Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo

Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo

Kelele za Mchina zina nguvu ndogo sana. US ilipeleka pendekezo UN la kutaka China itambulike kama Taifa tajiru ili mchango wake UN uongezwe, China ilikataa katakata na kudai kuwa ukubwa wa pato la China unasababishwa na uwingi wa watu, na siyo kipato kikubwa cha wananchi wake, na kwamba wachina wengi wanaishi kwenye umaskini mkubwa.

Sasa kama hutaki kugharamia hizo taasisi za kimataifa, huwezi kuwa na nguvu sawa na hao wanaozutegemeza.
Baada ya Marekani inafuatiwa na China ndio taifa la pili kwa kuichangia UN na taasisi zake

UN regular budget 2023:

USA 🇺🇸 (22%),
China 🇨🇳 (15.25%),
Japan 🇯🇵 (8.03%)
Germany 🇩🇪 (6.11%)
 
Hapa nakubaliana na wewe...Lakini siyo kweli, Africa na dunia ikiamua G7 inaweza kufanya lolote...Hao wanatumia psychology kuaminisha watu kwamba wao ni super beings...
Mkuu, tatizo ni kwamba watu wasiosimamia tunu na maadili ya pamoja hawawezi kuungana kwa lolote. Si rahisi kwa Afrika na dunia kuamua kupambana na G7 wakati utajiri wa viongozi wetu unatunzwa katika nchi za G7 na wengi wetu tukiwa machawa wa hao viongozi mafisadi.

Ni miaka mingi Afrika imeshindwa kusimama pamoja kupigania maslahi yake. Waafrika wamekuwa wakiuzana wenyewe kwa wenyewe tangu enzi za utumwa, ukoloni hadi leo wanasaidia wageni kuhujumu rasilimali za taifa. Na huko duniani kwingi, viongozi hawana mipaka mbele ya rushwa na ufisadi. Maslahi binafsi yanazidi uzalendo kwa nchi zao.

Nchi za G7 zina viongozi na raia wengi wenye akili kubwa na misimamo imara ya kuimarisha himaya za nchi zao kwa vizazi vingi vijavyo. Hawaendekezi ujinga kama huku kwetu. Viongozi mafisadi wanadhibitiwa na mifumo imara. Hiyo ndiyo kete kuu ya G7.
 
Eti Nchi zinazoendelea kiviwanda,shortly Nchi zinazoongoza kiuchumi.Kati ya hayo mataifa 7 ukichukua uchumi wa Mataifa 5
Uchumi wa Uingereze,,Germany,Italy,Canada & France bado hawafiki uchumi wa China but cha ajabu China hayumo kwenye umoja huo.

Wazungu wanafiki sana,
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Soko kubwa la China ni Nchi za Sea, ikifuatiwa na Us halafu ndio Ulaya
🇨🇳China's top trading partners (% of China's total exports):

1.🇺🇸US: 16%
2.🇭🇰HK: 8%
3.🇯🇵Japan: 4%
4.🇰🇷S Korea: %4%
5.🇻🇳Vietnam: 4%
6.🇮🇳India: 3%
7.🇳🇱Netherlands: %3
8.🇩🇪Germany: 3%
9.🇲🇾Malaysia: %2
10.🇹🇼Taiwan: 2%
11.🇬🇧UK: 2%
12.🇸🇬S'pore: 2%
13.🇦🇺Australia: 2%
14.🇹🇭Thailand: 2%
 
Ujifungie utaishije?. Mikopo Nani atakupa. Maana nchi nyingi za Africa zinaishi kwa madeni kutoka G7.
Nimetoa mfano, wanaihitaji Africa kuliko Africa inavyowahitaji wao.

Miaka ya 1970s mfalme wa Saudia Faisal alitoa hii kauli,
images (27).jpg

Hapo ni baada ya wamarekani kutishia kulipua Visima vya mafuta vya Saudi jamaa akawajibu kwamba "ni Nyie ndio Hamuwezi kuishi bila mafuta, sisi tumetoka jangwani na wazee wetu waliishi kwa kutegemea Tende na Maziwa tunaweza kurudi kuishi kama hivyo tena"

Jiulize kitu Kimoja mkuu, Dhahabu, Almasi, Tanzanite na madini mengine nani anayahitaji sana? Mzungu ama Mu africa? Tusipochimba tunakosa nini? Pengine 5 ama 10% tu, wao wanayahitaji zaidi kuliko sisi tunavyoyahitaji

Juu hapo kama umeona Comment yangu kuhusu Indonesia, jamaa wametoboa na raw Materials tu, sidhani kama Indonesia ana utajiri hata robo tu ya Congo, ila jamaa wamelinda Resource zao na zinafaidisha nchi, ila sisi Chawa pro max tunagawa tu.
 
Hata china ana BRICS kila nchi ina kundi lake, lakini G7 ndio inasidia nchi nyingi hasa mikopo na nk
Kaka acha kuchanganya madesa,hapo issue sio mataifa yanayosaidia Nchi zingine Mikopo bali zinazoongoza kiuchumi.
Kama ni Mikopo,Mikopo iliyotolewa na China jumla ukiijumuisha utawezankujumuisha hayo mataifa 5 hapo hata wasimfikie.
Nchi kama Italy anatoa Mikopo gani.
 
Eti Nchi zinazoendelea kiviwanda,shortly Nchi zinazoongoza kiuchumi.Kati ya hayo mataifa 7 ukichukua uchumi wa Mataifa 5
Uchumi wa Uingereze,,Germany,Italy,Canada & France bado hawafiki uchumi wa China but cha ajabu China hayumo kwenye umoja huo.

Wazungu wanafiki sana,
Wanauwezo wa kutawala akili za watu...Wanaijua sana psychology ya mwanadadamu, ki kama imami ya ukristo inavyotufundisha shetani alivyo...Anatumia FEAR ku oppress powerful christians...

Ni matapeli wazuri
 
🇨🇳China's top trading partners (% of China's total exports):

1.🇺🇸US: 16%
2.🇭🇰HK: 8%
3.🇯🇵Japan: 4%
4.🇰🇷S Korea: %4%
5.🇻🇳Vietnam: 4%
6.🇮🇳India: 3%
7.🇳🇱Netherlands: %3
8.🇩🇪Germany: 3%
9.🇲🇾Malaysia: %2
10.🇹🇼Taiwan: 2%
11.🇬🇧UK: 2%
12.🇸🇬S'pore: 2%
13.🇦🇺Australia: 2%
14.🇹🇭Thailand: 2%
Vietnam, Singapore, Malyasia etc zote zinakuja kama Sea Region, inategemea na utakavyo categorize.
Screenshot_20230522-232059_1.png

Source
 
Kuna wanaoitwa "maskini jeuri". Wanajali heshima yao na hawako tayari kuiuza kwa gharama yoyote!! Watakuambia "potelea mbali na pesa yako". Watu kama mwalimu Nyerere, Robert Mugabe, Fideral Castro nk.
Labda panya wa nyumbani kwako wakuheshimu
 
Umewasikia China walivyowabwatukia hao wanaojiita "world leaders". Nikupatie kipande hiki:

Gone are the days when a handful of Western countries can just willfully meddle in other countries’ internal affairs and manipulate global affairs.

Kwa sasa kuna kizazi cha mataifa ambacho kimeshaweka msimamo kuwa hawawezi kuyumbishwa na nchi za magharibi. Nchi kama China, Urusi, Korea ya kusini, Iran, Afrika ya kusini, Ghana, Uganda, Syria, Saudi arabia, India nk,(sina uhakika kwa Tanzania)! Wamesema no thank you!! Hatuwezi kuelekezwa cha kufanya na hatuwezi kupangiwa marafiki na maadui.
Kuna tofauti ya kubweka na kung'ata...fikiri
 
Baada ya Marekani inafuatiwa na China ndio taifa la pili kwa kuichangia UN na tasisi zake

UN regular budget 2023:

USA 🇺🇸 (22%),
China 🇨🇳 (15.25%),
Japan 🇯🇵 (8.03%) and
Germany 🇩🇪 (6.11%)
Mrusi yuko kama jibwa KUBWA lisilo ng'ata hana faida kimataifa
 
ukichukua uchumi wa Mataifa 5
Uchumi wa Uingereze,,Germany,Italy,Canada & France bado hawafiki uchumi wa China but cha ajabu China hayumo kwenye umoja huo.

Wazungu wanafiki sana,
Kigezo kimojawapo cha kuwa member wa G7 eti wanasema lazima taifa lako liwe na uchumi mkubwa na la democracy na uheshimu aspects za democracy kama human rights n.k

Ndio maana wanajiita bloc of industrialized democracies

China sio nchi ya kidemokrasia ndio maana wanasema hana sifa na hajawahi hata kualikwa kwenye vikao vya G7 kama mataifa mengine yenye uchumi unaokua kwa kasi na ya kidemokrasia kama India, Brazil na South Korea yanavyoalikwa

Mwaka huu 2023 India na Brazil zilialikwa kuhudhuria G7 summit kule Japan

China kuja kuwa member wa G7 hilo sahau hata awe na uchumi kumzidi Marekani
 
Kinabadilika kama kuna jitihada, yaani wewe uende kwa Mchungaji akuombea ili upate kazi mara uende kwa Merdie kule Kenya Sakayola ufe njaa ili uonane na Yesu...mara kwa Gwajima ununue kuku eti yenye mibaraka...tumieni akili zenu.

Wewe unadhani Tanzania itakuja lini kulingana na England ya mwaka 1990 ki maendeleo? Alafu unakataa asikupangie namna ya kuishi.

Hivi ukiacha uongo, Tanzania inaisaidia nini USA?
Nakubaliana na point zako nyingi isipokuwa pale uliposema Tanzania haiisaidii chchote USA. Hivi ukae ukijua kuwa mi binafsi na watanzania kama wote hivi wanaweza kuishi (na tunaishi) bila msaada wa Marekani. So usije kujidanganya kamwe kwamba kuna model ya aina moja ya maisha ya utoshelevu hapa duniani. Vivyo hivyo kanuni za maisha na utawala wa dunia wanazoziweka Marekani na washirika wake zitakuwa na nguvu only kama umejiweka akili kutawaliwa na hizo kanuni. Mfano mdogo ni jinsi walivyotaka kuweka makanuni ya jinsi ya kuishi baada ya corona. Ukiwa mpuuzi utaishi kama wanavyotaka wao uishi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Viongozi wa G7 naona wameamua kujibatiza kama viongozi wa dunia!! Vyombo vya habari vya magharibi viko mstari wa mbele kuwatangaza kama viongozi wa dunia. Watu husema kuwa uongo ukisemwa sana, na watu wakaumezea hubadilika pole pole kuwa ukweli.

Dunia lazima ikatae sasa kuwa marais wa Marekani, kanada, uingereza, ujerumani, Italia, ufaransa,na Japani ni marais wa nchi hizo tu wala viongozi wa dunia. Vinginevyo hawa G7 wataona dunia imewakubali kama viongozi wao, na hapo ndipo watapata nguvu ya kuweka sheria na taratibu zao ili kulinda maslahi yao tu na bila kujali maslahi ya nchi zingine. BBC wanasema Zelensky kazungumza na viongozi wa dunia (world leaders).

Zelensky's talks with world leaders

View attachment 2628783
EPACopyright: EPA
In the last few minutes, we've just heard from Volodymyr Zelensky about his meetings with world leaders at the G7 summit, including the UK, Italian and Indian prime ministers.

Hasa Marekani huwa inajihesabu kama kiongozi wa dunia wakati siyo!! Dunia ina mataifa 193 yanayotambuliwa rasmi na umoja wa mataifa. Haiwezekani mataifa 7 (G7) yakajitangazia kuwa ni viongozi nwa dunia. HAPANA.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Wana dunia yao.....
 
Viongozi wa G7 naona wameamua kujibatiza kama viongozi wa dunia!! Vyombo vya habari vya magharibi viko mstari wa mbele kuwatangaza kama viongozi wa dunia. Watu husema kuwa uongo ukisemwa sana, na watu wakaumezea hubadilika pole pole kuwa ukweli.

Dunia lazima ikatae sasa kuwa marais wa Marekani, kanada, uingereza, ujerumani, Italia, ufaransa,na Japani ni marais wa nchi hizo tu wala viongozi wa dunia. Vinginevyo hawa G7 wataona dunia imewakubali kama viongozi wao, na hapo ndipo watapata nguvu ya kuweka sheria na taratibu zao ili kulinda maslahi yao tu na bila kujali maslahi ya nchi zingine. BBC wanasema Zelensky kazungumza na viongozi wa dunia (world leaders).

Zelensky's talks with world leaders

View attachment 2628783
EPACopyright: EPA
In the last few minutes, we've just heard from Volodymyr Zelensky about his meetings with world leaders at the G7 summit, including the UK, Italian and Indian prime ministers.

Hasa Marekani huwa inajihesabu kama kiongozi wa dunia wakati siyo!! Dunia ina mataifa 193 yanayotambuliwa rasmi na umoja wa mataifa. Haiwezekani mataifa 7 (G7) yakajitangazia kuwa ni viongozi nwa dunia. HAPANA.
Sawa kabisa, ni propaganda tu na kuna watu wanaamini hilo. Ukitaka kuongea na viongozi wa dunia basi ni pale unapoongea kwenye viunga vya umoja wa mataifa New York. Tatizo vyombo vyenu vya habari ni dhaifu sana na vinategemea vyombo vyao kupata habari
 
Shida haujui Dunia inavyoongozwa, G7 ndiyo wanakupangia namna ya kupata mikopo...riba na namna ya kuzitumia pia namna ya kuendana na wananchi wako.
Sasa huko Korea wanachangia nini hapa Duniani hadi wewe unufaike? Zana za kilimo yenyewe ameshindwa kuisaidia Dunia.

Hao G7 wanasisitiza sana wanasayansi kufanya kazi za utafiti kwa weledi zaidi ili maisha ya wanadamu ziboreshwe...wewe unaleta mambo ya korea kaskazini.
Unasahau kwamba hawa unaowaita viongozi wa dunia hawawezi kumpangia China, Russia, Syria wala Iran
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hao ndio wanaoishape Dunia iwe namna ilivyo. Ndio wamiliki wa karibu tekinolojia tekinolojia zote za Dunia.
Yes, wanamiliki teknolojia lakini kuna utofauti kati ya kuwa na teknolojia ikakusaidia kuwa na uwezo wa kiuchumi na kutaka kuwatawala watu wote wa dunia hii waishi kama unavyotaka waishi. Ile ya kwanza ni nguvu ya uchumi ila hii ya pili ni ulevi tu wa kikoloni.
 
Back
Top Bottom