Nani anafaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kifo cha Balozi John Kijazi?

Nani anafaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kifo cha Balozi John Kijazi?

Hii nafasi ya Makonda!
Makonda umfikirie kwa nafasi zingine za kiasiasa kama RC na nafasi ndani ya CCM. Hizo za Ukatibu Mkuu hata wa Wizara ndogo hawezi, achilia mbali kuwa Katibu Mkuu Kiongozi (KMK). KMK ni nafasi ya kitaalam sana ya kiutendaji na busara za kumshauri Rais, na kusimamia utendaji wa watumishi wote wa umma, kusoma kwa umakini nyaraka za Baraza la Mawaziri na kushauri ipasavyo.
 
Kuna mijitu wao kutwa wanafikiria teuzi
Wenzako wako kwenye msiba na hawajaumaliza
Unataka uteuliwe

Ova
 
Huko TANAPA na Wizara ya Maliasiri na Utalii panakutosha sana wewe A. Kijazi
 
Nafasi ya Katibu Mkuu kiongozi ni nafasi inayohitaji uzoefu katika utumishi wa umma, weledi wa hali ya juu, kichwa kilichotulia na busara kubwa.

Uwe na uwezo mkubwa wa kushawishi, uelewa mkubwa na sheria za nchi, kanuni mbali mbali zinazoongoza utumishi wa serikali.

Uelewa mkubwa wa mambo ya jumla ya kitaifa, kipaji cha recruitment na kuona uwezo wa watu.. katibu mkuu kiongozi mzuri ni yule ambaye ufanisi wake, unaonekana kwa uwezo wa utekelezaji wa walio chini yake.

Kwa kifupi kama ni mzuri sana.. (of which Tanzania imebarikiwa kuwa na MaKMK bora kabisa) huwezi kujua hata kama yupo huyo kiongozi.
Tickson Nzunda Ana hizo sifa unazozisema japo sio royal wa everything,amefanya kazi ofisi ya Rais sekretariati ya maadili ya viongozi wa umma kwa mda mrefu.

Pili nafasi zote alikofanya ame excel vizuri na ni hard worker sana
 
John Kijazi hakuwa muadilufu kama munavyoaminishwa bali yeye alikuwa ni sehemu ya "oligarchy" inayoshiriki kutengeneza rushwa kwa njia ya miradi mikubwa Kisha kugawana na Meko.

Fuatilia watu kama akina Mfugale wa TANROADS, Deus Kakoko wa TPA au Charles Kicheere CAG. Wote hao wamejenga "unholy alliance" na Meko eversince yuko NW na Full Waziri kule Wizara ya miundombinu.

Jiulize katika watu wote aliowatumbua kwenye nafasi zao au kuwafikisha Mahakamani Kama kuna mtu wa TANROADS au Wizara ya Ujenzi na Miundombinu
 
Back
Top Bottom