Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo

Uzuri mataifa mengine hayajakatazwa na wao kujiita majina wayatakayo mfano G2, BRICS na kadhalika issue ni mwenye nguvu ndiyo anatrend ndiyo maana russia anamshobokea china, india maana wana hela ambazo yeye russia hana
 
Ni mipango inaongozwa na mabeberu wa marekani. Wanapanga nani wawemo G7, nani wawemo G 20. Waliwawi kuiingeza urusi G7 ikiwa G8, walipoona mrusi hachezi tune ya marekani wakamtoa ikarudi G7. Kwa hakika nchi za kibeberu tu ni mikutano yao kupanga njama kuidhibiti dunia.
Tena wakati mwingine G7 hualika nchi au nchi kuishiriki mikutano yao kwa agenda moja au mbili tu wakilenda kupata usaidizi wa nchi hiyo au hizo kwenye jambo fulani.
 
Hivi ndio WanavyotKa uamini ila uhalisia Vita tu ya Ukraine na Urusi imesababisha Dunia Nzima mfumuko wa bei, Hela haikusaidii Chochote kama hupati mahitaji ya Ki Binadamu.

Mfano Leo Congo ama Africa kwa Ujumla waamue kujifungia hakuna kitu kutoka ama kuingia Tutaishi bila tatizo lolote ila Hao unaowaita mataifa yenye nguvu ndio wataanza kuhaha.
 
Mmeshindwa japo kuondoa ukuu wa CCM unaota kuondoa ukuu wa G7.
 
Taratibu hubadilika kulongana na wakati na matakwa. Kuwa na akili basi hata kidogo sio kila kitu ni cha kukariri
 
Shida mnakariri Africa Africa, ukiwa na akili unapata mbinu mmbala wa kukabiliana na maisha ya muda huo...kaa uongozwe na wenye akili na teknolojia, umekaa unapiga porojo wenzako wako maabara wanabadikisha karatasi kutumika badala ya copper na shaba.
Kwani unadhani Afrika mkijifungia mtafaidika na nini? Mtaanza kugombania madaraka na kutandikwa na Maradhi hadi mpotee.

Wewe uliona wapi binadamu mwenye akili timamu ananunua eti kuku aliebarikiwa...mara wapo kwa Merdie kule Kenya wanazikwa porini
 
Taratibu hubadilika kulongana na wakati na matakwa. Kuwa na akili basi hata kidogo sio kila kitu ni cha kukariri
Kinabadilika kama kuna jitihada, yaani wewe uende kwa Mchungaji akuombea ili upate kazi mara uende kwa Merdie kule Kenya Sakayola ufe njaa ili uonane na Yesu...mara kwa Gwajima ununue kuku eti yenye mibaraka...tumieni akili zenu.

Wewe unadhani Tanzania itakuja lini kulingana na England ya mwaka 1990 ki maendeleo? Alafu unakataa asikupangie namna ya kuishi.

Hivi ukiacha uongo, Tanzania inaisaidia nini USA?
 
Tatizo hauoni kama jitihada zimeshaanzishwa. Unachotakiwa no kuinga mkono na kuacha ujinga
 
Huu ni msiba mkubwa kuona mwafrika anakuwa na akili kama hizi za kufurahia kupelekeshwa na kuwanyari wanaopinga huu upumbavu
 
Haya ni baadhi ya majukwaa makubwa yaliyokutana mwezi huu Russia akiwekwa pembeni.

1.G7
2.Arab league summit
3.China-Central Asia Summit
 
Sheria gani zimeshinikizwa na G7 kwa maslahi yao?
 
MASHOGA...
 
Acha kelele na makasiriko ya hovyo tafuteni hela nanyi mjiunge na hao G7!
 
Umeongea kama wale wanaume ambao mkewe anapewa lift na jirani halafu wanaume wenzake wanahoji yeye anajitetea kuwa mkewe asipopewa lift anapata shida kwenye madaladala sasa huyu mwanaume jirani amejitolea kumpeleka kazini mimi ninamshukuru sana.

Umeongea kizembe sana. Umeongea kama mtu ambaye amelewa mahaba ya mataifa ya magharibi ambayo yanajilikana wazi kuwa yananyonya mataifa changa.
 
Reactions: Ame
G7. Kila mtu anatunza pesa zake Marekani na Ulaya. Putin na matajiri wa Urusi, China, India, Afrika Kusini hata Korea ya Kaskazini (kupitia China) wametunza utajiri wao hata wa kifisadi katika benki za G7. Kwa nini G7 wasiidhibiti dunia?

Hatupendi iwe hivyo. Lakini tunapoendekeza kuongozwa na mafisadi nchini mwetu hakuna namna, lazima hao viongozi wetu watawapigia magoti G7. Hapo ndipo lilipo tatizo. Ukishindwa kujiongoza, watemi wa dunia watakuongoza.
 
Mmeshindwa japo kuondoa ukuu wa CCM unaota kuondoa ukuu wa G7.
Mimi ndiye huyo CCM sasa huoni unachekesha? Unapoona najiamini ujue na nguvu isiyo sawa na yako ndiyo sababu umeshindwa wewe kuniondoa....
 
Mbona hujauliza nani aliyachagua mataifa 5 tu Duniani kuwa ndiyo permanent UN security council member countries, na yenyewe yawe na kura ya veto?

Ufahamu kuwa hayo mataifa 7 tajiri Duniani ndiyo yanayozitegemeza taasisi zote za umoja wa mataifa, na ndiyo yanayoongoza kuyasaidia hayo mataifa mengine.

Usiishi kwenye nadharia, uuishi uhalisia. Anayekutegemeza, anayetatua matatizo mengi katika jamii yoyote ile, ndiye kiongozi wako hata kama hukumpigia kura. Maamuzi, neno lake, reaction yake, hupewa uzito na kila mmoja. Ujue kuwa hao G7 ndio unaoenda kuwaomba kukiwa na wakimbizi, ndio unaowategemea wagundue dawa kukizuka ugonjwa mpya, ndio unaowategemea wakupe chanjo za watoto wako, walipie matibabu ya magonjwa kama TB na saratani, ndio watoe na dawa za kufubaza virusi vya HIV, n.k. Na hao ndio wagunduzi wa tekinolojia mbalimbali ambazo hata ukiwa na vijisenti vyako wakiamua wakunyime, hufiki popote. Unapoenda kuwaomba tu, tayari maana yake umetambua kuwa wao ndio wakuu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…