Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo

Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo

China amewabwatukia G7 pamoja na mkubwa wao Marekani: Kawaambia hamuwezi kushinikiza matakwa yenu na sheria zenu kwetu kwa maslahi ya kwenu!! Amewagomea peupe kuwa waqo siyo world leaders bali ni kikundi tu cha watu!!

China questions ‘credibility’ of G7 members​

Beijing has accused the US-led bloc of trying to impose its will on others
China questions ‘credibility’ of G7 members

Leaders of the G7 countries in Hiroshima, Japan, May 20, 2023. © Michael Kappeler / dpa / Getty Images
The international community will not allow the US-led G7 dominate world affairs, nor will it fall in line with the pro-Western rules pushed by the group, the Chinese Foreign Ministry said in a statement on Saturday.
“China will never accept the so-called rules imposed by the few. The international community does not and will not accept the G7-dominated Western rules that seek to divide the world based on ideologies and values,” the statement read.
The Foreign Ministry went on to accuse the group of acting on behalf of “America-first” policies and attempting to impose its will on others. “That simply shows how little international credibility means to the G7,” the ministry said.

Mbona habari yenyewe ya kuchonga?. Hakuna wa kuwadindia G7. China aendelee na BRICS aache maneno.
 
Umewasikia China walivyowabwatukia hao wanaojiita "world leaders". Nikupatie kipande hiki:

Gone are the days when a handful of Western countries can just willfully meddle in other countries’ internal affairs and manipulate global affairs.

Kwa sasa kuna kizazi cha mataifa ambacho kimeshaweka msimamo kuwa hawawezi kuyumbishwa na nchi za magharibi. Nchi kama China, Urusi, Korea ya kusini, Iran, Afrika ya kusini, Ghana, Uganda, Syria, Saudi arabia, India nk,(sina uhakika kwa Tanzania)! Wamesema no thank you!! Hatuwezi kuelekezwa cha kufanya na hatuwezi kupangiwa marafiki na maadui.

Wamesema lini? Usiongee mambo ya kufikirika. Mikopo yote inatoka huko. Huyo Ghana anakaribia kufilisika kutokana na Deni la nje, halafu ndio aje aongee Nini?.
 
Umaskini wa akili ni umaskini mbaya sana!! Hizi nchi zinazodaiwa ni tajiri, utajiri wao ni wa wizi na utapeli tu!! Umaskini wa Afrika kwa mfano si umaskini halisi!! Ni umaskini wa akili!! Tuna raslimali nyingi sana!!

Huo ndio ukweli, Bado uduni wa akili unatausumbua Africa, ila kulaumu nchi zilizoendelea ndio uduni wenyewe wa akili. Rushwa na ufisadi umejaa utamlaumu mzungu?
 
Dunia tu haijajitambua nguvu zake...Hivi dunia iki gang up against hao watamtishia nani? Kama ni nuclear si na wao itawaumiza? Akili tu hizi zilizotiwa woga, siku moja tutaungana na Korea na wenye calibre kama hizo kuwaondolea huo ukuu wao imaginary waliojitengenezea

Hata china ana BRICS kila nchi ina kundi lake, lakini G7 ndio inasidia nchi nyingi hasa mikopo na nk
 
Ni mipango inaongozwa na mabeberu wa marekani. Wanapanga nani wawemo G7, nani wawemo G 20. Waliwawi kuiingeza urusi G7 ikiwa G8, walipoona mrusi hachezi tune ya marekani wakamtoa ikarudi G7. Kwa hakika nchi za kibeberu tu ni mikutano yao kupanga njama kuidhibiti dunia.
Tena wakati mwingine G7 hualika nchi au nchi kuishiriki mikutano yao kwa agenda moja au mbili tu wakilenda kupata usaidizi wa nchi hiyo au hizo kwenye jambo fulani.

Sio kweli, Russia Russia aliondolewa mwaka 2014 baada ya kuivamia Ukraine na kuichukua Crimea.
 
Hivi ndio WanavyotKa uamini ila uhalisia Vita tu ya Ukraine na Urusi imesababisha Dunia Nzima mfumuko wa bei, Hela haikusaidii Chochote kama hupati mahitaji ya Ki Binadamu.

Mfano Leo Congo ama Africa kwa Ujumla waamue kujifungia hakuna kitu kutoka ama kuingia Tutaishi bila tatizo lolote ila Hao unaowaita mataifa yenye nguvu ndio wataanza kuhaha.

Ujifungie utaishije?. Mikopo Nani atakupa. Maana nchi nyingi za Africa zinaishi kwa madeni kutoka G7.
 
Umeongea kama wale wanaume ambao mkewe anapewa lift na jirani halafu wanaume wenzake wanahoji yeye anajitetea kuwa mkewe asipopewa lift anapata shida kwenye madaladala sasa huyu mwanaume jirani amejitolea kumpeleka kazini mimi ninamshukuru sana.

Umeongea kizembe sana. Umeongea kama mtu ambaye amelewa mahaba ya mataifa ya magharibi ambayo yanajilikana wazi kuwa yananyonya mataifa changa.

Nakataa, Africa tunajinyonya wenyewe. Ufisadi ni mkubwa kwa Viongozi ila tumebaki kuwalaumu G7.
 
Sasa kuna mataifa gani mengine yenye nguvu kushinda hayo saba nguvu za kiuchumi na ushawishi
 
Nadhani hata hayo maangamizi ya Nuclear hujui kuwa kwa sasa hayawatishi hao jamaa wa G7. Kwamba USilisha unda mitambo Patriots ambayo kazi yake ni kudungua makombora yenye vichwa vya siraha za Nuclear kama yatarushwa na Kichaa Putin au Dishi Kuyumba Kiduku, makombora hayo yataduguriwa yakiwa kwenye anga za nchi zao? Hivyo makombora hayo yakirushwa watakao athirika zaidi ni Warusi, Wakorea na nchi za jirani? Lakini pia US ilisema ikiiona Urusi iko kwenye maandalizi ya kutaka kuyarusha makombora yenye kubemba vichwa vya siraha za Nuclear tu. US itavurumisha makombora yake kuyabonda makombora yenye vichwa vya siraha za Nuclear kabla ya kurushwa? Kwa Sasa endelea kuelewa kuwa US bado ni Police wa Dunia, ikifuatiwa kwa mbali na Uchina.
Aise, mbona hawamvamii sasa Mrusi kama huu ndiyo ukweli?

Hata kama mnapata good time ya hao ndugu tusiwe obsessed kiasi hichi cha kuwaabudu...Hata sisi wengine ndiyo wanaotufadhili lakini akili zetu hatuziazimii kwao, we know what is right and wrong
 
Nakataa, Africa tunajinyonya wenyewe. Ufisadi ni mkubwa kwa Viongozi ila tumebaki kuwalaumu G7.
Hapa nakubaliana na wewe...Lakini siyo kweli, Africa na dunia ikiamua G7 inaweza kufanya lolote...Hao wanatumia psychology kuaminisha watu kwamba wao ni super beings...
 
China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
 
Hapa nakubaliana na wewe...Lakini siyo kweli, Africa na dunia ikiamua G7 inaweza kufanya lolote...Hao wanatumia psychology kuaminisha watu kwamba wao ni super beings...

Sawa mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Ame
China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
Lakini kumbuka why yapo China? Cost of production ipo chini sana China, hivuo kuna comparative na competitive advantages za kupeleka hayo makampuni China, na kwa ilivyo hata wakiyahamisha lazima China itayatengeneza hybrids za hizo...So wote wawili wanaogopana japo wanatishiana nyau
 
China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
Makampuni kurudi US hayawezi gharama za uzalishaji, bidhaa zitashindwa kupambana sokoni
 
We jamaa unachekesha sana!! Unauliza nani aliwaweka!? Ni nguvu ya uchumi wanaomiliki. Yaani mwenye uwezo wa kukodi zomari ndie atachagua wimbo, we mwenzangu na mimi ukinuna au ukafurahi utajaza mwenyewe.

Ni kama vile tu moo au gsm walivyo na nguvu kwenye hivi vilabu vyenye wanachama maelfu.
Hata wewe pia unachekesha kwa akili yako china, urusi, india na baadhi ya nchi kama south korea nk haziwezi kuingia hapo, huo ni mpango tu wakuendelea wa kujiona wAo ndio kila kitu.
 
Nikupe mfano kidogo, kijijini kanisani (hasa katoliki) tajiri akitoa hoja hata kama ni pumba watu wanamshangilia kwa kusema "ndio Mzee" hata kama ni kijana mdogo. Basi hayo mataifa ni tajiri, wanastahili "ndio Mzee".
 
Nakataa, Africa tunajinyonya wenyewe. Ufisadi ni mkubwa kwa Viongozi ila tumebaki kuwalaumu G7.
Hii mada imetuzidi ukubwa tujadili mada level yetu,bajet yetu kila mwaka matumizi ya kawaida pesa ni nyingi kuliko maendeleo bajeti za kufikirika,ujasili wa kujadili nchi ambazo zimeishapitisha bajeti zao hadi 2030 na pesa zipo mezani tunaupata wapi? Tujadili kutupiana majini,wanganga wajadi,kipindupindu,utapiamlo nk
 
Kumbe wewe hujui ata maendeleo ya Indonesia, Taiwan, Japan, China, Brunei, Singapore zimechangizwa na kuwa pamoja na West? Bure kabisa...nenda China uone wanavyopigania kwenda kusoma Ulaya na USA ili kupata elimu iliyo bora...wewe unapigania kwenda kusoma China, huko Korea Kaskazini kwenyewe kwa Jeuri Mapanki amepata elimu yake West.

Ukitaka kula na wewe kubali kuliwa wakati huo unapangilia mambo yako vyema ili unachokula kidogo kije baadae kikupe jeuri ya kupunguza kuliwa.
Maendeleo yao yameletwa na Hard working, kuanzia Mapinduzi ya Kilimo na vinginevyo,

Taiwan wana dominate sana Soko la Electronic, ni rahisi kusema wamesaidiwa na Marekani kwa mvivu asietaka kusoma, ila ukisoma Historia baada ya vita vya pili vya Dunia jamaa walirudi shambani, wakafanya Reform ya Sheria watu wakapewa ardhi wakalima, kutokea kilimo viwanda vikaanza, viwanda vinavyohusiana na Kilimo kama vya Nguo na baadae kidogo kidogo waka Transform kwenda Electronics. Unaweza soma historia yao hapa


Indonesia hawa wametoka kivingine, mpaka 1998 Indonesia ni Uchumi mdogo mno ila sasa hivi wapo G20, hawaja Mcopy mtu wala kumfanya yoyote awe role model wao wameangalia dunia Inataka nini wakawapa wanachotaka, Indonesia sasa hivi ni Muuzaji mkubwa wa Nickel kwa ajili ya Battery, Anauza Kote west na China atakaefika dau anauza, Anauza Mchele, Kahawa, Mafuta, Gesi, Mawese, Rubber etc. Kifupi Indonesia ametoka kwa ku Supply raw materials.

China wanapigania Masoko yoyote yale Duniani sio ya Us na Ulaya tu, Soko kubwa la China ni Nchi za Sea, ikifuatiwa na Us halafu ndio Ulaya. Pia China yeye ndio ameforce waende waka invest kwake, ni mipango yao na Akili zao sio kwamba Usa wamemsaidia China bali mipango ya china ndio imemleta Usa pale.

Kifupi mkuu hao wa Asia ni hardworker kupita maelezo na wakipata njia ya kutokea wanafanya kazi kwa bidii hadi wanatoka, hawajakuwa matajiri kwa misaada ni cheap propaganda tu.
 
Back
Top Bottom