Nani anaendesha nchi endapo Rais na Makamu wa Rais watakuwa nje ya nchi?

Nani anaendesha nchi endapo Rais na Makamu wa Rais watakuwa nje ya nchi?

K
Mkuu Kijakazi, japo unaonekana kama umeuliza Jambo dogo la kawaida, lakini kiukweli umeuliza Jambo fulani kubwa sana.

JMT kama tulivyo na Muungano unique, pia tuna hierarchy unique ya aina mbili
1. Protocol - kiprotokali.
2. Constitution - Kikatiba.

Hierarchy inayyofuatwa zaidi ni ile ya Kiprotokali na sio ya Kikatiba.

Kiprotokali hierarchy inayyofuatwa ni
  1. Rais wa JMT
  2. Makamo wa Rais
  3. Rais wa Zanzibar
  4. Waziri Mkuu
  5. Makamo wa Kwanza Zanzibar
  6. Makamo wa Pili Zanzibar
  7. Spika
  8. Jaji Mkuu
  9. Mkuu wa Majeshi
Hierarchy ya Kikatiba, Rais wa JMT ni Mkuu wa Mhimili, hivyo hierarchy ya Kikatiba iko kimihimili na sio ki protokali
  1. Rais wa JMT
  2. Makamo wa Rais wa JMT
  3. Spika wa Bunge la JMT
  4. Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Rufani ya JMT
  5. Mkuu wa Majeshi
Kwenye katiba
Waziri Mkuu is nobody, sio Mkuu wa Mhimili. Rais anapokuwa hayupo, nchi inashikwa na Mkuu wa Mhimili. Nakumbuka enzi za Spika Sitta aliwahi kuwa Kaimu Rais na Waziri Mkuu alikuwepo, kwasababu japo anaitwa ni Waziri Mkuu wa JMT, jurisdiction ni Mkuu tuu wa shughuli za serikali Bungeni.

Rais wa Zanzibar pamoja na wale Makamo wawili wa Zanzibar, they are nobodies huku na kwenye katiba yetu, anayetambuliwa ni rais tuu wa Zanzibar, wale Makamo wawili wa Zanzibar, hawatambuliwi na katiba ya JMT.

NB, Rais anapokuwa hayupo, kuna handover 2. Ya kwanza ni political handover ya nchi inakuwa chini ya Makamo wa Rais, kama hayupo Spika au Jaji Mkuu. Handover ya pili ni ya Dola, hii inaitwa Security Instruments, rais anapokuwa hayupo, usalama wa nchi unakabidhiwa Kwa Mkuu wa Majeshi, CDF, , hivyo Rais anaposafiri nje ya nchi, mtu wa mwisho kumuaga ni Mkuu wa Majeshi, na akirejea Mtu wa kwanza kumpokea ni Mkuu wa Majeshi.

Rais wa JMT ni an executive president, akiwa hayupo, hakuna amri au document yoyote inayohitaji saini ya Rais, itasainiwa na kaimu, president seal is only for president and nobody else.
P.
Kidogo leo umeandika kitu cha ukweli
 
Katiba yetu inasemaje kuhusu chain of command, najua Rais akiwa hayupo Makamu hukaimu, sasa nimesikia Rais na yeye anaondoka ina maana Rais na Makamu wake wote wako oversees, nani anakaimu?
Waziri Mkuu Jombaaa
 
Back
Top Bottom