Imegharimiwa na Ghalib Said Mohamed na ofisi yake, yaani GSM foundation, GSM- Msasani Mall, GSm pikipiki, GSM Magororo you name it. Na ndio hao waliogharamia lile zoezi lake la kupima afya mnazo mmoja lililoishia kuwa kituko, ndio waliolipia safari zake za marekani, Dubai nk na ndio waliogarimia safari yake ya hivi sasa ya South Afrika. Wanapata nini? kwanza wanapata mtu wa kushikilia iliyokuwa nafasi ya Ridhiwana katika kusimamia maslahi ya kifedhuli ya hii Yemen Group mfano, swala zima la Silent Ocean clearing agency iliyo wahi ku paralize port yetu, pamoja na makelele yote hawa mabwana wanaendelea na ile biashara kama ilivyokuwa hapo mwanzo. Kwa kupitia makonda tender zote za halmashauri zote za DSM kwa sasa ziko mikononi mwa hawa GSM. kwa wale mapumba wanaodai eti hakuna tatizo ni waganga njaa wasio na shule wanaoshindwa kujua madhara ya muingiliano wa serikali na matapeli hawa wakimataifa wanaosafisha pesa chafu. Kuna watu bado ndani ya CCM walioshikwa pabaya na huyu bwana kiasi kwamba wanalazimika kuwasimamia waendelee kuhujumu uchumi wetu. Kama hamuamini Usalama wa taifa watupe macho, lakini wawe watu wenye integrity wataona maana ukweli uko machoni kabisa. Kumbukeni wamepewa ardhi iliyokuwa na Tanu na kujenga just next to CCM lumumba. Hizo ofisi zao ni kama sebule ya viongozi wa chama, kunywa chai, kupewa posho n,k ni aibu kabisa na hii scope nawapa mwanahalisi na Jamhuri, maana ndio wanaume wa investigative reporting na hawana woga. Hawa ni kama bomba la ulaji la hao jamaa walio next to them.Ukimjua aliyegharamia halafu wewe itakusaidia nini? Kwa mfano akiamua kutumia sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kununua computer au mapambo kuna shida? Acheni hizo.
Kwahiyo Nyerere alikuwa TLP au aliwahi kuongoza serikali kupitia CHADEMA.?Serikali ya Nyerere ndiyo ilitufungia kila kitu, hata chakula madukani ilikuwa mpaka uletewe na serikali, sijuwi ulikuwepo? Mwinyi akaja kubadili hayo na yote yakawa "ruksa". Kuanzia hapo umasikini wako ni wa kichwani mwako kwani baada ya Mwinyi tumeona mabilionea wa Kitanzania wakiibuka.
Wewe kimekushinda nini wenzako wameweza? Fikiri.
Ni GSM waligharamia kimya kimya kwa ahadi ya kuwatetea kwa mkulu wasidaiwe kodi za huko nyuma walizokwepa.Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.
Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.
Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.picha zaidi za ukarabati huu ziko instagram page ya. QUALITY HOMES
View attachment 348618
Hakuna kilichofuatwa ukarabati ulifanyka kimya kimya tu ni ukarabati wa kifisadi wa kusaka dili na tenda mbalimbali.Je Taratibu za Manunuzi ya Umma zilifuatwa
Acha ujinga hakuna mwenye wivu na hiyo Ofisi bali watu wanataka kujua GSM alipata nini baada ya kuigharamia? je? Taratibu za kutangaza tenda zilifuatwa? Ofisi za chadema na Ofisi za makonda vina uhusiano gani? Kaa ukijua kuwa Wapinzani wa makonda kwa sasa ni CCM wengi kwani familia ya marehemu kabwe ni CCM wote, akina Manji na wengineo kibao wanataka kujua Ukweli wa Daud Albert kwa kila jambo hata Umtetee vipi safari hii hachomoki kamwe.Hahahahahaaaaa. Yaani mmemtafuta Makonda mmemkosa. Sasa mnaanza kuwa na wivu na ofisi yake. Imewauma sana kuona Ofisi yake inakuwa na hadhi nzuri kuliko Ofisi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mtaa wa Ufipa licha ya kupokea mamilioni ya fedha za ruzuku
Katua jana South Africa kazuga zuga kidogo, Leo anapanda ndege kuelekea Gambia kwa Sangoma marufuku Duniani ambaye anaishi Msituni pembezoni mwa mto Gambia huko atakaa week kadhaa akifanya matambiko na kafara za kila Aina kwa sasa Daud Albert ni kigagula amepagawa anafanya vitu vya ajabu ajabu, jumapili alisali makanisa matatu tofauti huku BAKWATA wakishinda na kukesha kwake na sasa anaelekea kwa waganga sugu wa kienyeji ni hatari sana.utadhani ataishi kwenye hiyo ofisi milele.
Kwahiyo Nyerere alikuwa TLP au aliwahi kuongoza serikali kupitia CHADEMA.?
Unaulizwa sufuria unajibu karai.
Kwa kuwa umeruka swali sasa labda tufanye hivi 50-2o = 30.
Kwahiyo miaka 30 ya uongozi "msafi" tena chini ya serikali hiyo hiyo ya CCM(kama unavyotaka tuamini) na uliofungulia kila kitu, Je Tanzania ni Masikini au sio masikini?
Kama bado ni masikini ni kwa nini?
Na Ashukuriwe Mungu, laiti kama Mwalimu Nyerere, angelithubutu kuanza kuchimba kila aina ya Madini yanayopatikana hapa nadhani kila lawama na jiwe angelirushiwa yeye.
Mwisho conclude na ule msemo wako pendwa................ Ujinga?
Ni wenye akili za aina yako pekee watakuunga mkono, ila tambua ofisi za srikali zina fungu maalumu la ukarabati ,swali iweje iwe ya mkuu wa mkoa pekee wakati kuna za wilaya ndani bado zikiwa kuu kuu na je! Kwanini iwe moja tu kati ya mikoa na majiji yote nchini? Huo ndio mzizi hasa wa swali, maana serikali iko kwenye kuondoa matumizi yote yasiyo lazima ili kubana matumizi sasa kulikuwa na ulazima wowote wa msingi kufanya marekebisho hayo na kwa kiasi hicho na kwa wakati huu wa kauli mbiu ya kubana matumizi??Namuunga mkono Makonda kunadorisha office...office nyingi za umma zinatia aibu chafu na kila kitu cha kizamani...hazina hata motisha wa kufanyia kazi humo
.
Katua jana South Africa kazuga zuga kidogo, Leo anapanda ndege kuelekea Gambia kwa Sangoma marufuku Duniani ambaye anaishi Msituni pembezoni mwa mto Gambia huko atakaa week kadhaa akifanya matambiko na kafara za kila Aina kwa sasa Daud Albert ni kigagula amepagawa anafanya vitu vya ajabu ajabu, jumapili alisali makanisa matatu tofauti huku BAKWATA wakishinda na kukesha kwake na sasa anaelekea kwa waganga sugu wa kienyeji ni hatari sana.
Nyerere alipokuwepo madarakani alifuta vyama vyote vya upinzani na kubakisha chama kimoja tu, TANU. Kilichoasisiwa na wazee waliompokea Dar (siku hizo walikuwa vijana) akina Abdul Wahid Sykes, Dossa, na wengine wengi.
Kwa hiyo kuuliza kama wakati wa utawala wa Nyerere kulikuwa na TLP ni ujinga huo.
Swali sijaruka, nimekujibu uhalisia wa umasikini ulipoanzia. Wakati wa Nyerere Tanzania ilikuwa ni nchi masikini zaidi duniani kuliko zote. Leo hatuko huko.
Leo hii ukiwa kijana na hauna tatizo lolote la kiafya na unalialia kuwa u masikini basi utakuwa na tatizo kichwani mwako au ni mvivu wa kutupwa.
Kwa hiyo wewe hapo ni tajiri??
Bi mkubwa naona uko vizuri sana katika mas-ala ya balaghaNeno tajiri linatoka na neno tijara, biashara. Tajiri maana yake ni mfanya biashara, kwa maana hiyo, naam Mimi ni tajiri sana tena sana kwa kuwa biashara ni jadi yangu na nimejiingiza kwenye biashara nyingi sana, kuanzia majumba ya kupangisha, kilimo, ufugaji na kuwekeza hapa na pale.