Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Hapana hao askali ni waongo. Yule dogo siyo kichaa afanye hayo aliyoyafanya. Nina uhakika kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Kuna mtu mmoja siku moja Dar alikuwa hizi hoteli za uswahilini, tena ni dereva wa serikali, sasa askali wakapita walikuwa na ukaguzi wa kawaida.

Basi wakamgongea mshikaji akafungua, bahati mbaya jamaa alikuwa kaweka waleti yenye hela zimetuna na zingine zimetokezea (zilikuwa per diem na mafuta ya safari), basi yule askali alivyoona jamaa alipigwa bonge la kofi na mateke bila hata kumuuliza na akasema nyie ndiyo majambazi tunawatafuta.

Baada ya hapo jamaa kapigwa pingu na kupelekwa mahabusu, alijitahidi kujielezea wapi, akaenda kuwekwa mahabusu na waleti yake na hela zimechukuliwa.

Wakaanza kumuandikisha maelezo yeye kama jambazi. Bahati nzuri alifahamiana na watu, yule askali alifukuzwa kazi baada ya kujulikana ukweli.

Naamini watoto wa viongozi wanapaswa kupewa heshima na siyo kuwadhalilisha.

Mkuu kama hautojali rekebisha, ni askari sio askali
 
GTs,

Kama tulivyoona kijana wa Mh. Simbachawene alivyoingia kituoni halafu kuna askari akamchoza kwa tusi. Je, hiyo ni sahihi? Je, ni kweli alitukana na je, ndiyo njia sahihi ya askari kufanya kazi?

Je, haki za kijana wa Mh. Simbachawene zilifuatwa, au alitishiwa na hao askari ili atoe rushwa ila baada ya hao askari kujua ni mtoto wa kiongozi, ikabidi wamrekodi na kumchokoza ili akasirike warekodi na kumdhalilisha?

Naamini jeshi la polisi litafanya uchunguzi ili kubaini hasa kitu gani kilitokea. Maana hao askari inaonekana walijipanga kuhakikisha dogo wana mdhalilisha.

Na kibaya walilenga kumdhalilisha Mh. Simbachawene, na huyo kijana inaonekana ni mtu mwenye heshima na anajitambua ila hao askari walimtengenezea mazingira baada ya kuona wamekosea ili kujikosha kwa jamii. Ila mtindo wa askari ndiyo huo kudhalilisha na kusumbua ili wapate rushwa.
Hivi alikuwa anaendesha gari akiwa amelewa au la?

Ukiwa mtoto wa kiongozi unapaswa kujua namna ya ku behave.
 
Lakini wasi wasi wetu ni hayo mazingira na tabia za polisi kubambika watu makosa, hii tabia yao ikomeshwe hao askari. Iwapo wakifanikisha iko siku watakudhalilisha hata wewe. Yaani polisi wajue saikolojia ya kudeal na watuhumiwa na siyo kutumia njia ambazo hazijengi.
Yaan kilichotokea hapa ni kutunishiana misuli..binafsi naheshimu sana askari...
 
Wanaopigwa picha ni watu wa aina gani ndugu yangu wakiwa wamefanya kosa.? Kwa sababu yeye ni mtoto wa rais amefanya kosa asipigwe picha kwa upuzi wake kisa ni mtoto wa rais.

Ebu kuwen siriasi. Kwenye mambo ya msingi. Hii issues ingekua kwa wenzetu wanaojielewa ingemuondoa simbachawen ofisin. Tatzo huku kwetu viongozi ni miungu watu. Na wakifanya la maana sana kuibua huu uovu.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
Kwa nini msinge mfinya kimyakimya Kama mnavyo fanyaga kwa wa halifu wengine!? Kulikua na ulazima gani wa kuchukua mavideo, huyo Dogo mlikua hamshindwi kumkamata na kumtupa selo ili utaratibu wa kisheria ufuatwe ikiwepo na kuwajulisha ndg zake!! Kama ni pombe au chai yote mngeyasoti kwa utaratibu sahihi!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo maana tusimhukumu dogo, uchunguzi ufanyike. Simbachawene hana shida kabisa na huyo dogo hatujawahi kabisa msikia ukorofi wake. Ukiangalia vizuri hao askali nina uhakika walitaka kumpiga/rushwa na walimdhalilisha ila walipogundua mtoto wa kigogo wakaona wataenda kuchomewa, ikabidi haraka wamseti.
Vipi na yule jamaa kwenye wheel chair,naye kapangwa amsingizie dogo?
Hayo mambo mbona hata kipindi cha JPM tena akiwa waziri,hatukuwahi kusikia kwa watoto wake kukosa nidhamu?
Tulee watoto vyema.
 
Ukipigwa picha ukiwa mlevi utafurahia?
Huwezi kumkuta mtoto wa Bosi wako amelewa then unashadadia kumpiga picja za kuziposti,
Mfano: Huwezi kumpiga picha mtoto wa Samia akiwa mlevi na kuziposti huko ni kukosa adabu!
Kwamba mtoto wa mkubwa huwa hafanyi makosa sio?
 
Huyu dogo kama atapelekwa gereza la keko basi tuhesabu maumivu Kwa familia yake kwasababu Kwa jinsi alivyo na mwili mteketeke sijui kama atasalimika
Umaskini unasababisha mnakuwa na roho mbaya, aende jela Kwa kesi gani? Mawakili wote hawa kazi yao ni nini? hiyo kesi siyo bailable?

Kwanza traffic case ni kesi za faini tu, na kama kutukanwa hao Polisi huwa wanatukanwa sana mahakamani na mahabusu, wasengerema tu.

Huyo mtoto amefanya kosa kama human being na siyo kama mtoto wa Simbachawene, tuache roho za kimaskini.
 
Hao Askari ni wapuuzi wooote hapo kituoni...tena wanastahili kuhamishiwa kijijini kusiko na umeme na maji

1.Dogo alikuwa mlevi na twajua pombe sio chai angeweza hata kuvua nguo je wangerusha picha zake?
Mtu yuko tungi tungi bado unamtegeshea kamera ili iweje?kama hawakuwa na nia ovu ya kumdhalilisha waziri?

2.Always protect your Superior...hao Askari baada ya kujua ni mtoto wa bosi wao na yuko mtungi wangemsukuma ndani faster kumficha toka kwenye macho ya umma.

3. Quickly wamemtaarifu mzee wake kuwa mwanao tumemficha hapa kituoni kuna msala kafanya na yuko tungi

4. Naamin Simbachawene angeagiza fanyeni Assessment waathirika wanataka nini au shilingi ngapi nimalizane hao ndani ya dakika kumi watawanyike

5. Baba yake angemaliza Jambo juu kwa juu sasa hapo ndio angejuana na mwanae njee ya macho ya umma
Kwani walijua kama ni mtoto wa mkubwa sidhani kama wangefanya hvyo.
 
Kwanza nianze kwa kukiri ya kuwa pamoja ya kuwa Mimi ni mtu mzima, na mtoto wa Askari polisi aliyetukanwa sijapokea na kumsamehe Joji Simbachawene.

Siwezi msamehe Mh Waziri Simbachawene kamwe na Sitofanya hivyo maana Baba yangu mzazi amefedheheshwa sana sana sana sana mbele ya macho ya umma.

Siwezi kubali hakika ya kuwa Baba yangu atukanwe kwani yeye ndiye aliyenizaa Mimi Nina hakika ila sio sana maana mwenye hiyo hakika ni mama yangu.

Ila nimeamua kwenda mbele zaidi baada baba kurudi nyumbani kimefanyika kikao kizito cha kujadili ilihali wa baba yetu aliyetukanwa, Ili kudhibitisha yakuwa sio kweli tusi alilotukanwa na sisi tu wanae.

Katika kikao hicho tumekubaliana yafatayo.

Kwanza watoto wote tufanyiwe vipimo vya DNA testing.

Pili Ikibanika tu Wana wa baba mmoja basi baba atukubalie sisi tufungue kesi dhidi ya Simbachawene kwa malezi yake mabaya kwa vijana nguzo ya Taifa hili.

Niliwahi jiuliza Kwanini mwendazake aliwahi mwambia Simbachawene yakuwa hakuwa Ikulu kuuza sura? Sasa naanza pata majibu.
Una stress za maisha wewe, huna la maana
 
GTs,

Kama tulivyoona kijana wa Mh. Simbachawene alivyoingia kituoni halafu kuna askari akamchoza kwa tusi. Je, hiyo ni sahihi? Je, ni kweli alitukana na je, ndiyo njia sahihi ya askari kufanya kazi?

Je, haki za kijana wa Mh. Simbachawene zilifuatwa, au alitishiwa na hao askari ili atoe rushwa ila baada ya hao askari kujua ni mtoto wa kiongozi, ikabidi wamrekodi na kumchokoza ili akasirike warekodi na kumdhalilisha?

Naamini jeshi la polisi litafanya uchunguzi ili kubaini hasa kitu gani kilitokea. Maana hao askari inaonekana walijipanga kuhakikisha dogo wana mdhalilisha.

Na kibaya walilenga kumdhalilisha Mh. Simbachawene, na huyo kijana inaonekana ni mtu mwenye heshima na anajitambua ila hao askari walimtengenezea mazingira baada ya kuona wamekosea ili kujikosha kwa jamii. Ila mtindo wa askari ndiyo huo kudhalilisha na kusumbua ili wapate rushwa.
mwanafamilia ya walamba asali tumeelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana hao askali ni waongo. Yule dogo siyo kichaa afanye hayo aliyoyafanya. Nina uhakika kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Kuna mtu mmoja siku moja Dar alikuwa hizi hoteli za uswahilini, tena ni dereva wa serikali, sasa askali wakapita walikuwa na ukaguzi wa kawaida.

Basi wakamgongea mshikaji akafungua, bahati mbaya jamaa alikuwa kaweka waleti yenye hela zimetuna na zingine zimetokezea (zilikuwa per diem na mafuta ya safari), basi yule askali alivyoona jamaa alipigwa bonge la kofi na mateke bila hata kumuuliza na akasema nyie ndiyo majambazi tunawatafuta.

Baada ya hapo jamaa kapigwa pingu na kupelekwa mahabusu, alijitahidi kujielezea wapi, akaenda kuwekwa mahabusu na waleti yake na hela zimechukuliwa.

Wakaanza kumuandikisha maelezo yeye kama jambazi. Bahati nzuri alifahamiana na watu, yule askali alifukuzwa kazi baada ya kujulikana ukweli.

Naamini watoto wa viongozi wanapaswa kupewa heshima na siyo kuwadhalilisha.
Mtoto wa kiongozi unataka na nyie tuanze kuwapa ving'ora barabarani?...haya hayo magari sita yaliyogongwa nayo kasingiziwa?

Hivi ninyi watoto wa viongozi huwa mnasali kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nianze kwa kukiri ya kuwa pamoja ya kuwa Mimi ni mtu mzima, na mtoto wa Askari polisi aliyetukanwa sijapokea na kumsamehe Joji Simbachawene.

Siwezi msamehe Mh Waziri Simbachawene kamwe na Sitofanya hivyo maana Baba yangu mzazi amefedheheshwa sana sana sana sana mbele ya macho ya umma.

Siwezi kubali hakika ya kuwa Baba yangu atukanwe kwani yeye ndiye aliyenizaa Mimi Nina hakika ila sio sana maana mwenye hiyo hakika ni mama yangu.

Ila nimeamua kwenda mbele zaidi baada baba kurudi nyumbani kimefanyika kikao kizito cha kujadili ilihali wa baba yetu aliyetukanwa, Ili kudhibitisha yakuwa sio kweli tusi alilotukanwa na sisi tu wanae.

Katika kikao hicho tumekubaliana yafatayo.

Kwanza watoto wote tufanyiwe vipimo vya DNA testing.

Pili Ikibanika tu Wana wa baba mmoja basi baba atukubalie sisi tufungue kesi dhidi ya Simbachawene kwa malezi yake mabaya kwa vijana nguzo ya Taifa hili.

Niliwahi jiuliza Kwanini mwendazake aliwahi mwambia Simbachawene yakuwa hakuwa Ikulu kuuza sura? Sasa naanza pata majibu.
Aliyetukana siyo minor mshtaki yeye.

Kwani wewe aliyekutuma umshtaki Simbachawene ni baba yako au moyo wako?

Inaonekana kama wewe nawe hauna malezi mazuri kama mtoto wa Joji
 
Kwani walijua kama ni mtoto wa mkubwa sidhani kama wangefanya hvyo.
No kitendo cha makusudi walichokifanya, kwanza Mimi nachukia sana hii tabia ya kutumia simu vibaya, hawa ndio mazuzu huwa yanapiga Picha mpaka maiti.

Mimi simu yangu mpaka nitumie camera ujuwe nimefika sehemu imenivutia sana ndio huwa natumia camera kupata kumbukumbu.
 
Ndiyo maana tusimhukumu dogo, uchunguzi ufanyike. Simbachawene hana shida kabisa na huyo dogo hatujawahi kabisa msikia ukorofi wake. Ukiangalia vizuri hao askali nina uhakika walitaka kumpiga/rushwa na walimdhalilisha ila walipogundua mtoto wa kigogo wakaona wataenda kuchomewa, ikabidi haraka wamseti.
umeambiwa Askari sio askali...huyo dogo sisi hatumfahamu...tumemfahamu baada ya tukio...muwe na adabu ninyi watoto wa wakubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom