Nani anaelewa mbinu ya huyu askari aliyepigwa risasi?

Nani anaelewa mbinu ya huyu askari aliyepigwa risasi?

Ila ilikuwa ni reckless move, hata alipoanza kukimbia, jamaa angekuwa serious kidogo, huyo shujaa asingekuwepo sasa.

Waliokuwa wanamfanyia covering walikuwa wanapiga off-target by far na pengine wakimlenga yeye wakidhani ndo wanam-cover😅
Kiukweli covering ilikuwa ya hali ya chini ila yote kwa yote "soldier born to die for others"
 
Wewe endelea na kejeli za nyuma ya keyboard ila ipo siku utatamani hata huyo unaemuona boya ajitokeze kukuokoa.
Humu kuna watu wanatoa maoni kwa kutumia elimu walizozipata katika filamu za rambo zilizotafsiriwa.

Pamoja na udhaifu wa Jeshi letu, nawashukuru kwa kuendelea kuwa tayari kuhatarisha maisha yao ili wengine tuendelee kula ugali na kuwakejeli tukishashiba.
 
askari lazima uwe JASIRI...huyu ni mfano wa kuigwa na wenzake...alijisahau tuu...hakuwa na risasi za akiba...alipaswa kushoot on target...na waliokuwa wanamkava....wapuuzi sana...wote hawakuwa na shabaha....sababu alitoa kichwa zaidi ya mara 2.....ni kwamba HAMZA lishaamua kufa pia....angeweza kuwasumbua sana....
 
Mimi nilichoona ni kwamba inawezekana kabisa huyo "Gaidi" alikuwa na Bullet Proof ndo maana walikuwa wanamkosa. Pia yule Askari alikuwa na Bullet proof pia namwona ni shujaa kabisa kwa jinsi alivyokwenda pale. Lakini pia kwa kuwa jamaa alikuwa ktk kibada iilikuwa sawa kutumia mabomu ya machozi kupamba na yule ili atoke. Kejeli za baadhi yenu zinanifanya niamini utafiti kuwa katika kila waTZ watano wanne wana jalada la matibabu Milemba
 
Mimi nilichoona ni kwamba inawezekana kabisa huyo "Gaidi" alikuwa na Bullet Proof ndo maana walikuwa wanamkosa. Pia yule Askari alikuwa na Bullet proof pia namwona ni shujaa kabisa kwa jinsi alivyokwenda pale. Lakini pia kwa kuwa jamaa alikuwa ktk kibada iilikuwa sawa kutumia mabomu ya machozi kupamba na yule ili atoke. Kejeli za baadhi yenu zinanifanya niamini utafiti kuwa katika kila waTZ watano wanne wana jalada la matibabu Milemba
Kuna watu mlio wa risasi anaishia kuusikia kwenye magame huko online, lakini anakuja hapa kumkejeli mtu aliyejitolea kuingia katikati ya milio ya risasi kwa faida ya wengi. Pia ieleweke kwa askari kufa kwa risasi ni sehemu ya maisha yake bila kujali kuna uzembe au hakuna.
 
Katika Jeshi, huyu ni Hero....!

Yeye ndiye aliemtoa mhalifu alikojificha kwa kumrushia Bomu la machozi (Disgusting/Tear gas)

Mwanajeshi kufa au kuua vitani ni ushindi sio Woga, angekuwa mwoga angelala nyumbani au angegoma kuingia katika mapambano

THINK
 
Huyu Sio atakua huyo wanayedai mlinzi wa kampuni binafsi aliyeuwawa?

Watu Chuma sijui wanaichukuliaje, kama ni hio badge wanivue tuu ila mbele ya chuma Sitaki unifundishe uzalendo, kaacha Dona kizembe sana.
Askar mezembe sana huyo washazoea kusumbua wapinzani tu hawana mbinu wala weredi wowote wamejawa maigizo tu , SGA na pistol wapi na wapi, SGA huwa wanatumia magobole
 
Hapo ndo naona Kuna tatizo, Police hawakujiandaa au mafunzo ya kutosha hafifu.
Askari yule Kama Kuna Askari mwenzake angefanya Cover ya kutosha Risasi kwenye kibanda mfululizo, naamini huyo angekua wa kwanza kumdungua huyo Msomali!
But kapigwa Risasi coz muda mwingi alikua anaomba Cover kwa Ishara ya mikono, mpaka anapigwa Risasi.

Hawa Police hata Movie hawaangalii? Namba unaweza kufanya Cover kwa mwenzako aliyesogea front....
Mkuu hivi unafikiri askari wengi wana shabaha ya kufanya covering.? huyo askari angeweza kuuawa na wenzake.. maana walikuwa wanarusha off target
 
Back
Top Bottom