Nani aliyemshauri Rais Samia jambo hili ambalo limeleta mateso na aibu kubwa mitaani na mitandaoni?

Okay, hoja iko hapa: Inakuwaje haya mazao yasiwe bei juu immediately baada ya msimu wa mavuno, badala yake yanapanda bei miezi kadhaa baada ya mavuno? Kama ni gharama za uzalishaji, Je, mwezi Julai au August 2022 mchele bomba uuzwe sh. 2500/= kwa kilo, halafu mavuno hayo hayo Februari 2023 mchele ule ule bomba uuzwe sh. 3,600/= ? Hizo gharama za mbolea zimeakisiwa lini wakati mvuno ni ule ule mmoja?
Hapa ndio nimeona umeuliza maswali yenye kueleweka.
Sasa ni hivi, bei ya mazao au kitu chochote mara nyingi hupanda kutokana na sababu kadhaa. Sababu hizo zinaweza kuwa gharama za mbolea, madawa nk.

Lakini kama gharama imekuja kupanda katika kati ya msimu wa mauzo basi huenda bei ya petrol imepanda na kusababisha gharama ya usafirishaji kuwa juu.
 
Ukielewa nilichoandika wala usingeumiza kichwa na mahasira yako
Jina lako linaendana na kile unachoandika. Ama kweli wewe ni msanii maana hoja za maana kama hizi wewe unaleta usanii wako hapa JF.
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Leo sina mengi zaidi ya kutafuta jibu la swali langu hapo juu. Maana ukiliangalia suala hili kupitia baadhi ya waathirika wenyewe unaweza kuliona dogo, lakini kiuhalisia ni kubwa na lina madhara mabaya ya kimwili na kiakili.

Fikiria watu walikuwa wanapiga kelele na mikwara kibao kuwa wanashindwa kuonesha uhai na uimara wa vyama vyao kutokana na katazo la mikutano lililowekwa na aliekuwa Rais wetu wa awamu ya tano hayati dr John Magufuli.

Wengine wakasema kwamba vyama vyao vitaongeza uimara wake pindi Rais aliepo madarakani (Samia) atatoa katazo la mikutano na kuruhusu viongozi wao waliopo nje ya nchi kurejea kufanya siasa zao kwa njia ya amani na uhuru.

Watu hao walishindwa kujua kwamba uimara wa vyama vyao ulikuwa umejificha katika hicho hicho kimvuli cha ukatazaji mikutano. Hawakujua kwamba watanzania wa 2021 sio wale wa 2001. Watanzania wa 2001 walikuwa wanashinda juani na mvuani kupigania vyama uchwara ili vishinde uchaguzi na kuwaneemesha viongozi wao, watanzania wa 2021 wanashinda makazini na katika maeneo mbali mbali ya utafutaji rizki kwa ajili ya kutafuta ugali wao na wa familia zao. Watu hawana tena muda wa kwenda kusimama juani kusubiri mwanasiasa aje amdanganye kuwa Lowasa ni fisadi, afu kesho tena katika uchaguzi mkuu adanganywe tena kuwa Lowasa ni mtakatifu nk.

Kuruhusu mikutano kufanyika kumesababisha makamu mwenyekiti wa chama fulani kuja nchini kwa mbwembwe nyingi na mwisho wa yote akajikuta anaondoka nchini na aibu bila kuaga. Laiti kama Rais asingetoa katazo basi haya yasingetokea maana asingekuja, lakini pia ingekuwa ngumu watu kujua mbivu na mbichi za vyama hivyo.

Kuruhusu mikutano kumewavua nguo wengi akiwepo yule profesa uchwara wa uchumi pale Buguruni, na jirani yake wa Kigoma "Mr chauongo" anaepika data za uongo kuhusu uongozi wa hayati Magufuli.

Lakini pia kumewaumiza wengi ki akili na ki mwili maana kuna watu sasa wanashindwa hata kula, wengine wanaugua kabisa haswa wale ambao hawakuwa wanajua au kutarajia kujua kama vyao vyao vimeshakufa na kwamba vilikuwa vinaonekana kama vipo hai kutokana na kichaka cha ukatazaji mikutano, kingine kilichowaumiza watu zaidi ni kitendo cha makamu kuja huku wakiwa na matumaini kwamba amekujaa kukaa kusaidia na boss wake kujenga chama. Sasa jamaa ameingia gizani kimya kimya na kuwaacha chawa wake na wanachama kwa ujumla wakiwa kwenye question mark wasijue la kufanya.

Sasa najiuliza ni nani aliemshauri Rais kutoa marufuku ambayo ilikuwa inawasaidia wapinzani kujifichia kufanya propaganda zao. Haoni kama kasababisha taflani, aibu na fedheha ndani ya vyama hivyo?
Watanzania watu wa ajabu sana! Sasa wewe unafikiri ilikuwa sawa kwa demokrasia yako ya uhuru wa vyama vingi kufungiwa?! Au unafikiri demokrasia ni kwa ajili ya Mbowe na Lissu?
Sasa wewe unafikiri demokrasia ni kila chama kukusanya watu juani kila siku na kuwaambia habari za kupigwa risasi 36, au ndege 10 mbovu?

Demokrasia ina njia nyingi ambazo vyama vya upinzani vinaweza kuzitumia kufikisha ujumbe kwa wananchi bila kuwasimamisha juani.

Hata huko UK kulipokomaa demokrasia au Belgium alipo Lisu leo hii hauwezi kwenda ukakuta vyama vya siasa vinakusanya watu kila siku au week viwanjani kupiga propaganda uchwara dhidi ya utawala.

Huko UK na Belgium kuna muda maalum wa kufanya mikutano na bado vyama hivyo vikapata wafuasi na wapiga kura wengi pengine zaid hata ya vyama tawala.

Sasa angalia kabla mikutano haujaruhusiwa wanachama wao na viongozi wao akiwemo Lisu walikuwa wanajua kama bado wana nguvu zile zile walizokuwa nazo miaka ile enzi za kina Dr Slaa, Lisu akakurupuka kuja akifikiri watanzania wa leo ni wale wa enzi zile. Kaja kafika na kukuta mazingira yapo tofauti sana na alivyofikiria kitu kilichomfanya aamue kukimbia mapema kabla haijamkuta aibu ile ya 2020 ambapo akijikuta anaambulia kiti kimoja tu cha ubunge na kusingizia kuwa kaibiwa kura, na pia akakimbia na kukwepa aibu huku akiwahadaa wanachama wake kuwa alitaka kuuwawa nk.

Najua kama raisi Magufuli angekuwa basi hata hii ya juzi angesema kuwa amekimbia kuuwawa. Lakini kwa mama ameona hawezi kumsingizia kwa sababu uongozi wa mama haujawahi kutiwa madoa kama ule wa JPM so angemsingizia watu wasingemuelewa kabisa.
Watu wengi sana wanateseka kwasababu ya watu kama wewe mnaojiangalia nafsi zenu tu na hamna huruma na watu wanyonge. Mkishashiba basi!
 
Jina lako linaendana na kile unachoandika. Ama kweli wewe ni msanii maana hoja za maana kama hizi wewe unaleta usanii wako hapa JF.
Sanaa haijawahi kuwa ni tatizo katika jamii. Hamna tofauti na wale ambao wanabadilisha maana ya upinde wa mvua kwa maana ya hovyo kabisa.

Jifunze kujenga hoja member mwenzangu mwenye jina la uharibifu wa mazao
 
Hao wananchi kukaa juani was a democratic process kwa wakati huo, karibu kuwa na mtazamo mpana kwamba msingi WA nchi sio chama kiwe imara au SI imara hiyo ni conditional, jua kwamba msingi WA nchi ni uhuru WA wananchi kufanya mambo Yao kwa mujibu WA sheria.
Nikwambie Rais Samia amefanya mamuzi muhimu na imara sana kwa ajili ya nchi kuruhisu nchi iendelee kukua kimocrasia.
Kuhusu uimara WA vyama kipimo sahihi ni kura wakati WA uchaguzi katika mazingira yaliyo sawa yaan free and fair elections, au labda ufanyike utafiti WA kitaalam kuonyesha wananchi Wana mrengo upi
Usipime maji kwa kutanguliza miguu yote.
 
MaCHADEMA yatazuka huko na mitusi kama mazuzu.
Ila ujumbe y amepata
 
Watanzania watu wa ajabu sana! Sasa wewe unafikiri ilikuwa sawa kwa demokrasia yako ya uhuru wa vyama vingi kufungiwa?! Au unafikiri demokrasia ni kwa ajili ya Mbowe na Lissu?

Watu wengi sana wanateseka kwasababu ya watu kama wewe mnaojiangalia nafsi zenu tu na hamna huruma na watu wanyonge. Mkishashiba basi!
Mikutano yote ya Lisu kuzugumzia kupigwa risasi 36, Mbowe kumshambulia Magufuli kule Mwanza na Zito kudai ndege 10 ziko gereji imekusaidiaje wewe mnyonge?

Je kabla ya mikutano kuruhusiwa kuna polisi walitumwa na serikali kuja kusimama mlangoni kwako kukuzuia usiende kujitafutia riziki yako?

Je kuna mfanyakazi, mfanyabiashara au mnyonge yoyote anaekula na kuishi vizuri kwa sababu ya mikutano?
 
CCM wanatumia mbinu ya "DIVIDE AND RULE" maguberi watanielewa... huyo mbowe wawe nae makini sana huyo!
Mkuu wewe unaona mbali sana ila uliowapa ushauri wameshadhibitiwa akili na huyo huyo Mbowe, so ni vigumu sana kukuelewa.

Ushahidi wa ulichokisema huo hapo videoni
 
Attachments

  • 5218795-900eac709d849ea146fff30dcf48cf3c.mp4
    4.1 MB
Mkuu wewe unaona mbali sana ila uliowapa ushauri wameshadhibitiwa akili na huyo huyo Mbowe, so ni vigumu sana kukuelewa.

Ushahidi wa ulichokisema huo hapo videoni
Kuna kitu ningekiongea hapa ila nafkiri sio sehemu sahihi. Ni hatari pia watu hawawezi kuelewa.

Itoshe tu kusema huyu bwana hayuko kama tunavyomjua. Anaicheza script yake iliyoandaliwa na wakubwa wake wa kazi 😊
 
Na hivyo ndivyo anavyojipatia kula yake 🤣🤣🤣
 
Huu ndio ukweli wenyew mkuu. Dunia ya sasa haina siri, japo sometimes watu huamua kufunika kombe ili mwanaharam apite.
Siwezi kataa. Huko kuna tapeli chama kikipewa misaada lenyewe linadai limekikopesha chama.

Kila mwaka chama kinalipa madeni hewa.
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Leo sina mengi zaidi ya kutafuta jibu la swali langu hapo juu. Maana ukiliangalia suala hili kupitia baadhi ya waathirika wenyewe unaweza kuliona dogo, lakini kiuhalisia ni kubwa na lina madhara mabaya ya kimwili na kiakili.

Fikiria watu walikuwa wanapiga kelele na mikwara kibao kuwa wanashindwa kuonesha uhai na uimara wa vyama vyao kutokana na katazo la mikutano lililowekwa na aliekuwa Rais wetu wa awamu ya tano hayati dr John Magufuli.

Wengine wakasema kwamba vyama vyao vitaongeza uimara wake pindi Rais aliepo madarakani (Samia) atatoa katazo la mikutano na kuruhusu viongozi wao waliopo nje ya nchi kurejea kufanya siasa zao kwa njia ya amani na uhuru.

Watu hao walishindwa kujua kwamba uimara wa vyama vyao ulikuwa umejificha katika hicho hicho kimvuli cha ukatazaji mikutano. Hawakujua kwamba watanzania wa 2021 sio wale wa 2001. Watanzania wa 2001 walikuwa wanashinda juani na mvuani kupigania vyama uchwara ili vishinde uchaguzi na kuwaneemesha viongozi wao, watanzania wa 2021 wanashinda makazini na katika maeneo mbali mbali ya utafutaji rizki kwa ajili ya kutafuta ugali wao na wa familia zao. Watu hawana tena muda wa kwenda kusimama juani kusubiri mwanasiasa aje amdanganye kuwa Lowasa ni fisadi, afu kesho tena katika uchaguzi mkuu adanganywe tena kuwa Lowasa ni mtakatifu nk.

Kuruhusu mikutano kufanyika kumesababisha makamu mwenyekiti wa chama fulani kuja nchini kwa mbwembwe nyingi na mwisho wa yote akajikuta anaondoka nchini na aibu bila kuaga. Laiti kama Rais asingetoa katazo basi haya yasingetokea maana asingekuja, lakini pia ingekuwa ngumu watu kujua mbivu na mbichi za vyama hivyo.

Kuruhusu mikutano kumewavua nguo wengi akiwepo yule profesa uchwara wa uchumi pale Buguruni, na jirani yake wa Kigoma "Mr chauongo" anaepika data za uongo kuhusu uongozi wa hayati Magufuli.

Lakini pia kumewaumiza wengi ki akili na ki mwili maana kuna watu sasa wanashindwa hata kula, wengine wanaugua kabisa haswa wale ambao hawakuwa wanajua au kutarajia kujua kama vyao vyao vimeshakufa na kwamba vilikuwa vinaonekana kama vipo hai kutokana na kichaka cha ukatazaji mikutano, kingine kilichowaumiza watu zaidi ni kitendo cha makamu kuja huku wakiwa na matumaini kwamba amekujaa kukaa kusaidia na boss wake kujenga chama. Sasa jamaa ameingia gizani kimya kimya na kuwaacha chawa wake na wanachama kwa ujumla wakiwa kwenye question mark wasijue la kufanya.

Sasa najiuliza ni nani aliemshauri Rais kutoa marufuku ambayo ilikuwa inawasaidia wapinzani kujifichia kufanya propaganda zao. Haoni kama kasababisha taflani, aibu na fedheha ndani ya vyama hivyo?
Vyama vyote ni uchwara tu kama maana ya uchwara ni kutokukubalika kwa wananchi !! Hata chama tawala pamoja na kutumia nguvu kubwa za kiuchumi na za kimamlaka bado kinaonyesha kimeshapoteza kabisa mvuto kwa wananchi. !! Ni kweli wananchi wengi wameshaanza kuelimika na endapo wataanza kuzijua haki zao za msingi basi kuanzia mwaka 2025 na kuendelea tutarajie kindumbwendumbwe kwenye uchaguzi Mkuu !!
 
Siwezi kataa. Huko kuna tapeli chama kikipewa misaada lenyewe linadai limekikopesha chama.

Kila mwaka chama kinalipa madeni hewa.
Walifanya kosa kumpa uongozi wa chama. Mtu yeyote anaeishi kwa hadaa mkimpa uongozi lazima awaumize.
 
Vyama vyote ni uchwara tu kama maana ya uchwara ni kutokukubalika kwa wananchi !! Hata chama tawala pamoja na kutumia nguvu kubwa za kiuchumi na za kimamlaka bado kinaonyesha kimeshapoteza kabisa mvuto kwa wananchi. !! Ni kweli wananchi wengi wameshaanza kuelimika na endapo wataanza kuzijua haki zao za msingi basi kuanzia mwaka 2025 na kuendelea tutarajie kindumbwendumbwe kwenye uchaguzi Mkuu !!
Uliloongea lina mantiki fulani, nikimaanisha kuwa kuna ukweli mwingi katika andiko lako.
 
Wewe mtoto wa mbunge wa CCM aliyepita bila kupingwe wewe, unahofia ubunge was baba yako utaota mabawa?
 
Back
Top Bottom