Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

Yaani wewe ni wa hovyo kabisa
Unataka mkuu afanyie kazi chooni?
Pale panaitwa bomani panastahili kuvunjwa kabisa kuondoa taswira s kikoloni
Serikali inaruhusu kupokea michango kutoka kwa wafadhili haswa ikiwa kama hiyo ya kurekebisha ofisi zake,hiyo ofisi sio ya makonda ni ya serikali
Chadema mnapenda sana uchafu,ndio maana lowassa kahamishia ofisi mikocheni toka ufipa kwenye banda la kuku
Swala ni nani anatoa pesa hizo? Maneno na matusi mengi hayatusaidii.
Ofisi ya Serikali huwa pesa hazitoki mfukoni kwa mtu kutengeneza. Yeye katoa wapi pesa za ukarabati?
Pili tunataka vyeti.
 
Sio unahororojoka tu soma hapo uelewe inaonekana nyie ndo wale vichwa tofali darasani,we unadhani Makonda alikarabati Ofisi from no where ebooh,!aibu yenu


Utangulizi

Mkoa wa Dar es Salaam unazo Wilaya tano ambazo ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni, Aidha ina Halmashauri sita ambazo ni Halmashauri ya Jiji, Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigambo. katika mwaka wa fedha 2016/17 Mkoa wa Dar es salaam unatarajia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.


Miradi inayotekelezwa mwaka 2016/2017

Katika mwaka wa fedha 2016/17, Mkoa umetengewa kiasi cha Sh. 293,119,381,000/= kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo; kati ya fedha hizo Sh. 140,878,671,000/= ni fedha za ndani ambapo Sh. 19,808,467,000/= ni Ruzuku na Sh. 121,070,204,000/= ni mapato ya ndani kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam na Sh. 152,240,710,000/= mi fedha za nje.

Miradi ya Maendeleo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa:

• Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
• Ujenzi wa Ofisi za Maafisa Tarafa
• Ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
• Ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya
• Mfuko wa kuunga mkono juhudi za wananchi
• Ufuatiliaji wa Miradi (Participatory Appraisal)
• Mfuko wa maendeleo ya ngozi (LDF)

Fedha za Nje:
• Mfuko wa pamoja wa Afya( Health Sector Dev. Support
• Ruzuku ya maendeleo ya Kilimo (DADPs)
• Usambazaji wa Maji Vijijni na Usafi wa Mazingira (RWSSP)
• Mfuko wa pamoja wa Afya (HSBF)
• Kuzuia Maambukizi ya UKIMWI (UNICEF)
• Kuzuia Maambukizi ya UKIMWI (TACAIDS)
• Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo wa Shule za Sekondari (SEDEP)

Na link hiyo: MIRADI MKOA WA DAR ES SALAAM
WAITE NA WENZIO MNAOANZISHA NYUZI MKISHIBA VIROBA,ETI KAPATA WAPI HELA NO RESEARCH,DON'T SPEAK MAO ZE DONGI ANGEWANYONGA NYIE MNAOIBUA ISSUE MSIZO USHAHIDI NAZO[emoji36]
Tangu mwaka jana kuna mtu alitoa jibu sahihi , wakawa wanaliruka na kuendeleza porojo zao.

Hili ni tatizo kubwa la jamii tuliyonayo kiasi kwamba hata wakija na jambo la maana , huishiwa kupuuzwa...
 
Tangu mwaka jana kuna mtu alitoa jibu sahihi , wakawa wanaliruka na kuendeleza porojo zao.

Hili ni tatizo kubwa la jamii tuliyonayo kiasi kwamba hata wakija na jambo la maana , huishiwa kupuuzwa...
Hizi za uongo tu
 
Bila shaka walimwekea na sound proof ili mungu wa Dar asibuguziwe na kelele za machinga na magari pale Ilala!!

Na huenda hatukumuelewa alipojiita mungu wa Dar,mungu haitaji kuwa na vyeti wala kutii sheria!!
 
Tuletee za kweli tuzione na si kutengeneza dhana ya kukiogopa hata kisichotisha...
Huyo uliyemnukuu hapo juu anaongelea Bajeti ya 2016/2017 ambayo huanza July,mada hii imeandikwa mwezi May 2016 kabla Bajeti haijapitishwa

Maana yake, je 2015/2016 kuna fedha ilitengwa?

Jibu hakuna pesa ilitengwa ikiwamo ya kununua hizi kompyuta za apple zenye thamani ya milioni 29 kila moja
 
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.picha zaidi za ukarabati huu ziko instagram page ya. QUALITY HOMES

View attachment 348618
Quality homes inamilikiwa na...
 
Mkuu haki ya kusema fedha imetoka wapi ni ya Makonda mwenyewe. Lakini kumbuka ukubwa wa jiji hili na vyanzo vyake vingi vya mapato.

Na sio vizuri kuhukumu kabla mtu anayehoji juu ya ni wapi fedha zimepatikana, hajafanya juhudi ya kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa mkoa, ili aweze kupewa taarifa sahihi.

Unaijua budget ya Mkuu wa mkoa lakini? Je ni halali kutumia 400 milioni kurekebisha ofi
 
Jamani mimi niulize tu hiyo OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM Iko maeneo gani ?
 
d062582e8a530099a23460725e38ae83.jpg
Kwahiyo kuna hadi studio ya mziki,
 
Angeiweka vibaya vibaya napo mngesematu, mnajema basi nyie!!!!
 
Kufikiri kimasikini ni kubaki masikini.

Kama ni kweli, safi sana Makonda.
Kwahiyo umaskini wa Taifa ni ufikiri wa kimaskini wa serikali yetu kupitia CCM tena zaidi ya miaka 50?
 
Kwahiyo umaskini wa Taifa ni ufikiri wa kimaskini wa serikali yetu kupitia CCM tena zaidi ya miaka 50?

Serikali ya Nyerere ndiyo ilitufungia kila kitu, hata chakula madukani ilikuwa mpaka uletewe na serikali, sijuwi ulikuwepo? Mwinyi akaja kubadili hayo na yote yakawa "ruksa". Kuanzia hapo umasikini wako ni wa kichwani mwako kwani baada ya Mwinyi tumeona mabilionea wa Kitanzania wakiibuka.

Wewe kimekushinda nini wenzako wameweza? Fikiri.
 
Hiyo ndo ofisi ya kijanja hata ukipigia selfie unajiona mtu kweli roho inapata. Aman
 
Nipo ofis moja ya halmashaur nafanya kazi hapo ni mbayaaaaa hakuna mfano Mpaka untia aibu kuna muda vijana kadhaa qaliandika barua ya kuacha kqzi
 
Back
Top Bottom