GTs,
Kama tulivyoona kijana wa Mh. Simbachawene alivyoingia kituoni halafu kuna askari akamchoza kwa tusi. Je, hiyo ni sahihi? Je, ni kweli alitukana na je, ndiyo njia sahihi ya askari kufanya kazi?
Je, haki za kijana wa Mh. Simbachawene zilifuatwa, au alitishiwa na hao askali ili atoe rushwa ila baada ya hao askali kujua ni mtoto wa kiongozi, ikabidi wamrekodi na kumchokoza ili akasirike warekodi na kumdhalilisha?!
Naamini jeshi la polisi litafanya uchunguzi ili kubaini hasa kitu gani kilitokea. Maana hao askari inaonekana walijipanga kuhakikisha dogo wana mdhalilisha.
Na kibaya walilenga kumdhalilisha Mh. Simbachawene, na huyo kijana inaonekana ni mtu mwenye heshima na anajitambua ila hao askari walimtengenezea mazingira baada ya kuona wamekosea ili kujikosha kwa jamii. Ila mtindo wa askari ndiyo huo kudhalilisha na kusumbua ili wapate rushwa.