Nani aliyemshauri Rais Samia jambo hili ambalo limeleta mateso na aibu kubwa mitaani na mitandaoni?

Nani aliyemshauri Rais Samia jambo hili ambalo limeleta mateso na aibu kubwa mitaani na mitandaoni?

Uko sahih Sana Tena umeongea fact [emoji817] zote bila kubeba mtu au chama Cha ccm Zaid Sana uko vzr mkuu

Mm watu kam wee ndio huwa nawapa attention

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Karibu mkuu, kwa kweli hata na mimi nimefurahishwa na michango yako.

Sisi wengine huwa tunapenda kuongea ukweli bila kujali kuwa ukweli huo unamuumiza nani. Kuogopana kuambiana ukweli ndio kunapelekea mambo mengi vyamani yanakwenda shaghala bagala, kitu ambacho wengi hatupendi kukiona.

Ubarikiwe sana mkuu.
 
Watanzania watu wapuuzi sana! Sasa wewe unafikiri ilikuwa sawa kwa demokrasia yako ya uhuru wa vyama vingi kufungiwa?! Au unafikiri demokrasia ni kwa ajili ya Mbowe na Lissu?
Sasa wewe unafikiri demokrasia ni kila chama kukusanya watu juani kila siku na kuwaambia habari za kupigwa risasi 36, au ndege 10 mbovu?

Demokrasia ina njia nyingi ambazo vyama vya upinzani vinaweza kuzitumia kufikisha ujumbe kwa wananchi bila kuwasimamisha juani.

Hata huko UK kulipokomaa demokrasia au Belgium alipo Lisu leo hii hauwezi kwenda ukakuta vyama vya siasa vinakusanya watu kila siku au week viwanjani kupiga propaganda uchwara dhidi ya utawala.

Huko UK na Belgium kuna muda maalum wa kufanya mikutano na bado vyama hivyo vikapata wafuasi na wapiga kura wengi pengine zaid hata ya vyama tawala.

Sasa angalia kabla mikutano haujaruhusiwa wanachama wao na viongozi wao akiwemo Lisu walikuwa wanajua kama bado wana nguvu zile zile walizokuwa nazo miaka ile enzi za kina Dr Slaa, Lisu akakurupuka kuja akifikiri watanzania wa leo ni wale wa enzi zile. Kaja kafika na kukuta mazingira yapo tofauti sana na alivyofikiria kitu kilichomfanya aamue kukimbia mapema kabla haijamkuta aibu ile ya 2020 ambapo akijikuta anaambulia kiti kimoja tu cha ubunge na kusingizia kuwa kaibiwa kura, na pia akakimbia na kukwepa aibu huku akiwahadaa wanachama wake kuwa alitaka kuuwawa nk.

Najua kama raisi Magufuli angekuwa basi hata hii ya juzi angesema kuwa amekimbia kuuwawa. Lakini kwa mama ameona hawezi kumsingizia kwa sababu uongozi wa mama haujawahi kutiwa madoa kama ule wa JPM so angemsingizia watu wasingemuelewa kabisa.
 
Mkuu Hziyech22 huyu jamaa akiwa timamu huwa hawezi kujibu hoja nzito na za maana kama hizi.

Labda mpaka angalau anywe viloba viwili vitatu ili vimpe ujasiri wa kuja kutapika hovyo mitandaoni 🤣🤣🤣.
Kwa kitendo Cha kumuonesha hiyo video ya Mbowe umemnyamazisha kweli kweli hawa jamaa Wana ushabiki wa kijinga Sana wa vyama ndio maana unakuta hawafikiri kwa akili zao wenyewe
 
Nafahamu haujapenda,huta penda na kamwe hatutakaa ukapenda kuondolewa Katazo,unatamani usiowapenda waishi kama mashetani (matamanio ya Mtu mmoja)
Umesoma vizuri hoja yangu au umekurupuka tu kuandika?
 
Kwani uchaguzi tayari? Kuna watu wana hasira na bei za vyakula kupanda, wapo kimya kimya wanasubiri tu muda. Hapo ndipo utapima vizuri kama ondoleo la katazo la mikutano limefanya kazi gani
Ni nchi gani ambayo sasa hivi vyakula havijapanda? Mimi niko South Africa hapa bei ya vyakula imepanda mara dufu.

Kina Eric Omond juzi waliandamana na kukamatwa huko Kenya kutokana na upandaji wa bei za vyakula, Rwanda, Burundi, Uganda na mpaka huko Ulaya watu wanalalamikia ugumu wa maisha mpaka wengine wanapingana na serikali zao za magharibi kwa sababu ya kuiwekea vikwazo Urusi, wakiamini kwamba kuiwekea vikwazo Urusi na kuchochea vita vya Ukraine ndo kumesababisha hali ya maisha kuwa ngumu zaidi afu wewe leo usiejua dunia inakwendaje unakubali kupumbazwa na wanasiasa uchwara kuhusu swala la vyakula.

Ila sishangai kwa sababu mara nyingi wapinzani wamekuwa wakitumia ujinga wa wanachama wao kufanya siasa zao. Mfano ni nyie nyie mlieambiwa kuwa Lowasa ni fisadi namba 1 asiestahili kupewa uongozi hata wa udiwani, lkn baadae mkaambiwa tena mumchague huyo huyo Lowasa aje kuongoza nchi ya Tanzania, tena mnaambiwa na wale wale waliowaambiwa mwanzo kuwa hafai kuongoza hata familia yake.

Kwahiyo mpaka hapo umeshaona jinsi wanasiasa uchwara wamekuwa wakichezo na vichwa vyenu wakiamini kwamba nyinyi ni wabovu wa vichwa ambao hamuwezi kufikiria nje ya box ili kugundua uongo na unafiki wao.
 
Kwa kitendo Cha kumuonesha hiyo video ya Mbowe umemnyamazisha kweli kweli hawa jamaa Wana ushabiki wa kijinga Sana wa vyama ndio maana unakuta hawafikiri kwa akili zao wenyewe
Na ndio maana imekuwa rahisi kushikiwa akili na viongozi wao. Leo hii hakuna kijana wa upinzani ambae anaweza kuandika au kuongea jambo ambalo halitomfurahisha boss wake.

Yani kwao ili uonekane mjanja na mfia chama basi ni lazimama umpambe, umsifu na kumpambania kiongozi wao kwa hali na mali hata kama ana haribu.
 
Ni nchi gani ambayo sasa hivi vyakula havijapanda? Mimi niko South Africa hapa bei ya vyakula imepanda mara dufu.
Huo utetezi ndio utakaojibiwa majukwaani baada ya walioruhusiwa kufanya mikutano kuzungumzia upandaji wa bei za vyakula. Kabla ya ondoleo la zuio la mikutano, kusingekuwa na haja ya utetezi maana washambuliaji walishanyamazishwa kwa kuzuiwa kuongea.

By the way raia hawasikilizi mifano ya nchi nyingine, wao wanajiuliza ya nchi yao maana hivyo vilivyopanda bei vinazalishwa nchini, wala havisafirishwi kutoka Ukraine na Russia kwenye vita, au China kwenye Covid. Mchele unazalishwa Kyela, Morogoro, Mpanda na kwingineko. Maharage ndio usiseme, mahindi sijui utasema nini. Gharama za kuprocess ni mashine za kusaga na kukoboa, hazijapanda. Uzalishaji haujapanda. Lakini bei imepanda na Waziri wa Kilimo wa Serikali hii anasisitiza acha bei ipande tu! hayo yataulizwa na yatahitaji majibu!
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Leo sina mengi zaidi ya kutafuta jibu la swali langu hapo juu. Maana ukiliangalia suala hili kupitia baadhi ya waathirika wenyewe unaweza kuliona dogo, lakini kiuhalisia ni kubwa na lina madhara mabaya ya kimwili na kiakili.

Fikiria watu walikuwa wanapiga kelele na mikwara kibao kuwa wanashindwa kuonesha uhai na uimara wa vyama vyao kutokana na katazo la mikutano lililowekwa na aliekuwa Rais wetu wa awamu ya tano hayati dr John Magufuli.

Wengine wakasema kwamba vyama vyao vitaongeza uimara wake pindi Rais aliepo madarakani (Samia) atatoa katazo la mikutano na kuruhusu viongozi wao waliopo nje ya nchi kurejea kufanya siasa zao kwa njia ya amani na uhuru.

Watu hao walishindwa kujua kwamba uimara wa vyama vyao ulikuwa umejificha katika hicho hicho kimvuli cha ukatazaji mikutano. Hawakujua kwamba watanzania wa 2021 sio wale wa 2001. Watanzania wa 2001 walikuwa wanashinda juani na mvuani kupigania vyama uchwara ili vishinde uchaguzi na kuwaneemesha viongozi wao, watanzania wa 2021 wanashinda makazini na katika maeneo mbali mbali ya utafutaji rizki kwa ajili ya kutafuta ugali wao na wa familia zao. Watu hawana tena muda wa kwenda kusimama juani kusubiri mwanasiasa aje amdanganye kuwa Lowasa ni fisadi, afu kesho tena katika uchaguzi mkuu adanganywe tena kuwa Lowasa ni mtakatifu nk.

Kuruhusu mikutano kufanyika kumesababisha makamu mwenyekiti wa chama fulani kuja nchini kwa mbwembwe nyingi na mwisho wa yote akajikuta anaondoka nchini na aibu bila kuaga. Laiti kama Rais asingetoa katazo basi haya yasingetokea maana asingekuja, lakini pia ingekuwa ngumu watu kujua mbivu na mbichi za vyama hivyo.

Kuruhusu mikutano kumewavua nguo wengi akiwepo yule profesa uchwara wa uchumi pale Buguruni, na jirani yake wa Kigoma "Mr chauongo" anaepika data za uongo kuhusu uongozi wa hayati Magufuli.

Lakini pia kumewaumiza wengi ki akili na ki mwili maana kuna watu sasa wanashindwa hata kula, wengine wanaugua kabisa haswa wale ambao hawakuwa wanajua au kutarajia kujua kama vyao vyao vimeshakufa na kwamba vilikuwa vinaonekana kama vipo hai kutokana na kichaka cha ukatazaji mikutano, kingine kilichowaumiza watu zaidi ni kitendo cha makamu kuja huku wakiwa na matumaini kwamba amekujaa kukaa kusaidia na boss wake kujenga chama. Sasa jamaa ameingia gizani kimya kimya na kuwaacha chawa wake na wanachama kwa ujumla wakiwa kwenye question mark wasijue la kufanya.

Sasa najiuliza ni nani aliemshauri Rais kutoa marufuku ambayo ilikuwa inawasaidia wapinzani kujifichia kufanya propaganda zao. Haoni kama kasababisha taflani, aibu na fedheha ndani ya vyama hivyo?
Sukuma Gang mna wakati mgumu sana walahi !!!
 
Huo muda wa Upinzani wa update wapo kupngealea mambo ya kupanda kwa bei wakati hoja yao kuu ni kumuongelea marehemu
 
Huo utetezi ndio utakaojibiwa majukwaani baada ya walioruhusiwa kufanya mikutano kuzungumzia upandaji wa bei za vyakula. Kabla ya ondoleo la zuio la mikutano, kusingekuwa na haja ya utetezi maana washambuliaji walishanyamazishwa kwa kuzuiwa kuongea.
By the way raia hawasikilizi mifano ya nchi nyingine, wao wanajiuliza ya nchi yao maana hivyo vilivyopanda bei vinazalishwa nchini, wala havisafirishwi kutoka Ukraine na Russia kwenye vita, au China kwenye Covid. Mchele unazalishwa Kyela, Morogoro, Mpanda na kwingineko. Maharage ndio usiseme, mahindi sijui utasema nini. Gharama za kuprocess ni mashine za kusaga na kukoboa, hazijapanda. Uzalishaji haujapanda. Lakini bei imepanda na Waziri wa Kilimo anasisitiza ipande tu!
Dah unatia aibu ndugu yangu. Ama kweli mganga wa Mbowe ni kiboko maana upumbazwaji huu sio wa maneno ya kawaida. Lazima atakuwa alipata msaada wa kigagula ili aweze kuzitia akili zenu ndani ya box msione wala kusikia lolote linalotoka nje ya mdomo wake hata kama ni la kweli.

Pole sana mkuu kwa kusubiri wapinzani uchwara washike nchi na kukuuzia kilo ya mchele sh 500.
 
Sijaona ulipojaribu kujibu hoja zaidi ya kunishambulia. Ni dalili za mtu asiye na hoja kuizima ya mwenzake kwa kumshambulia
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Leo sina mengi zaidi ya kutafuta jibu la swali langu hapo juu. Maana ukiliangalia suala hili kupitia baadhi ya waathirika wenyewe unaweza kuliona dogo, lakini kiuhalisia ni kubwa na lina madhara mabaya ya kimwili na kiakili.

Fikiria watu walikuwa wanapiga kelele na mikwara kibao kuwa wanashindwa kuonesha uhai na uimara wa vyama vyao kutokana na katazo la mikutano lililowekwa na aliekuwa Rais wetu wa awamu ya tano hayati dr John Magufuli.

Wengine wakasema kwamba vyama vyao vitaongeza uimara wake pindi Rais aliepo madarakani (Samia) atatoa katazo la mikutano na kuruhusu viongozi wao waliopo nje ya nchi kurejea kufanya siasa zao kwa njia ya amani na uhuru.

Watu hao walishindwa kujua kwamba uimara wa vyama vyao ulikuwa umejificha katika hicho hicho kimvuli cha ukatazaji mikutano. Hawakujua kwamba watanzania wa 2021 sio wale wa 2001. Watanzania wa 2001 walikuwa wanashinda juani na mvuani kupigania vyama uchwara ili vishinde uchaguzi na kuwaneemesha viongozi wao, watanzania wa 2021 wanashinda makazini na katika maeneo mbali mbali ya utafutaji rizki kwa ajili ya kutafuta ugali wao na wa familia zao. Watu hawana tena muda wa kwenda kusimama juani kusubiri mwanasiasa aje amdanganye kuwa Lowasa ni fisadi, afu kesho tena katika uchaguzi mkuu adanganywe tena kuwa Lowasa ni mtakatifu nk.

Kuruhusu mikutano kufanyika kumesababisha makamu mwenyekiti wa chama fulani kuja nchini kwa mbwembwe nyingi na mwisho wa yote akajikuta anaondoka nchini na aibu bila kuaga. Laiti kama Rais asingetoa katazo basi haya yasingetokea maana asingekuja, lakini pia ingekuwa ngumu watu kujua mbivu na mbichi za vyama hivyo.

Kuruhusu mikutano kumewavua nguo wengi akiwepo yule profesa uchwara wa uchumi pale Buguruni, na jirani yake wa Kigoma "Mr chauongo" anaepika data za uongo kuhusu uongozi wa hayati Magufuli.

Lakini pia kumewaumiza wengi ki akili na ki mwili maana kuna watu sasa wanashindwa hata kula, wengine wanaugua kabisa haswa wale ambao hawakuwa wanajua au kutarajia kujua kama vyao vyao vimeshakufa na kwamba vilikuwa vinaonekana kama vipo hai kutokana na kichaka cha ukatazaji mikutano, kingine kilichowaumiza watu zaidi ni kitendo cha makamu kuja huku wakiwa na matumaini kwamba amekujaa kukaa kusaidia na boss wake kujenga chama. Sasa jamaa ameingia gizani kimya kimya na kuwaacha chawa wake na wanachama kwa ujumla wakiwa kwenye question mark wasijue la kufanya.

Sasa najiuliza ni nani aliemshauri Rais kutoa marufuku ambayo ilikuwa inawasaidia wapinzani kujifichia kufanya propaganda zao. Haoni kama kasababisha taflani, aibu na fedheha ndani ya vyama hivyo?
Neno la busara kwako

Badala ya kujadili vyama rivals vya kisisss, jadili hoja wanazozitoa kwrenye mikutano yao.

CCM tupunguze uzwazwa kwa sass. Hoja za wapinzani zijibiwe
 
Sijaona ulipojaribu kujibu hoja zaidi ya kunishambulia. Ni dalili za mtu asiye na hoja kuizima ya mwenzake kwa kumshambulia
Sikushambulii bali nakushangaa mpaka leo haujui ni kwanini Tanzania na dunia kwa ujumla vitu vinapanda bei.
Wewe unazungumzia habari za chakula kulimwa nyumbani lakini haujui mbolea, madawa ya kuuwa wadudu vinatoka wapi, vinapatikanaje na vinafika fikaje kwa wakulima. Kwamba havinunuliwi, haviletwi na usafiri, huo usafiri unaovileta hautumii petrol nk.

Kifupi kukuelekeza wewe ni kujichosha tu maana hata kama unaelewa ninachoandika, lazima ubadilisha na kujifanya hauelewi ili kuwafurahisha wakubwa wako wa chama ambao sera zao ni kupinga kila jambo linalofanywa na serikali liwe zuri au baya.
 
Mkuu Mr Dudumizi, nimetoka kukwambia kuhusu kuzungumzia hoja badala ya individuals (mtu au chama). Tazama hapa kuna mwingine amekushauri jambo hilo hilo

Neno la busara kwako. Badala ya kujadili vyama rivals vya kisisss, jadili hoja wanazozitoa kwrenye mikutano yao. CCM tupunguze uzwazwa kwa sass. Hoja za wapinzani zijibiwe
 
Wewe unazungumzia habari za chakula kulimwa nyumbani lakini haujui mbolea, madawa ya kuuwa wadudu vinatoka wapi, vinapatikanaje na vinafika fikaje kwa wakulima. Kwamba havinunuliwi, haviletwi na usafiri, huo usafiri unaovileta hautumii petrol nk.
Okay, hoja iko hapa: Inakuwaje haya mazao yasiwe bei juu immediately baada ya msimu wa mavuno, badala yake yanapanda bei miezi kadhaa baada ya mavuno? Kama ni gharama za uzalishaji, Je, mwezi Julai au August 2022 mchele bomba uuzwe sh. 2500/= kwa kilo, halafu mavuno hayo hayo Februari 2023 mchele ule ule bomba uuzwe sh. 3,600/= ? Hizo gharama za mbolea zimeakisiwa lini wakati mvuno ni ule ule mmoja?
 
Neno la busara kwako

Badala ya kujadili vyama rivals vya kisisss, jadili hoja wanazozitoa kwrenye mikutano yao.

CCM tupunguze uzwazwa kwa sass. Hoja za wapinzani zijibiwe
Kulikuwa na haja gani ya kujifanya mwana CCM? Kwani mada inazungumzia CCM au inazungumzia ruhusa ya vyama kufanya mikutano?

Je ungesema wewe ni chama pinzani usingesikilizwa. Inamaana siku hizi wapinzani mmeanza kujificha kwenye vimvuli vya CCM baada ya kugundua kwamba ni aibu sasa hivi mtu kuwa mpinzani na kujiita yeye ni mpinzani.

Anyway unaposema kwamba tujibu hoja za wapinzani zinazotolewa kwenye mikutano ya upinzani unamaanisha nini?
Mbona toka mikutano ianze hakuna mpinzani aliezungumzia hoja yoyote zaidi ya kusema wamepigwa risasi 36.

Sasa swala la kupigwa risasi 36 lina faida gani kwa raia wa kawaida? Kwamba mimi nichague chama fulan kwa sababu mgombea wake alipigwa risasi 36? Hiki ni kituko cha mwaka aisee.
 
Back
Top Bottom