Unafahamu sheria ya Manunuzi wewe ama unahara hara tu hapa?
Sio unahororojoka tu soma hapo uelewe inaonekana nyie ndo wale vichwa tofali darasani,we unadhani Makonda alikarabati Ofisi from no where ebooh,!aibu yenu
Utangulizi
Mkoa wa Dar es Salaam unazo Wilaya tano ambazo ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni, Aidha ina Halmashauri sita ambazo ni Halmashauri ya Jiji, Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigambo. katika mwaka wa fedha 2016/17 Mkoa wa Dar es salaam unatarajia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Miradi inayotekelezwa mwaka 2016/2017
Katika mwaka wa fedha 2016/17, Mkoa umetengewa kiasi cha Sh. 293,119,381,000/= kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo; kati ya fedha hizo Sh. 140,878,671,000/= ni fedha za ndani ambapo Sh. 19,808,467,000/= ni Ruzuku na Sh. 121,070,204,000/= ni mapato ya ndani kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam na Sh. 152,240,710,000/= mi fedha za nje.
Miradi ya Maendeleo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa:
• Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
• Ujenzi wa Ofisi za Maafisa Tarafa
• Ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
• Ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya
• Mfuko wa kuunga mkono juhudi za wananchi
• Ufuatiliaji wa Miradi (Participatory Appraisal)
• Mfuko wa maendeleo ya ngozi (LDF)
Fedha za Nje:
• Mfuko wa pamoja wa Afya( Health Sector Dev. Support
• Ruzuku ya maendeleo ya Kilimo (DADPs)
• Usambazaji wa Maji Vijijni na Usafi wa Mazingira (RWSSP)
• Mfuko wa pamoja wa Afya (HSBF)
• Kuzuia Maambukizi ya UKIMWI (UNICEF)
• Kuzuia Maambukizi ya UKIMWI (TACAIDS)
• Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo wa Shule za Sekondari (SEDEP)
Na link hiyo:
MIRADI MKOA WA DAR ES SALAAM
WAITE NA WENZIO MNAOANZISHA NYUZI MKISHIBA VIROBA,ETI KAPATA WAPI HELA NO RESEARCH,DON'T SPEAK MAO ZE DONGI ANGEWANYONGA NYIE MNAOIBUA ISSUE MSIZO USHAHIDI NAZO[emoji36]