Nani anaendesha nchi endapo Rais na Makamu wa Rais watakuwa nje ya nchi?

Nani anaendesha nchi endapo Rais na Makamu wa Rais watakuwa nje ya nchi?

Ata wanapokuwepo matatizo au maamuzi yote ya kiserikali huwa anayatafutia ufumbuzi waziri mkuu.

Bi Tozo na makamu wake kazi yao uwa kufungua miradi, kuhudhuria makongamano, kuteuliwa na kuapisha; wakimaliza hao wanakwea pipa wanapojua nje ya nchi.
Makamu anapambana sana, ndo anafanya shughuli zote za ofisini alizopaswa kufanya Rais, ukitaka kufahamu hilo nenda Dodoma
 
Katiba yetu inasemaje kuhusu chain of command, najua Rais akiwa hayupo Makamu hukaimu, sasa nimesikia Rais na yeye anaondoka ina maana Rais na Makamu wake wote wako oversees, nani anakaimu?
Autopilot. Incase kama kuna dharula Jakaya yupo msoga for further use 😀😀😀😀
 
Ukiwa mdogo utatumwa na kutumikiashwa..

Ndio Kazi ya PM,mwambie asiwataje hao huko anakotatua matatizo aone moto..
Kwani PM ndio kajiamulia hayo ni maamuzi ya civil services inavyoonekana vinginevyo ata yeye PM awezi jua wapi aende kwenye tatizo sugu; sasa wala sio la kushangaza akisema katumwa na boss wake si ajabu ata mwenyewe hajui nini kinaendelea.

Lakini lipo wazi civil service Bi Tozo wamemuachia majuku ya kwenda kukata utepe na mkasi, makongamano, kuapisha na kutoa speech za rejareja; wakipata fursa wanamtoa nje ya nchi.

Otherwise majukumu ya kuendesha nchi wamemrushia Majaliwa serikarini sema kuna maamuzi kama PM awezi fanya ni ya raisi tu.

Sio siri wanachofanya civil servants wa Ikulu kiko wazi.
 
Katiba yetu inasemaje kuhusu chain of command, najua Rais akiwa hayupo Makamu hukaimu, sasa nimesikia Rais na yeye anaondoka ina maana Rais na Makamu wake wote wako oversees, nani anakaimu?
Mkuu Kijakazi, japo unaonekana kama umeuliza Jambo dogo la kawaida, lakini kiukweli umeuliza Jambo fulani kubwa sana.

JMT kama tulivyo na Muungano unique, pia tuna hierarchy unique ya aina mbili
1. Protocol - kiprotokali.
2. Constitution - Kikatiba.

Hierarchy inayyofuatwa zaidi ni ile ya Kiprotokali na sio ya Kikatiba.

Kiprotokali hierarchy inayyofuatwa ni
  1. Rais wa JMT
  2. Makamo wa Rais
  3. Rais wa Zanzibar
  4. Waziri Mkuu
  5. Makamo wa Kwanza Zanzibar
  6. Makamo wa Pili Zanzibar
  7. Spika
  8. Jaji Mkuu
  9. Mkuu wa Majeshi
Hierarchy ya Kikatiba, Rais wa JMT ni Mkuu wa Mhimili, hivyo hierarchy ya Kikatiba iko kimihimili na sio ki protokali
  1. Rais wa JMT
  2. Makamo wa Rais wa JMT
  3. Spika wa Bunge la JMT
  4. Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Rufani ya JMT
  5. Mkuu wa Majeshi
Kwenye katiba
Waziri Mkuu is nobody, sio Mkuu wa Mhimili. Rais anapokuwa hayupo, nchi inashikwa na Mkuu wa Mhimili. Nakumbuka enzi za Spika Sitta aliwahi kuwa Kaimu Rais na Waziri Mkuu alikuwepo, kwasababu japo anaitwa ni Waziri Mkuu wa JMT, jurisdiction ni Mkuu tuu wa shughuli za serikali Bungeni.

Rais wa Zanzibar pamoja na wale Makamo wawili wa Zanzibar, they are nobodies huku na kwenye katiba yetu, anayetambuliwa ni rais tuu wa Zanzibar, wale Makamo wawili wa Zanzibar, hawatambuliwi na katiba ya JMT.

NB, Rais anapokuwa hayupo, kuna handover 2. Ya kwanza ni political handover ya nchi inakuwa chini ya Makamo wa Rais, kama hayupo Spika au Jaji Mkuu. Handover ya pili ni ya Dola, hii inaitwa Security Instruments, rais anapokuwa hayupo, usalama wa nchi unakabidhiwa Kwa Mkuu wa Majeshi, CDF, , hivyo Rais anaposafiri nje ya nchi, mtu wa mwisho kumuaga ni Mkuu wa Majeshi, na akirejea Mtu wa kwanza kumpokea ni Mkuu wa Majeshi.

Rais wa JMT ni an executive president, akiwa hayupo, hakuna amri au document yoyote inayohitaji saini ya Rais, itasainiwa na kaimu, president seal is only for president and nobody else.
P.
 
Kwani PM ndio kajiamulia hayo ni maamuzi ya civil services inavyoonekana vinginevyo ata yeye PM awezi jua wapi aende kwenye tatizo sugu; sasa wala sio la kushangaza akisema katumwa na boss wake si ajabu ata mwenyewe hajui nini kinaendelea.

Lakini lipo wazi civil service Bi Tozo wamemuachia majuku ya kwenda kukata utepe na mkasi, makongamano, kuapisha na kutoa speech za rejareja; wakipata fursa wanamtoa nje ya nchi.

Otherwise majukumu ya kuendesha nchi wamemrushia Majaliwa serikarini sema kuna maamuzi kama PM awezi fanya ni ya raisi tu.

Sio siri wanachofanya civil servants wa Ikulu kiko wazi.
Katumwa na ni Kazi yake,ndio maana huko Bungeni maswali anaulizwa yeye na Mawaziri sifa kwa Rais..

Mwambie asifanye hivyo basi aone moto.
 
Katiba yetu inasemaje kuhusu chain of command, najua Rais akiwa hayupo Makamu hukaimu, sasa nimesikia Rais na yeye anaondoka ina maana Rais na Makamu wake wote wako oversees, nani anakaimu?
Spika wa bunge
 
Katiba yetu inasemaje kuhusu chain of command, najua Rais akiwa hayupo Makamu hukaimu, sasa nimesikia Rais na yeye anaondoka ina maana Rais na Makamu wake wote wako oversees, nani anakaimu?
Mimi ni mwalimu wa uraia wa kujitolea.Kama kuna mwanafunzi mlete kwangu.
 
3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na
masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha
Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na
shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa
kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi.

(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi

c)Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya
Muungano.
Ukiangalia hapo, Waziri mkuu hakutajwa popote, ktk Nchi hii ukishafika level ya UWAZIRI MKUU, sahau kabisa kuhusu nafasi Ile ya JUU, ni MWIKO.
 
Back
Top Bottom