Kupanda bodaboda, kula kwa mama ntilie ugali dagaa na maigizo mengine ni chini hata ya matarajio ya aliyekuteua. Ishu za hivyo waachie wanasiasa wasio wabunifu waliozoea uongo. Wewe kufanya mbanga kama hizo ni kufanya tu uonekane huna jipya.
Ninadhani uwe tu realistic. Nenda onana na vijana wape nafasi watoe maoni yao. Huna haja ya kuwahutubia sana. Kuna mambo mengi tu yakifanyiwa kazi yatagusa maisha ya vijana. Usipoteze muda kwa drama zilizopitwa na wakati.
Kwa mfano mikopo na ruzuku kwa vijana ni kero kubwa. Kuna mambo mengi yanayotia hasira kwenye hiyo mikopo. Pia bado sheria zetu hazina unafuu kwa kijana aliye-graduate anayejitafuta kupitia kujiajiri. Kijana anatoka nje ya geti la chuo na invoice ya HESLB ila akianza kujiajiri tayari anavamiwa na mamlaka kadhaa za tozo na kodi kama nyuki bila hata kumpa grace period hata ya miezi 6 ajipange. Wasikilize vijana kisha peleka muswada bungeni sheria zifanyiwe marekebisho na kutungwa mpya kwa ajili ya vijana.
Kuigiza kuwa uko sawa na vijana wavuja jasho wanaokula ugali dagaa kila siku haina msaada kwa vijana wala serikali. Hiyo ni sawa na kuwahimiza waendelee kuwa maskini zaidi kwa kutofikiria nje ya box. Vijana pia wanataka wali kuku na kinywaji baridi. Wape matumaini ya kufika ndoto zao badala ya kuwafanya waone sawa tu kula ugali dagaa.