
 
kuna mafala humu eti bado yanalaumu.

hawa wajinga kwa miaka 5 wa unanijua mimi nani huko nyuma walikuwa sandukuni sasa wameanza tena usumburu maana nchi ya majina imerudi.
 
Usiseme hana ushawishi, serikali ni dude hata kama mtu katoka. Hao askari nina uhakika watafukuzwa ni waovu.
uhakika unautoa wapi wewe[emoji28][emoji28]wafukuzwe kwa kosa gani???

huyo dogo ana bahati karekodiwa ashukuru,wengine wangemtia mitama waandike ni majeraha kayapata akiwa anagonga gari nyingine.

hawa askari ni wastaarabu sana tofauti na ninaowajua mimi.
 
siri unazijua wewe!!!

yeye kafanya upuuzi na akamtaja baba yake,kwamba nimefanya kwa sababu mimi ni mtoto wa simbachawene.
watu pamoja na hilo wakaamua kukomaa naye bado anatukana.

hivi unadhani huyo ndiye mtoto wa kwanza wa kiongozi kukamatwa na polisi???
 
Kumbe alikimbia ?,yeye nimesikia anasema walitaka kumpiga, ila Kuna vitu hao jamaa wamemkosea hawasemi tu

Mfano wanadai kakejeri passo, huenda walimkera
Kwa hiyo ukikerwa, inapaswa kurudisha kero..!! Hivi ile ya kujichukulia sheria mkononi, si huwa mtu anaanzwa halafu anatakiwa akaripoti?

BTW, DONT DRINK AND DRIVE..!!! Hilo pekee linatosha, achia mbali kuita wenzie wangese, na akaulizwa akarudia na akasema hajawahi kukaa polisi na hakuna kitu watamfanya..!! HUKU NI KULEWA MADARAKA YA BABA
 
Dogo kachemsha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…