Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu.
Leo sina mengi zaidi ya kutafuta jibu la swali langu hapo juu. Maana ukiliangalia suala hili kupitia baadhi ya waathirika wenyewe unaweza kuliona dogo, lakini kiuhalisia ni kubwa na lina madhara mabaya ya kimwili na kiakili.
Fikiria watu walikuwa wanapiga kelele na mikwara kibao kuwa wanashindwa kuonesha uhai na uimara wa vyama vyao kutokana na katazo la mikutano lililowekwa na aliekuwa Rais wetu wa awamu ya tano hayati dr John Magufuli.
Wengine wakasema kwamba vyama vyao vitaongeza uimara wake pindi Rais aliepo madarakani (Samia) atatoa katazo la mikutano na kuruhusu viongozi wao waliopo nje ya nchi kurejea kufanya siasa zao kwa njia ya amani na uhuru.
Watu hao walishindwa kujua kwamba uimara wa vyama vyao ulikuwa umejificha katika hicho hicho kimvuli cha ukatazaji mikutano. Hawakujua kwamba watanzania wa 2021 sio wale wa 2001. Watanzania wa 2001 walikuwa wanashinda juani na mvuani kupigania vyama uchwara ili vishinde uchaguzi na kuwaneemesha viongozi wao, watanzania wa 2021 wanashinda makazini na katika maeneo mbali mbali ya utafutaji rizki kwa ajili ya kutafuta ugali wao na wa familia zao. Watu hawana tena muda wa kwenda kusimama juani kusubiri mwanasiasa aje amdanganye kuwa Lowasa ni fisadi, afu kesho tena katika uchaguzi mkuu adanganywe tena kuwa Lowasa ni mtakatifu nk.
Kuruhusu mikutano kufanyika kumesababisha makamu mwenyekiti wa chama fulani kuja nchini kwa mbwembwe nyingi na mwisho wa yote akajikuta anaondoka nchini na aibu bila kuaga. Laiti kama Rais asingetoa katazo basi haya yasingetokea maana asingekuja, lakini pia ingekuwa ngumu watu kujua mbivu na mbichi za vyama hivyo.
Kuruhusu mikutano kumewavua nguo wengi akiwepo yule profesa uchwara wa uchumi pale Buguruni, na jirani yake wa Kigoma "Mr chauongo" anaepika data za uongo kuhusu uongozi wa hayati Magufuli.
Lakini pia kumewaumiza wengi ki akili na ki mwili maana kuna watu sasa wanashindwa hata kula, wengine wanaugua kabisa haswa wale ambao hawakuwa wanajua au kutarajia kujua kama vyao vyao vimeshakufa na kwamba vilikuwa vinaonekana kama vipo hai kutokana na kichaka cha ukatazaji mikutano, kingine kilichowaumiza watu zaidi ni kitendo cha makamu kuja huku wakiwa na matumaini kwamba amekujaa kukaa kusaidia na boss wake kujenga chama. Sasa jamaa ameingia gizani kimya kimya na kuwaacha chawa wake na wanachama kwa ujumla wakiwa kwenye question mark wasijue la kufanya.
Sasa najiuliza ni nani aliemshauri Rais kutoa marufuku ambayo ilikuwa inawasaidia wapinzani kujifichia kufanya propaganda zao. Haoni kama kasababisha taflani, aibu na fedheha ndani ya vyama hivyo?