Nani ameweka hizi bei elekezi za taxi pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere?

Nani ameweka hizi bei elekezi za taxi pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere?

Hawa jamaa wahuni sana...

Kuna Siku nimefika pale na ndege ya Mchana wakaniuliza kama wanaweza kunipeleka ninapokwenda...of course nilikuwa naelekea Posta.

Kuuliza nauli wakaniambia shilingi 45,000, nikasema ngoja nicheki nauli za Bolt...kucheki nauli ya bolt ili kuwa shilingi 9,500

Nikamwambia Kuna ndugu yangu anakuja kunifata...

Baada ya dakika 5 jamaa wa Bolt alikuwa ameshafika kunichukua maana alikuwa maeneo ya pale Kituo cha mafuta nje.

Nikawa nimeokoa zaidi ya ya shilingi 35,000

Wenzao kule Mbeya Wana shuttle zao wanakuchaji shilingi 10,000 kutoka Airport hadi Mwanjelwa/Kabwe japo mnakuwa mmepanda wasafiri 5 ama 6
So far utaratibu wa shuttle nimeukuta KIA mbeya airport nyingine km songea, mtwara, kigoma, mwanza ambako Airport iko mbali kidogo na mji hawaja adopt huu utaratibu. Ila ni utarsatuibu mzuri sana unsampa unafuu consumer pia drivers wanapata chao.
 
Wewe mjinga dunia kwa sasa ni kama kijiji... hata hao wageni sio wapumbavu wasithaminishe hiyo bei na currency yao. Watu wana mahesabu. Mwaka 2018 nilienda Dubai nikalipa kama Tsh 150k nikapelekwa Dragon Mall kutoka Deira na tukatoka hapo kwenda Dubai Mall kabla ya kurudi tena Deira. Na huko kote ni umbali wa kutosha.
Wewe ndio mpumbavu unafikiri watu hatusafiri.

Hizo bei wala sio tatizo kwa watu wanaotoka humo ni wewe tu maskini ndo unahangaika
 
Sio mimi nakupa kwa experience, ipo hivo. Naamini wapo wanaofanya hivo. Na sijasema hawapo soma vizuri nilichoandika.
Nimesema sometimes tutoe mawazo sio kila kitu mara madale sijui kimanzichNa. How do you see the prices. Nani anapanga jibu swali.
Si uongozi wao?
Mnafikiri wao wataingizia go mapato hapo?
 
Mbaya sana. Ila wanabana tu ila muda ukifika huo upumbavu utasambaratika. Kwa hali ilivyo ngumu kumchaji mtu Tsh 60k kwenda Masaki ni ushetani.
Kwa kweli haitabadilika, ndio kwanza mafuta yakipanda na zitaongezeka
Hao taxi driver wanalipia nao kupata kibali cha kupakia hapo airport, yaani wamesajiliwa.
Nadhani unaweza ukaita bolt au uber, haina shida, lakini akiingia lazima achukue tiketi getini, na saa ya kutoka lazima alipie, na hiyo gharama ataongezea juu ya nauli yako.
 
Sasa wewe una hela ya kupanda ndege halafu huna hela ndogo ya taxi?
Any way hii ni kawaida hata mambele huko, na ukiita uber au taxi binafsi, kuingia au kushusha wanachajiwa.
Hao Taxi wamesajiliwa kufanya kazi hapo tu airport, kwa hiyo lazima wajilinde kimaslahi.

Mna bahati ka airport kadogo unaweza kutembea mpaka nje barabarani, Airport kama Heathrow au Schiphol ni unatembea maili kadhaa ndio utaona nje.
Akili za kitoto kabisa na za kipumbavu kwa kuwa tunaweza panda ndege ndio twende city centre kwa 60 elfu kwa kuwa tuna hela za kichezea?

Kwa hiyo kwakuwa watu wanapata mshahara basi sukari iuzwe 30 elfu?

Huyu aliyepanga hizi bei ni mjinga na kwanza ilitakiwa kuwepo na tax mtandao zilizo sajiliwa na hapo ilikuwa sio lazima kutumia mfumo wa kizamani na kuumiza watu ..labda waseme kodi hapa ni kubwa sana!
 
Umewahi safiri wewe? Hizo bei nani kasema ndogo. 15 usd to 30 usd ni accomodation quotes za BNB nyingi bongo. Hizo bei wanapanda tu wale wasiolijua jiji.
Ndio maana taxi nyingi ukiarrive tu akikufata unanegotiate. Na zaidi utaita ndugu yako, mtu wako wa karibu au taxi mtandao. Itayokubeba kutoka ndani. Inaruhusiwa.
Hizo bei ni kali kwa kila binadamu. Usifanye wageni hawajui hela.
Sometimes muwe mnachangia nyuzi za watu sio mnaponda tu. Amehoji vizuri sana huyu mtu.
Huyo mtoto hajui hata uchungu wa hela huyo hahahaha
 
Mbali na uwepo wa taxi mtandao kama Uber, bolt nk, bado Watanzania tuko nyuma ya muda.

Karne ya 21. bado tunakomaa na namna ya zamani ya kufanya biashara. Sisemi kwamba watu wafanye taxi kizamani, kwa kuwa kuna maeneo madereva wa taxi mtandao hawataki kwenda.

Hata hivyo, walioweka bei hizi za taxi wametumia vigezo gani kuweka bei kubwa kiasi hiki. Aidha mbona maeneo mengine hayapo?

View attachment 2881681
Wamewekewa mpaka benchi la kukaa. Sijawahi kuona popote duniani taxi airport wamewekewa benchi la kukaa
 
Back
Top Bottom