Namuacha kwa sababu ana matumizi makubwa ya pesa

Namuacha kwa sababu ana matumizi makubwa ya pesa

Kiherehere Gani kilikufanya uache 50k mkuu?ulikosa chenji ya 10k?next time kabla ya kurudi home tafuta chenji kabisa,kwenye pochi Sunda buku mbili kibao,Kila asbuhi unachomoa karume unateleza.Ishi nao Kwa Akili,you didn't get the memo?
 
Huyu mpezi wangu Nilitaka nimuoe ila nimeahirisha. Kila Nikiacha hela asubuhi, hata kama Ni nyingi lazima aitumie yote.

Mfano; leo niliacha elfu 50 na Ndani Kuna shehena za unga, mchele, maharagwe, mafuta ya kupikia, unga wa ngano, viungo vyote vya mboga n.k lakini nimerudi nakuta imetumika yote.

Alafu vitu vinavyoonekaza alinunua leo Ni maziwa ya unga 400g, cocoa ya elfu 5 na tea masala ya elfu 5 eti elfu 50 imeisha. Kwanza hivyo vitu vina umuhimu gani zaidi ya kuchezea hela tu? Yaani alafu kwao ni maskini hauwezi amini kwanini haheshimu pesa.

Nikimuuliza ananipandishia sauti. Nimewaza nimkatae tu.
Mfundishe Bajeti tu!!

Halafu kupandishiana kwanini!?
 
Ongea naye kwa kina mweleze hali halisi mpe muda ukiona hakuna mabadiliko ufanye maamuzi sahihi.
 
Hongera zake kupata bwana anayemwachia 50 per day hata kabla hajaolewa Wala kuzaa na huyo bwana.
Yani elfu 50 mtu anaanzisha thread. Angemnunulia Vitz si angeanzisha maandamano kabisa?
 
Back
Top Bottom