Nani aliwadanganya CHADEMA wamponde Hayati Magufuli majukwaani!!? Hili jambo litawanyima kura miaka elfu

Hivi wapinzani kumponda Magufuli kama Magufuli bila kuihusisha ccm ni sahihi?
Wapinzani waliumizwa sana na JPM so ni haki Yao wakionyesha uchungu wao jukwaani. In fact walimkosoa sana akiwa hai why waache Sasa hivi? Hata kipindi Cha JPM nakumbuka JK alitukanwa sana majukwaani na CCM na JPM ila sikuona mkimtetea!!
Chadema kwenye uchaguzi inashindana na ccm au na Magufuli?
Inashindana na CCM ndio maana kwenye mikutano wanaongelea gharama za maisha, mgao wa umeme, mfumuko wa bei, ufisadi n.k sema tu walimkosoa JPM hapa na pale basi inabebewa bango kubwa as if ndio ilikua ajenda kuu.

Umedai hapo kwamba sukuma gang(ambapo mi ni mmojawapo japo ni mmakuwa) hawana option nyingine,kwamba wakimpa Samia(ccm) moto wakiwapa chadema moto,tafsiri yake unaridhishwa serikali ya ccm?
Kwanza sukuma gang sio wasukuma Bali ni supporters wa JPM hata Ndugai na Bashiru ni sukuma gang!!

2. Hoja hapa ni kwamba the more JPM anakosolewa na Chadema the more kura zinaporomoka. Ndio nikasema Sasa team JPM wasipompigia Chadema ndio watampigia Samia ambaye naye humkosoa JPM Kila kukicha!! Juzi mkutano wa Chadema kasema Never and Never again kurudi kwenye ukatili!!! Sasa team JPM watampigia nani hapo kura.

So kwa analysis yangu nimesema team JPM hawatopiga kura kabisa so Chadema na Samia watapambania hizo kura chache zitakazopigwa so mpaka hapo sukuma gang hawana faida yoyote kwenye uchaguzi wa 2025 unless wangekua na chama Cha siasa ndio tungesema wata take advantage.

NB: Chadema haturidhishwi na utawala wa CCM ndio maana tunataka katiba mpya Ili tuwang'oe CCM tuchukue Dola 2025. Ila kwa sukuma gang hawana option maana wakichague yeyote kati Yao bado JPM atapigwa za uso tu.
 
Vipi kile chama cha Umoja party? Kilifikia wapi?
Walishangaa wanachama wa kwanza wote TISS so wakaona wapotezee kwanza. Ilipaswa waende kimya kimya kama Maalim ACT, ila kuanza kujibrand mapema mapandikizi yakatangulizwa so kikafa hata kabla hakijaanza.

Uchaguzi wa 2025 ungenoga kama wale loyalists wa JPM wangeanzisha chama au wahamie ACT ndio hapo Sasa Uzi huu ungekua na mashiko ila kusema Chadema itapoteza kura ilihali mshindani wao ni Samia ni kujidanganya.
 
Unajua mtu kupondwa haimaanishi kwamba kweli yule mtu amekosea/hatendi ipasavyo.
Mfano mfanyakazi ''akimzibua''
mkeo usitegemee kama utamtazama vizuri hata kama kiutendaji atakuwa yupo sahihi.
Hiki ndicho anachopitia MAGUFULI.

Kwamba watu wamegeuza chuki zao binafsi na kutaka kuzifanya za kitaifa.


Mwingine ukimuuliza kwa nini Magufuli mbaya atadai alifukuza watu kazi, aliteka,aliua alizuia kufanya siasa.

Mbona hawasemi kipindi cha MKAPA mauaji kule Zanzibar? Au mauji ya kule Mtwara,Arusha na mwangosi.Au dr ULIMBOKA kipindi cha KIKWETE?

AU kuwekwa kizuizini kwa sheikh KASSIM na kuwekewa sumu.

Suala la vyeti feki alianza nalo KIKWETE(na alikuwa sahihi)ila Magufuli akaunga mkono,ila cha ajabu jumba bovu linamwangukia MAGUFULI.
Kwangu mimi Magufuli alikuwa sahihi 90% na msafi 95%
 
Ni kweli kabisa. Na mjadala mkubwa utakuwa juu ya uovu wake. Watu hawatarudia tena kuingiza shetani ikulu ya nchi
 
Mkuu siasa ni mchezo wa makosa. Sasa kama chadema inafanya makosa yote haya hasa ya kumuongelea magu vibaya na kwa jinsi ulivyoandika ni kwamba magu ana wafuasi wengi, kwa nini msianzishe chama mbadala ili ku-trap huo mtaji wa watu? Hili lingekuwa la maana sana kuliko kuwalazimisha chadema kufanya ama kutii itikadi ambazo sio itikazi zao.
 
Hoja yangu ni kwamba tuzungumzie matatizo yaliyopo tuache kupaza sauti kuhusu mtu ambaye hatunae lkni namna tunavyomuongelea sanasana tunaisaidia ccm izidi kuwa comfortable
Mkuu watu wanaposema juu ya magufuli, hamsemi yeye bali matendo yake. Yale mazuri yaendelezwe na yale mabaya asitokee mtu wa kuyarudia abadani!
 
Wapi Chadema wamemponda huyu muuaji? Magufuli alitumia mabilioni ya kodi za Watanzania kuihujumu Chadema na hakuficha chuki yake kwa Chadema sasa wao Chadema wanaposimulia madhila ya hiyo mwovu hadharani kosa liko wapi?
 
CCM haiko comfortable maana makundi mahasimu yako huko, kundi la dk Samia na sukumagang hali haiko shwari.

Na wanaomsema Magufuli kwa maovu yake siyo CHADEMA pekee, hata Zitto na ACT yake wanamsema Magufuli, CCM wanamsema Magufuli au aliyesema kulikuwa hakuna heshima bali kulikuwa na simba wa yuda anaogopwa alikuwa ni kiongozi wa CHADEMA? Tatizo lako ni unafiki wako tu, unaichukia CHADEMA na hufurahishwi na muitikio wa wananchi kwa CHADEMA baada ya kutolewa zuio la mikutano ya siasa
 
Exactly.
 
Sio kwa ukhanithi ule uliofanyika kwenye uchaguzi wa 2020. Kipenzi cha watanzania anapika mpaka idadi ya wapiga kura?! Uza ubongo huo bro.
Siasa ni mchezo wa kikubwa,nyie bado hamjakua ndio mana vilio haviwaishi.
Na kwa taarifa yenu Mh raisi SAMIA anawamezesha NDOANO kuja kushtuka mpo nchi kavu mna ''suffocate''
 
Siasa ni mchezo wa kikubwa,nyie bado hamjakua ndio mana vilio haviwaishi.
Na kwa taarifa yenu Mh raisi SAMIA anawamezesha NDOANO kuja kushtuka mpo nchi kavu mna ''suffocate''

Mngekuwa mnajua siasa mngetegemea vyombo vya dola miaka yote? Au siasa ndio huo ukhanithi?
 
Utakuwa mpumbavu no wonder, baada ya era ya apartheid kuisha Afrika ya kusini maovu ya makaburu hayakusemwa? Hakukuwa na tume ya maridhiano chini ya askofu Desmond tutu?

Legacy ya Magufuli bado ipo very strong, wanufaika wa ukatili wake dhidi ya ubinadamu mpo na mnawachukia yeyote anayezungumzia ukatili wa kutisha kuwahi kutokea kwenye ardhi ya Tanzania, na bado kundi lake la sukumagang wanatamani warudi madarakani na ndio wanamchukia dk Samia.

CHADEMA hapa ilipofika haina chuki na uhasama na dk Samia na serikali yake na wanaendelea na majadiliano ya kufikia muafaka wa maridhiano ya kisiasakitu ambacho wahafidhina hamkitaki. Ubaya wa Magufuli lazima usemwe ili taifa lisirudie tena kupata mashetani kuwa viongozi
 
Hayo mazuri ya kuua watu mnayatambua nyinyi wa kuzimu. Aliyesema kuwa kulikuwa hakuna uwajibikaji bali alikuwepo simba wa Yuda alikuwa ni CHADEMA?
Aliyetuambia mapesa ya plea bargaining yameporwa na kupelekwa kwenye akaunti China alikuwa ni CHADEMA?
Na hao wanaoiba uchaguzi wanaiba kwa matumbo ya nani?
Huwezi mpenda muuaji kama Magufuli ukawa na akili timamu
 
CHADEMA wana hali mbaya na wanzidi kuwa na hali mbaya baada ya maridhiano wanachofanya wanadhani kitawajenga kumbe kinawabomoa zaidi
 
Alichowashinda chuma alijenga Imani kubwa Kwa wanannchi wa chini ambao ndiyo wengi
 
Kwa hiyo wewe unakubaliana na matendo aliyoyafanya Magufuli kwa CHADEMA na kufuta haki ya kufanya siasa nchini?
Utakuwa na matatizo ya afya ya akili kufurahia mateso ya binadamu wenzio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…