Kwanza nianze kwa kukiri ya kuwa pamoja ya kuwa Mimi ni mtu mzima, na mtoto wa Askari polisi aliyetukanwa sijapokea na kumsamehe Joji Simbachawene.
Siwezi msamehe Mh Waziri Simbachawene kamwe na Sitofanya hivyo maana Baba yangu mzazi amefedheheshwa sana sana sana sana mbele ya macho ya umma.
Siwezi kubali hakika ya kuwa Baba yangu atukanwe kwani yeye ndiye aliyenizaa Mimi Nina hakika ila sio sana maana mwenye hiyo hakika ni mama yangu.
Ila nimeamua kwenda mbele zaidi baada baba kurudi nyumbani kimefanyika kikao kizito cha kujadili ilihali wa baba yetu aliyetukanwa, Ili kudhibitisha yakuwa sio kweli tusi alilotukanwa na sisi tu wanae.
Katika kikao hicho tumekubaliana yafatayo.
Kwanza watoto wote tufanyiwe vipimo vya DNA testing.
Pili Ikibanika tu Wana wa baba mmoja basi baba atukubalie sisi tufungue kesi dhidi ya Simbachawene kwa malezi yake mabaya kwa vijana nguzo ya Taifa hili.
Niliwahi jiuliza Kwanini mwendazake aliwahi mwambia Simbachawene yakuwa hakuwa Ikulu kuuza sura? Sasa naanza pata majibu.
Hii mada yako na ile ya wakili msomi
Pascal Mayalla zimedhihirisha namna gani makosa ya Tort ni mageni kabisa Tanzania.
Kikubwa kinachoangaliwa kwenye makosa haya ni :-
1.Duty of care
2. Breach of that duty
3.Demage
Sasa huyu ndugu Simbachawene ambaye naye ni msomi wa sheria kutoka chuo kikuu huria kama ilivyo kwa wakili msomi
Pascal Mayalla , je! ana duty of care kisheria kwa lijitu lizima ambalo limezidi miaka 18 na lina familia yake? Nadhani Simbachaweze ameamua kutokahadharani na kulaani kitendo hicho lajitu ka,a raia mwingine aliyekerwa na kitendo hicho cha kumdhoofisha afisaa akiwa anafanya kazi yake na tutambue kuwa bado simbachawene ni mwanafamilia wa taasisi hiyo kwani aliwahi kuwa waziri wake , hivyo kuna yale mahusiano ya kufaamiana kwaz kufanya kazi pamoja.
Kwangu mimi, kwa njia yoyote ile hutuwezi kumuunganisha Simbachawene kwenye ujinga alioufanya mtu huyu na sijawahi kusikia tort ya aina hiyo.
Tort kama ilivyo kwenye makosa ya jinai huwezi kuhukumiwa kwa kosa ambalo halipio kisheria (
Nulla poena sine lege ), Kadhalika baba wa Jurisprudence duniani Salmond alifafanua vilevile kuwa Tort nayo ina makosa yake, hivyo sio kila kitu utakifananisha na tort na kukipeleka mahakamani. Hapa alitolea ufafanuzi na kulinganisha na matundu ya nyumba ya njiwa kuwa ili njiwa aingie kwenye tundu lake lazima hilo tundu liwe na ukubwa ambao njiwa anaweza kukaa ( PEGION HOLE PRINCIPLE)
According to Salmond, “Tort is a civil wrong for which the remedy is a common-law action for unliquidated damages, and which is not exclusively the breach of contract, or, the breach of trust, or, other merely equitable obligation.”
Hivyo kwa maoni yangum wanaharakati wanaoliongelea hili, wanaongea kufurahisha jukwaa tuu au kwa sababu kuna mtu mkubwa katajwa lakini ilkienda mahakamani kama Simbachaweze atakuwa jointed inapigwa P.O asubuhi na mapema, lakini Polisi wana nafasi kubwa ya kumshitaki huyo kijana aliyefanya kosa hilo ( in his individual capacity) kwa makosa ya jinai cum usalama barabarani na Tort ikiwezekana ijapokuwa kupata UNLIQUDATED DEMAGES kwa askari kwa makosa ya tort yanayotokea kutokana na majukumu yake ni ngumu sana na hii nilisoma kesi nyingi za kizungu za askari waliopata madhara ya Post-traumatic stress disorder (PTSD) pale ambapo wanaposhukulikia matukio ya kutisha kama ajali, mauji nk na kuishia kupata mishtuko inayowaletea madhara ya kiakili na kimwili, kuna debate kubwa sana kwenye sheria kuhusu injury wanazozipata watu lakini hazionekani kwa macho na ni mbaya zaidi kuliko pysical injuries
Avogadro. LLB hons OUT