Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

Yote kheri. Hata wanangu nawaambia wasimwage chakula wengine wanashinda na njaa, wanakuwa Kama hawanielewi. Personally kuonyesha obvious wealth wakati wengine ni maskini, I find offensive. Hizi ni hisia zangu binafsi.
weka picha ya ofisi yako mkuu umekalia gunia ama jamvi kuonesha umaskini... joking kaka
 
Umemsahau yule ambaye alikuwa akigawa fedha makanisani?. Aliyetaka kuwa rais ili mradi tu alipize visasi vya kisiasa. Alijenga himaya ndani ya CCM kwa miaka mingi tu.

Mnajaribu kumshambulia Makonda kwa kuyasakama maisha yake binafsi badala ya kuyatazama kwa undani anayoyafanya.
Umehama katika mada.Tunazungumzia nyota ya RC inavyong'ara.
 
Maswali yaleyale walioulizwa akina wema na tuhuma zile zile walizotuhumiwa akina wema ndio hizo hizo anazotuhumiwa Makonda tena mbaya zaidi Makonda katuhumiwa bungeni na Wabunge. Kumbuka 'mke wa kaizari hapaswi kutuhumiwa'
Mkuu siku zote mti wenye matunda mazuri hupigwa mawe, umeyasoma majina ya wahusika wa madawa ya kulevya yaliyotajwa leo hii?.

Hao wa huko mjengoni ni binadamu ambao uchafu wao watu wanaufahamu vyema. Kama tuhuma zao zina nguvu na wao watumie njia zile zila anazotumia mkuu wa mkoa wa Dar katika kuziwakilisha mbele ya jamii.

Wanataja tuhuma za mkuu wa mkoa baada ya vita nzito kuanza.
 
Umehama katika mada.Tunazungumzia nyota ya RC inavyong'ara.
RC yupo vizuri tu, leo kaongeza idadi ya wahusika wa biashara haramu. Nyota yake inang'aa kweli, anataka ayaokoe maisha ya vijana wa Dar wanaoteketezwa kwa faida za utajiri wa watu wachache dhalimu.
 
RC yupo vizuri tu, leo kaongeza idadi ya wahusika wa biashara haramu. Nyota yake inang'aa kweli, anataka ayaokoe maisha ya vijana wa Dar wanaoteketezwa kwa faida za utajiri wa watu wachache dhalimu.
Mh kwa hiyo Mbowe ni teja au ndo siasa chafu za kuchafuana na kufungana.
 
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.picha zaidi za ukarabati huu ziko instagram page ya. QUALITY HOMES

View attachment 348618
Makonda hakwenda kwa waganga wa kienyeji kuutafuta Ukuu wa Mkoa hivyo hana masharti kama ninyi mliozoea kwenda kwa waganga wa kienyeji kijana. Maana mnazuiwa hata kuvaa nguo za kisasa. Andika ya maana Makonda kama Mkuu wa mkoa ana fungu lake matumizi ya ofisi hivyo subiri mkaguzi amning'inize si kwenda na visimu vyenu kupiga picha ofisi na kuifoto shop mnadhani mtamrudisha nyuma na kampeni yake aliyoigundua kutoka kwa Rodrigo Duterte....
 
Hahahahahaaaaa. Yaani mmemtafuta Makonda mmemkosa. Sasa mnaanza kuwa na wivu na ofisi yake. Imewauma sana kuona Ofisi yake inakuwa na hadhi nzuri kuliko Ofisi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mtaa wa Ufipa licha ya kupokea mamilioni ya fedha za ruzuku
Sio hivyo,una mke ,dada au mama yako aliyewahi jifungulia Chini?ufipa ni serikali?hiyo pesa igenunua vitanda na mashuka ma ngapi mwananyamala au Muhimbili?think twice poti duuuh
 
Lizaboni hebu tunza heshima ya JF,hili suala la ukarabati wa ofisi lilianzia hapa hapa JF
 
Hahahahahaaaaa. Yaani mmemtafuta Makonda mmemkosa. Sasa mnaanza kuwa na wivu na ofisi yake. Imewauma sana kuona Ofisi yake inakuwa na hadhi nzuri kuliko Ofisi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mtaa wa Ufipa licha ya kupokea mamilioni ya fedha za ruzuku
Tatizo vyeti acha maneno mengi
 
Back
Top Bottom